Unakumbuka nini kuanzia Mwaka 1998 hadi 2000?

Unakumbuka nini kuanzia Mwaka 1998 hadi 2000?

Mimi binafsi nimezaliwa mwaka 1988 wakati ambao Tanganyika & Zanzibar zilikuwa kwenye muungano uliozaa Tanzania.


Wiki ikiyopita niliamua kujipa likizo binafsi,kwakuwa ninafanya kazi nyingi kwa takribani mwaka mzima bila kupumzika,nikaona huu ni muda muafaka wa kuipumzisha akili!


Hivi sasa ninapoandika huu uzi nipo hapa hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) nikiwa nimetulia zangu nikipata mvinyo baridi kabisa kutoka pale Dodoma!.

Nikiwa huku,mara zote nimekuwa nikipenda kusikiliza ngoma za miaka ya nyuma kutoka mamtoni,ngoma ambazo kizazi cha sasa kinaona kama zimepitwa na wakati!

Ahahahahaaa!,Vijana wa kisasa wameyakosa mambo matamu mnooo ambayo enzi zetu sisi tuliya-enjoy!
Nimekumbukia sana miaka ya 1998 hadi 2000!.Mwaka 1998 mimi binafsi nilikuwa nina miaka 10,aiseee nimekumbuka mambo mengi sana yanayohusu burudani nikiwa na washikaji zangu ambao wengi wao kwasasa ni Marehemu!.Kuanzia mwaka huo wa 1998 hadi mwaka 2001 wasanii wa marekani ndiyo waliongoza kwa kutoa Hitsongs ulimwenguni!

Nakumbukia sana wimbo wa I need a Girl wake P. Diddy feat Usher & Loon ambao ulitoka mwaka 2001,Huu wimbo umenikumbusha mbali sana kiasi kwamba hadi machozi yamenitoka kwasababu nawakumbikia washikaji zangu wengi ambao nilikuwa nazunguka nao kwenye Peugeot 306 ya home,wengi wao hivi sasa hawapo duniani!,Aiseee nimekumbuka mbali sana!

Demu wangu enzi hizo alikuwa anakaa km 160 kutoka nilipo,hivyo nilikuwa naondoka na ma-bro tunaenda kwao nachukua mzigo then narudi nao maskani!,Ooooh God!,please take back the days!

Mwaka 2002 wakati kibao chake Nelly kiitwacho Dillema kinachiwa nilikuwa kwenye huba zito kiasi kwamba huu wimbo sitokaa niusahau hadi nafukiwa kwenye udongo!

Kwakuwa pia nilikuwa nampenda Mungu,nilikuwa shabiki wa kwanya ya Tumaini,iliyotoa albamu yao iliyoitwa Shangilieni,kwaya hii inapatikana pale Arusha!.,Aiseeee !

Mwaka 1998 to 2000 ,inapaswa kuwa miaka yenye kumbukumbu kwa wengi wetu!
Njaaa kali
 
Nilizamia computer lab kumbe Kuna pindi pale UDBS enzi hizo Fuculty of Business and Com.... pale UDSM wakati nadoea computer niwasikilize wasanii wa Marekani pia nimsalimie rafiki yangu mzungu akiwa Spokane Washington. Enzi hizo 2000 tunahesabika tunaojua kutumia computer na mambo ya emails. Nilikuwa raia wa kitaa mdogo tu.
 
Nakumbuka mwaka 2000 nilivyopiga pepa la lasaba halafu kila mtu akanikatia tamaa kasoro bimkubwa .Dakika za jiooooooni nikafaulu kwa second selection.Shule yenyewe ya serikali ilikuwa moja tu wilaya nzima.Ile furaha ya mama yangu mpaka sasa hivi kama naiona ilikuwa ni pureeee.
2004 nikapiga pepa la four .Nikaharisha kweli kweli mitihani yote saba F kasoro D ya Kiswahili.Ile hudhuni ya mama yangu kama naionaa mpaka alitoa vitone.Ikabidi niwekewe mipango kazi mezani.1 Kuanza kushona charahani.
2.Kujiunga na mafunzo ya ufundi pikipiki.
Hustler
 
Nakumbuka mwaka 2000 nikiwa na miaka mitatu mimi babu na bibi tulikua tunaish dodoma nyumba za serikali zilikua zina ukuta wa mabati kwa nje ila ndani ukuta ni singboard sijui zile za zamani so wafanyakazi weng walikua wanakaa pamoja unakuta nyumba moja ndefu kama darasa wanagawa kwa wafanya kazi watatu vyumba viwil na sebule kila mfanyakazi, kwa ufupi chumba nlichokua nalala kinafuatiwa na chumba cha mfanyakaz mwngne na mkewe,nkatoboa singboard kashmo kuangalizia yanayojiri kwa wakubwa dahhh wa zamani utoto raha sanaa
 
Back
Top Bottom