Unakumbuka nini kuanzia Mwaka 1998 hadi 2000?

Unakumbuka nini kuanzia Mwaka 1998 hadi 2000?

Mwaka 1998
*World Cup ya France nikanunuliwa na bag ya dark blue iliyokuwa na ile nembo ya World Cup France
  • Bigi Jii za stika za Wachezaji wa mpira ukimpata Ronald Nazario De Lima wewe una bahati sana 😅😅🤣
  • Album ya Kofi Olomide Loi iliwika sana mwaka ule
*Mwaka 1999 ilikuwa saa 7 mchana narudi shule kikatangazwa kifo cha Nyerere, Marehemu John Komba alifyatua sana nyimbo za maombolezo
*Mwaka 2000 nilipata Kipaimara.
 
1. Elnino pale home maji yalijaa balaa.
2. Ugaidi ubalozi wa marekani yani yale mabomu tuliyasikia.
3. Kifo cha Nyerere.
4. Kufutwa kwa mtihani darasa la saba 1997 na kurudiwa 1998. Nilikua mdogo sana ila nakumbuka.
5. Kuanza kwa michango ya wazazi ili kujenga shule za sekondari, ilikua kila mwanafunzi buku 5 kama sijasahau. Michango hii ndio iliwezesha kupata shule kadhaa ambapo baadae nilisoma moja ya shule hizo.
6. World cup ufaransa 1998.
7. Yote ya yote kirusi cha Y2K kilivyotishia computer kuzima dunia nzima 1999 kwenda 2000.
8. Bwana Kibwetere kuwachoma watu kanisani Uganda.
9. Kutangazwa kwa mwisho wa dunia 2000.

N.k n.k
Shuleni kwetu tulikuwa na michango 3 maarufu,kama hujalipa hiyo husogei darasani!


1.UPE
2.ULINZI
3.UMITASHUMTA
 
Iko kama hiv

- 1998 nimempoteza mama angu mzazi nikiwa mtoto mdogo tu Darasa la pili. Hii ndio kumbukumbu yangu kubwa mpaka leo

- 1999 nakumbuka msiba wa mwalimu nyerere ndio kumbukumbu yangu kubwa maana ilikua inasemekana akifa Nyerere Tanzania kutatokea vita. Siku ile nikiwa shulen nakumbuka kuwaona walimu wakiwa na huzuni sana, nilikua darasa la 3

- 2000 nakumbuka ndio kwa mara ya kwanza kabisa nafanya mtihani unaoitwa wa Taifa wa Darasa la 4. Tulikua tunaambiwa huo mtihani hutakiwi kukatakata hovyo majibu 😂
Muhenga on flick!
 
year 1999, tumetoka fanya mazoezi ya graduation ya darasa la saba, mdogo mdogo tukapiga tz11 hadi home, umbali kama wa kilomita 4-5 toka shule hadi home, tunafika home saa 10 jioni, tunachungulia dirishani tunamuona mama na rafiki yake wanakodorea macho tv, huo haukuwahi kuwa muda wa mama kuangalia tv, kuingia ndani ndio tunagundua Nyerere hayupo tena.

Kesho yake Mwalimu Mkuu akatangaza hakutakuwa tena na graduation, shughuli ya primary ikaishia hapo, hata cheti cha leaving hatukupewa tena.
 
Kwa haraka haraka nakumbuka mwaka 1998 nilikua sebleni na baba tunaangalia tv tukasikia kishindo kikubwa nje....nikatoka kuangalia nguzo ya umeme tukijua ndio tatizo...baadae tunapata taarifa ni bomu limelipuka ubalozi wa Marekani pale opposite na ubalozi wa France...ilikua siku ya huzuni kwa taifa.
 
1998 natoka Lusaka naelekea Cape Town kitongoji kimoja kinaitwa Gugulethu NY 21 House number 77 nilipofika Cape Town niliuliza hiace zinazoenda Gugulethu na nauli yake nilipanda Hiace mpaka Gugs nikashushwa mtaa wa NY 21 nikaanza kutafuta namba ya nyumba mpaka nikafika ndugu yangu aliponiona hakuamini kabisa maana alinipa Address nikiwa home Tanzania baadae mawasiliano nilipoteza ila Address yake niliandika nyuma ya Passport ndugu yangu alifurahi sana na hakuamini...ndio mwanzo wa Mapambano ya SA huko Cape stad The City of good hope au wenyewe wanaiita Mothercity nikasota mwaka mmoja kwa kazi za magari mara supermarkets ila mwaka 2000 nilipata kazi ya ndoto yangu Debeers Marine kama saidia fundi Engine room baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu na kupelekwa vyuo nikawa Fundi kamili Engine room kweli maisha tumetoka mbali sana...
 
1. I need a girl ya diddy inanikumbusha mara yangu ya kwanza kuingia club pale PAN AFRICA HOTEL MOSHI 2. mwaka 1998 gavoo ilifuta paper ya 4m4 baada ya kuvuja nchi nzima
 
Back
Top Bottom