Unakumbuka nini katika enzi za gazeti la Sani?

Pia kulikua na gazet la Sanifu ni full KATUNI,lilikua linatolewa na busines tymz
 
stori ya maji mazito ilikuwa kiboko. Unamkuta ommy kiss, vicky na mzee nani yule sijui. Upande wa pili wimbi la kitintale. Enzi hizo Sani lilisubiriwa kama kimwana getto siku ya kwanza
 
ulieanzisha hii mada hongera sana maana umenikumbusha mbali sana kipindi kile gazeti unalisubiria mwezi mzima vituko vya kipepe na mikasa ya mapenzi ya Dr.love pimbi.
 
Namkumbuka Zena na Betina na mzee kifimbo cheza..
 

unakumbuka Pulamalaka msosi pliz, na kidan shan shao?
 
Hongereni sana
1. Philip Ndunguru
2. John Kaduma
3. Ibra Radi W.
4. Ted Marealle
na wengine wote waliowezesha jarida la Sani kutufikia enzi hizo.
 
mzee ole, obi na linda
kipepe mzee wa pori
ndumilakuwili kibaka
betina na zena wapinzani wa jadi
pimbi mr love
lodi lofa na mgongo wa chura

aisee umenifurahisha kunikumbusha ndumilakuwilii....siku moja alimuibia briefcase jamaa mmoja hv kumbe wizard...si akaanza kupuliza puto kijiweni! kila anapopuliza busha linazidi kushuka kwa ndumilakuwili....da mbona alirudisha!!!
 
aisee umenifurahisha kunikumbusha ndumilakuwilii....siku moja alimuibia briefcase jamaa mmoja hv kumbe wizard...si akaanza kupuliza puto kijiweni! kila anapopuliza busha linazidi kushuka kwa ndumilakuwili....da mbona alirudisha!!!

Halafu hii dawa ya kupuliza/kujaza ugpepo puto/tairi la baiskeli na mwizi kujaa bado ipo au zimebaki stori?
 
Dah!!!! Mmenikumbusha mbali sana miaka ya nyuma tulikuwa tunafaidi sana,ndumilakuwili alikuwa ni mwizi professional,akikuibia akachomoka humpati alikuwa na speed utadhani ndege huku nyuma shati lake la madoadoa linapepea tu,
Katika fikra zangu nilikuwaga najua Ndumilakuwili yupo dar, natamani sana maisha ya zamani kwa kweli.
 
kusoma huu uzi tu ni kama nimesoma jarida lenyewe
 
hebu imagine JF ndo ingekuwa jarida la SANI la enzi zile unahisi JF members gani wangefit kuwa wahusika wa sani??
Nani angekuwa zena na Betina?? Nani angekuwa Ndumilakuwili? Madenge? Pimbi?? Lodilofa?? Kipepe?? Sokomoko?? Na wengineo!
 
me ningekuwa Mwinyi mpeku! Natoa zangu maneno ya hekima!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…