Unakumbuka nini katika enzi za gazeti la Sani?

Nilikuwepo, japo nilikuwa dogo lakini nilijua kusoma na kuandika. Hili toleo lilikuwa linatoka mara 1 kwa mwezi mara mbili kama sikosei.

Nilikuwa moshi ambapo ndio kwetu. Nakumbuka kipindi hiko mabasi ya town trip kcmc, kiboriloni yalikuwa ni SHIMAWIMO. Yaani (SHIrika la MAendeleo WIlaya ya MOshi)

Kumbi za cinema zilikuwa mbili. ABC na Plaza Cinema. Nilikuwa sikosi kwenda pale plaza kila jumapili saa nne kuangalia sinema. Hata kama sijapewa hela na mshua lazima niende ongalao niambulie fungulia mbwa.

Masteling wa wakati huo, Amitha Batchan, Mithuny Chakraborty, Rish Kopoor,Rajesh Kumar, Denzolpa, kwa upande wa kina mama walikuwepo kina Jaya, Hemma Malini, nk.

Movie nazozikumbika, Nasseb,Amne Samne, nk. Kotambo sana.

Kumbi za disco zilikuwa ni Vijana club, Libert hotel iliyokuwa karibu na green view ambayo ilikuja kuungua baadae.

Mafuta ya kupaka wakati huo ni YOU na YOLANDA yaliyokuwa kwenye mkebe. Mengine ni rays, Ashanti. Wajanja walikuwa wanavaa jenzi na rabber mtoni kama Ascot. Suruali za kitambaa zilikuwa Cacha rell, Mr Dio nk.

Wahusika wa kuu kwenye kazeti la Sani. Kipepe, Lodi lofa, Sokomoka, Pimbi, Madenge,na Yule mpiga roba nani sijui nimemsahau.

Mc Sukununu.

Hadithi zilizowahi kutamba wakati huo kwenye gazeti la sani na mtunzi akiwa marehemu Hammie Rajab ni pamoja na Pumbazo La moyo, Usiku waGiza ya Joyce na Dalanda na kibibi Gula.

Dah muda umeenda aisee, ila kama juzi tu.
Heshima yako Mhenga.
 
Kutili plaza? Kutili kabati ya mbeho? Enzi hizo ukitaka kuoa mchagga? Tv ilikuwa ni chuo cha polisi na chuo cha ushirika tu. Umesahau YMCA. Balozi wa Tanzania nchini Kuwait alikuwa form four chopra sec (mwanza sec school).
Ni ya kweli hayo kwamba Balozi wa TZ - KUWAIT alikuwa Mwaseco? Maana nimemaliza hapo form four 1989. Na 1984 nilikuta tayari inaitwa Mwanza sec.
 
Alimiza form four 1986 mwaseco. Alifundishwa Fizikia na mwl Mugyabuso na mahesabu mwl Mkono; mwl Kashusura history etc! Walikuwa na Marehemu Pendo etc Mwl Deya akiwa mwl mkuu kama sikosei.
 
Itakuwa sahihi maana mi nilianza form one 1986. Hao walimu wote niliwakuta na Mwl. Kashushura kwasasa ni jirani yangu ninapoishi alinifundisha geography. Mkono alinifundisha Additional Maths kwasasa ni marehemu.
 
Mwaka 1987, ulikuwa LY ....LAST YEAR ....tukiita hivyo enzi hizo, kumaliza Elimu ya Msingi
 
Nilikuwepo, japo nilikuwa dogo lakini nilijua kusoma na kuandika. Hili toleo lilikuwa linatoka mara 1 kwa mwezi mara mbili kama sikosei.

Nilikuwa moshi ambapo ndio kwetu. Nakumbuka kipindi hiko mabasi ya town trip kcmc, kiboriloni yalikuwa ni SHIMAWIMO. Yaani (SHIrika la MAendeleo WIlaya ya MOshi)

Kumbi za cinema zilikuwa mbili. ABC na Plaza Cinema. Nilikuwa sikosi kwenda pale plaza kila jumapili saa nne kuangalia sinema. Hata kama sijapewa hela na mshua lazima niende ongalao niambulie fungulia mbwa.

Masteling wa wakati huo, Amitha Batchan, Mithuny Chakraborty, Rish Kopoor,Rajesh Kumar, Denzolpa, kwa upande wa kina mama walikuwepo kina Jaya, Hemma Malini, nk.

Movie nazozikumbika, Nasseb,Amne Samne, nk. Kotambo sana.

Kumbi za disco zilikuwa ni Vijana club, Libert hotel iliyokuwa karibu na green view ambayo ilikuja kuungua baadae.

Mafuta ya kupaka wakati huo ni YOU na YOLANDA yaliyokuwa kwenye mkebe. Mengine ni rays, Ashanti. Wajanja walikuwa wanavaa jenzi na rabber mtoni kama Ascot. Suruali za kitambaa zilikuwa Cacha rell, Mr Dio nk.

Wahusika wa kuu kwenye kazeti la Sani. Kipepe, Lodi lofa, Sokomoka, Pimbi, Madenge,na Yule mpiga roba nani sijui nimemsahau.

Mc Sukununu.

Hadithi zilizowahi kutamba wakati huo kwenye gazeti la sani na mtunzi akiwa marehemu Hammie Rajab ni pamoja na Pumbazo La moyo, Usiku waGiza ya Joyce na Dalanda na kibibi Gula.

Dah muda umeenda aisee, ila kama juzi tu.
Dah safi sana mkuu, umenikumbusha mbali sana, enzi za Plaza, PICHA MBILI, KIINGILIO KIMOJA. Hiyo inaanzia sa 4 mpk liamba, dah MO TOWN tuliitendea haki sana na pale ABC kama waenda Railway Station
 
Back
Top Bottom