Unakumbuka nini kuanzia Mwaka 1998 hadi 2000?

Mkuu umenifurahisha sana, kwa kurejea hii era ya muziki hususan hiyo ya mamtoni, hakuna wakati wowote dunia imeshuhudia mziki mtamu na vipaji vya kukata na shoka kama kama zama hizi za 90s to 2000...na haitakaa itokee mpaka dunia inafika mwisho, ni mziki uliokuwa na vibe la kufa mtu...nimetengeneza playlist yangu ambayo nitaisikiliza mpk nazeeka natembelea mkongojo! nakuombea mapunziko yako yakawe yenye amani tele...
 
Kwangu ni kipindi cha mwaka wa mwisho chuoni, kuisaka kazi, kumpoteza Bibi mzaa Mama n.k. Ilikuwa hali ya kutokuwa na uhakika wa maisha.
 
Mwaka 98 anahamishwa kikazi kutoka Dom mpaka Rukwa, Mwaka 99 kwa mara ya kwanza nasafiri na mama kutoka Dodoma kwenda Mbeya na basi linaitwa URAFIKI tukafikia kwa babu yangu alikua askari magereza mstaafu alikua na tv inaonyesha rangi mbili tu hapo ndio msiba wa Nyerere unaonyeshwa ITV.

Mzee wangu alihamishwa kikazi Namanyere wilaya ya Nkasi, maisha tuliona ni magumu sana kwa sababu tulikua tunaishi Dodoma kuna umeme masaa 24 tunafika sehemu hakuna umeme wanatumia generator napo linawaka jioni ya saa 1 mpaka 3-4. Nyimbo zilizokua zinatawala ni lile kundi la Makoma. Daah nimekumbuka mengi sana
 
Nakumbuka enzi hizo kulikuwa na mashirika ya uchukuzi kila mkoa Mwanza ilikuwa KAUMA, Kagera ilikuwa KAGERA RETCO, Iringa ilikuwa IRINGA RETCO, Dodoma ilikuwa KAUDO, wadau mtaongezea.. Morogoro, Rukwa na kule kaskazini yalikuwa yanaitwaje..

1998 haya mashirika yalikuwa yashajifia zamani
 
umenikumbusha mbali kijana. huo mwaka uliozaliwa raisi mwinyi rip alikuja mkoani kwetu kufungua msikiti mkuu wa hapo mkoani kwetu
pia mwaka huohuo timu moja ya mkoani km sikosei kosto hiihii ya tanga ya akina mgunda huyu wa simba waliduwaza nchi kwa kutwaa kombe ligi kuu. miaka hiyo hizi simba na yanga wakikutana na reli ya morogoro kosto, pamba ya mwanza lolote linaweza kutokea.
 
una bahati mkuu ulienda nchi tayari ina president mweusi ubaguzi wa mtu mweupe unaishiaishia maana vinginevo ungeziona rangi zote.
 
Dah!Nimekumbuka zanani kweli mwaka 2003nikiwa na miaka minne.Nilanza chekechea.Nilipokuwa napelekwa nilikuwa nachekacheka.Ila,mama aliponiacha na wenzangu nililia sana.Halafu,sasa nakumbuka mwaka 2014 nikaanza kuuza mayai yaliyochemshwa na karanga za kukaanga.Nikachangisha hela hadi nikanunue simatifoni.Mbona walinikoma.Sisi watu wa zamani hatupendi kujionesha tu.Nina stori nyingi sana za kusisimua.Nagonga miaka 24 kwa sasa,yaani kwa kukaribishia ni robo karne.
 
Umenikumbusha kulikuwa na kipindi nadhani Chanel 10 kikiitwa Muziki na Buzz,Alikuwa akiendesha Frenk Mtao na Salma Msangi.Yaani nilikuwa natuma sana Salamu kwa Email kwenye Internet cafe...
 
Umenikumbusha kulikuwa na kipindi nadhani Chanel 10 kikiitwa Muziki na Buzz,Alikuwa akiendesha Frenk Mtao na Salma Msangi.Yaani nilikuwa natuma sana Salamu kwa Email kwenye Internet cafe...
Yeah, nilikuwa naenda internet cafe pale Ubungo RUBADA kwenye hostel za watu wa Masters unawekewa timer ukilipia nusu saa muda ukiisha ngoma inakata unachukia. Ilikuwa expensive Sana.
Sehemu nyingine UCC pale UDSM kulikuwa na internet cafe. Wateja wengi wazungu tu. Kama una confidence unapata mbebe wa kizungu...😃😃

Mimi nikiona mfuko hauko sawa nazamia Comp Lab ya Department of Math, au ya Faculty of Science pale AVU, au Department of Geology, au UDBS.
Nilipata marafiki wengi sana shuleni nikiwa advance sababu ya kujua comp na internet. Enzi za Netscape Navigator browser, Hotmail, AOL (American Online) email service.

Note:
Sikuwa mwanafunzi wa chuo, nikifungua madude wanafunzi wanashangaa wanakuja niwafundishe. My two brothers walikuwa viongozi wa Faculty of Science ndiyo walinipa ujasiri wa kuingia popote.
 
Hongera mkuu towa maconnection
 
"Mimi binafsi nimezaliwa mwaka 1988 wakati ambao Tanganyika & Zanzibar zilikuwa kwenye muungano uliozaa Tanzania", hii Tanganyika na Zanzibar yako ni tofauti na tunayoishi sisi! Muungano wa mwaka 1964 wewe unauona mwaka 1988!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…