Unakumbuka kauli gani chafu iliowahi kukukera ukajiengua from a Toxic partner?

Unakumbuka kauli gani chafu iliowahi kukukera ukajiengua from a Toxic partner?

(Aliniambia kwanza kuwa na mwanamke mrembo kama mimi ni bahati tu kwako,na hutopata mwanamke kama mimi)

Nilimjibu kuwa katika wanawake zangu kadhaa wewe ndo wa mwisho kwa kila kitu ..

.Alilia sana na mpaka sasa ananiomba msamaha
 
Sasa hapa umenifurahisha and this has always been my point! Hebu muite ndugu yako Extrovert asome hapa na ajibu halafu ndiyo utajua mimi na yeye tunapishanaga wapi!

Huyo Extrovert yeye anataka hivi! Hata yeye na mwanamke wake wote wawe wanatafuta pesa na wanachangia bills pasu kwa pasu basi kazi za ndani bado azifanye mwanamke peke yake yeye hahusiki kabisa which is totally unfair and against our african traditions!

Ndiyo maana nasema it's either mwanaume na mwanamke wasaidiane kutafuta pesa na kazi za ndani kwa pamoja au mwanaume atafute pesa peke yake na mwanamke afanye kazi za ndani peke yake! Lakini siyo eti mmoja anafanya jukumu moja ila mwingine anafanya yote mawili hiyo siyo sawa kabisa!

Na kama wewe upo hivyo basi hongera mkuu mko wachache sana! Wanaume wengi kwenye jamii zetu hizi za kiafrika wanaangukia kwenye hilo kundi nililolizungumzia hapo juu na hao ndiyo ninaowaongelea humu mara nyingi!
Wewe fanya kazi tu
 
Sawa hilo halina shida kama jamii haiwezi kuwa hivyo! Ila mbona na ninyi mnataka kulazimisha jamii ambayo mwanamke naye atakuwa anatoa pesa pasu kwa pasu sawa na mwanaume kwa kisingizio cha kwamba hayo ndiyo mapenzi wakati siyo tamaduni zetu?
Mwanamke anayekimbia kuchangia hela hata kidogo kwenye kuendesha maisha ya kawaida kila siku hafai. Ni. mbinafsi na mchoyo na hawezi kuvumilia shida hata siku 1 endapo uchumi wa baba utayumba. Ni wa kukwepa kama ukoma.
 
Sasa upande upi unaonufaika na upi unaoumia hapo? Tena mimi naona ninyi wanaume ndiyo huwa mnataka mnufaike kwenye kila kitu kinachohusiana na mapenzi!

Maana 50/50 inataka mwanaume na mwanamke wote wawe sawa kuanzia kwenye haki hadi kwenye majukumu! Ila ninyi wanaume hamtaki kuwe na haki sawa ila kwenye majukumu mnataka tuwe sawa tena majukumu yenyewe ni ya kiuchumi tu ndiyo mnataka tuwe sawa ila kwenye majukumu mengine hatuko sawa siyo?
Sasa majukumu ya hela ni sisi tunang'ang'ania au nyie watoto wa "Mwanaume sharti anihudumie"
 
Duuh sasa hapo hamuoni kuwa mnakuwa unfair kwa wanawake? Kwahiyo mkuu unataka mwanamke ndiyo afanye majukumu mengi kuliko mwanaume yaani msaidizi ndiyo afanye majukumu mengi kuliko kiongozi si ndiyo?
We unajua ubishani wako hauna mantiki. Kiufupi kaa single usijaribu hata kubeba mimba maana nafikiri unataka usaidiwe hata hilo sababu una kikazi chako.
 
Teh hivi mkuu una exposure ya maisha kweli wewe? Nakusikitikia unabishia vitu ambavyo vipo ila tu haujaviona wala haujavisikia!

Jiulize au waulize wanaume wenzio waliooa na wanaolalamika huwa wanalalamikia nini? Kwa taarifa yako kuwa single ni maamuzi yangu binafsi na wala eti siyo kwamba nimekosa mwanaume au eti wanaume hawanitongozi!
😀😀😀😀😀😀
 
Duuh mkuu unapoongelea wazazi mbona nakuwa sikuelewi kabisa yaani! Hao hao wazazi wetu si ndiyo waliishi katika misingi ya tamaduni zetu kuwa mwanaume anatafuta pesa na kuhudumia familia huku mwanamke anafanya kazi za ndani na kulea familia?

Na hicho ndicho kitu ambacho wanaume wengi wa sasa mnakipinga! Which means mnaenda kinyume na tamaduni zetu za kiafrika sasa mnataka tuwaeleweje yaani hebu kuweni wawazi chagueni kimoja mnataka tufuate tamaduni zetu za kiafrika au tufuate uzungu?
Lala ndani ijulikane moja sio unaenda job halafu hata umeme huchangii.
 
Back
Top Bottom