Unakumbuka nini kuanzia Mwaka 1998 hadi 2000?

Unakumbuka nini kuanzia Mwaka 1998 hadi 2000?

Mimi binafsi nimezaliwa mwaka 1988 wakati ambao Tanganyika & Zanzibar zilikuwa kwenye muungano uliozaa Tanzania.

Wiki ikiyopita niliamua kujipa likizo binafsi,kwakuwa ninafanya kazi nyingi kwa takribani mwaka mzima bila kupumzika,nikaona huu ni muda muafaka wa kuipumzisha akili!

Hivi sasa ninapoandika huu uzi nipo hapa hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) nikiwa nimetulia zangu nikipata mvinyo baridi kabisa kutoka pale Dodoma!.

Nikiwa huku,mara zote nimekuwa nikipenda kusikiliza ngoma za miaka ya nyuma kutoka mamtoni,ngoma ambazo kizazi cha sasa kinaona kama zimepitwa na wakati!

Ahahahahaaa!,Vijana wa kisasa wameyakosa mambo matamu mnooo ambayo enzi zetu sisi tuliya-enjoy!
Nimekumbukia sana miaka ya 1998 hadi 2000!.Mwaka 1998 mimi binafsi nilikuwa nina miaka 10,aiseee nimekumbuka mambo mengi sana yanayohusu burudani nikiwa na washikaji zangu ambao wengi wao kwasasa ni Marehemu. Kuanzia mwaka huo wa 1998 hadi mwaka 2001 wasanii wa marekani ndiyo waliongoza kwa kutoa Hitsongs ulimwenguni!

Nakumbukia sana wimbo wa I need a Girl wake P. Diddy feat Usher & Loon ambao ulitoka mwaka 2001,Huu wimbo umenikumbusha mbali sana kiasi kwamba hadi machozi yamenitoka kwasababu nawakumbikia washikaji zangu wengi ambao nilikuwa nazunguka nao kwenye Peugeot 306 ya home,wengi wao hivi sasa hawapo duniani!,Aiseee nimekumbuka mbali sana!

Demu wangu enzi hizo alikuwa anakaa km 160 kutoka nilipo,hivyo nilikuwa naondoka na ma-bro tunaenda kwao nachukua mzigo then narudi nao maskani!,Ooooh God!,please take back the days!

Mwaka 2002 wakati kibao chake Nelly kiitwacho Dillema kinachiwa nilikuwa kwenye huba zito kiasi kwamba huu wimbo sitokaa niusahau hadi nafukiwa kwenye udongo!

Kwakuwa pia nilikuwa nampenda Mungu,nilikuwa shabiki wa kwanya ya Tumaini,iliyotoa albamu yao iliyoitwa Shangilieni,kwaya hii inapatikana pale Arusha!.,Aiseeee !

Mwaka 1998 to 2000 ,inapaswa kuwa miaka yenye kumbukumbu kwa wengi wetu!
Kifo cha Mwalimu JK Nyerere mwaka 1999!
 
1999
Nakumbuka nipo primary tupo dinning room mida ya mchana TV inawashwa tunaona nyimbo za maombolezo baba wa taifa amefariki
Tunarudi class darasa zima ni kilio 😆 dah
 
1. Elnino pale home maji yalijaa balaa.
2. Ugaidi ubalozi wa marekani yani yale mabomu tuliyasikia.
3. Kifo cha Nyerere.
4. Kufutwa kwa mtihani darasa la saba 1997 na kurudiwa 1998. Nilikua mdogo sana ila nakumbuka.
5. Kuanza kwa michango ya wazazi ili kujenga shule za sekondari, ilikua kila mwanafunzi buku 5 kama sijasahau. Michango hii ndio iliwezesha kupata shule kadhaa ambapo baadae nilisoma moja ya shule hizo.
6. World cup ufaransa 1998.
7. Yote ya yote kirusi cha Y2K kilivyotishia computer kuzima dunia nzima 1999 kwenda 2000.
8. Bwana Kibwetere kuwachoma watu kanisani Uganda.
9. Kutangazwa kwa mwisho wa dunia 2000.

N.k n.k
 
Nakumbuka nikiwa mdogo na miaka kama 6 hivi, raisi wa marekani alikuja arusha, na kuna project alikua anaicheki jirani na kwetu (hospitali ya wilaya), sasa katika harakati na shamrashamra shule wanafunzi tukaruhusiwa mapema kwenda home...

Sasa yule baba(president) alivokua anapita kulikua na helkopta zinapita juu.

Ilikua ndio mara ya kwanza kuona hii kitu, nkaogopa nikakimbilia chini ya miti, bahatimbaya ule upepo wa helikopta ukikua mkali kiasi kwamba tawi la mti nililokuwa nimejificha likakwanyuka na kuniangukia

Niliisi nimekufa nikaogopa hata kujijeuza nlikaa pale bila kujigusa kama dakika 10, baadae ndio nikainuka uzuri sijaumia。。
Dah!....those were your days...
 
Nilizamia computer lab kumbe Kuna pindi pale UDBS enzi hizo Fuculty of Business and Com.... pale UDSM wakati nadoea computer niwasikilize wasanii wa Marekani pia nimsalimie rafiki yangu mzungu akiwa Spokane Washington. Enzi hizo 2000 tunahesabika tunaojua kutumia computer na mambo ya emails. Nilikuwa raia wa kitaa mdogo tu.
Ma Bro wengi walienda Marekani miaka hii kwasababu enzi hizo hakukuwa na akili ya kwenda nchi nyingine tofauti na Marekani
 
1. Elnino pale home maji yalijaa balaa.
2. Ugaidi ubalozi wa marekani yani yale mabomu tuliyasikia.
3. Kifo cha Nyerere.
4. Kufutwa kwa mtihani darasa la saba 1997 na kurudiwa 1998. Nilikua mdogo sana ila nakumbuka.
5. Kuanza kwa michango ya wazazi ili kujenga shule za sekondari, ilikua kila mwanafunzi buku 5 kama sijasahau. Michango hii ndio iliwezesha kupata shule kadhaa ambapo baadae nilisoma moja ya shule hizo.
6. World cup ufaransa 1998.
7. Yote ya yote kirusi cha Y2K kilivyotishia computer kuzima dunia nzima 1999 kwenda 2000.
8. Bwana Kibwetere kuwachoma watu kanisani Uganda.
9. Kutangazwa kwa mwisho wa dunia 2000.

N.k n.k
Shuleni kwetu tulikuwa na michango 3 maarufu,kama hujalipa hiyo husogei darasani!


1.UPE
2.ULINZI
3.UMITASHUMTA
 
Iko kama hiv

- 1998 nimempoteza mama angu mzazi nikiwa mtoto mdogo tu Darasa la pili. Hii ndio kumbukumbu yangu kubwa mpaka leo

- 1999 nakumbuka msiba wa mwalimu nyerere ndio kumbukumbu yangu kubwa maana ilikua inasemekana akifa Nyerere Tanzania kutatokea vita. Siku ile nikiwa shulen nakumbuka kuwaona walimu wakiwa na huzuni sana, nilikua darasa la 3

- 2000 nakumbuka ndio kwa mara ya kwanza kabisa nafanya mtihani unaoitwa wa Taifa wa Darasa la 4. Tulikua tunaambiwa huo mtihani hutakiwi kukatakata hovyo majibu 😂
 
Back
Top Bottom