Nakumbuka enzi hizo daftari za mistari mikubwa na midogo kwa ajili ya kujifunza mwandiko kwa wanafunzi zilikuwa zinapatikana maduka ya Tanzania Elimu Supplies tu.
Nakumbuka pia tulikuwa tunapewa madaftari bure shuleni kila mwaka shule ikifunguliwa na likiisha unakwenda kumuonyesha mwalimu anakupa jingine jipya.
Nakumbuka enzi hizo kulikuwa na mashirika ya uchukuzi kila mkoa Mwanza ilikuwa KAUMA, Kagera ilikuwa KAGERA RETCO, Iringa ilikuwa IRINGA RETCO, Dodoma ilikuwa KAUDO, wadau mtaongezea.. Morogoro, Rukwa na kule kaskazini yalikuwa yanyanaitwaje.