Unakumbuka nini kuanzia Mwaka 1998 hadi 2000?

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
2,345
Reaction score
6,970
Mimi binafsi nimezaliwa mwaka 1988 wakati ambao Tanganyika & Zanzibar zilikuwa kwenye muungano uliozaa Tanzania.

Wiki ikiyopita niliamua kujipa likizo binafsi,kwakuwa ninafanya kazi nyingi kwa takribani mwaka mzima bila kupumzika,nikaona huu ni muda muafaka wa kuipumzisha akili!

Hivi sasa ninapoandika huu uzi nipo hapa hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) nikiwa nimetulia zangu nikipata mvinyo baridi kabisa kutoka pale Dodoma!.

Nikiwa huku,mara zote nimekuwa nikipenda kusikiliza ngoma za miaka ya nyuma kutoka mamtoni,ngoma ambazo kizazi cha sasa kinaona kama zimepitwa na wakati!

Ahahahahaaa!,Vijana wa kisasa wameyakosa mambo matamu mnooo ambayo enzi zetu sisi tuliya-enjoy!
Nimekumbukia sana miaka ya 1998 hadi 2000!.Mwaka 1998 mimi binafsi nilikuwa nina miaka 10,aiseee nimekumbuka mambo mengi sana yanayohusu burudani nikiwa na washikaji zangu ambao wengi wao kwasasa ni Marehemu. Kuanzia mwaka huo wa 1998 hadi mwaka 2001 wasanii wa marekani ndiyo waliongoza kwa kutoa Hitsongs ulimwenguni!

Nakumbukia sana wimbo wa I need a Girl wake P. Diddy feat Usher & Loon ambao ulitoka mwaka 2001,Huu wimbo umenikumbusha mbali sana kiasi kwamba hadi machozi yamenitoka kwasababu nawakumbikia washikaji zangu wengi ambao nilikuwa nazunguka nao kwenye Peugeot 306 ya home,wengi wao hivi sasa hawapo duniani!,Aiseee nimekumbuka mbali sana!

Demu wangu enzi hizo alikuwa anakaa km 160 kutoka nilipo,hivyo nilikuwa naondoka na ma-bro tunaenda kwao nachukua mzigo then narudi nao maskani!,Ooooh God!,please take back the days!

Mwaka 2002 wakati kibao chake Nelly kiitwacho Dillema kinachiwa nilikuwa kwenye huba zito kiasi kwamba huu wimbo sitokaa niusahau hadi nafukiwa kwenye udongo!

Kwakuwa pia nilikuwa nampenda Mungu,nilikuwa shabiki wa kwanya ya Tumaini,iliyotoa albamu yao iliyoitwa Shangilieni,kwaya hii inapatikana pale Arusha!.,Aiseeee !

Mwaka 1998 to 2000 ,inapaswa kuwa miaka yenye kumbukumbu kwa wengi wetu!
 
Nelly mwenyewe anasema miaka hiyo kwake ilikuwa migumu kimziki , kwani kila msaniii alikua anatoa ngoma kali. Cha ajabu kila msaniii alikuwa anasikilizwa. Kuanzia akina ,P. Diddy, Jay Z, DMX, etc.
 
Nimekumbuka ajali ya MV Bukoba,

Uchaguzi wa 1995 Mrema akiwa NCCR Mageuzi aliwika sana.

Ninakumbuka miaka ya 90 kwetu Moshi wanachama wa NCCR walikuwa wanafanya vikao vya ndani na slogan yao NCCR......Mageuzi....!!!

Mwaka 1991 babu yangu alinichapa sana baada ya kuchezea mlango.

Mwaka 1998 niliangua machenza nikapewa shilingi 100/= ya noti nikaenda kununua soda ya koka.
 
Nakumbuka mwaka 2000 nilivyopiga pepa la lasaba halafu kila mtu akanikatia tamaa kasoro bimkubwa .Dakika za jiooooooni nikafaulu kwa second selection.Shule yenyewe ya serikali ilikuwa moja tu wilaya nzima.Ile furaha ya mama yangu mpaka sasa hivi kama naiona ilikuwa ni pureeee.
2004 nikapiga pepa la four .Nikaharisha kweli kweli mitihani yote saba F kasoro D ya Kiswahili.Ile hudhuni ya mama yangu kama naionaa mpaka alitoa vitone.Ikabidi niwekewe mipango kazi mezani.1 Kuanza kushona charahani.
2.Kujiunga na mafunzo ya ufundi pikipiki.
 
Mimi binafsi nimezaliwa mwaka 1988 wakati ambao Tanganyika & Zanzibar zilikuwa kwenye muungano uliozaa Tanzania.

Wiki ikiyopita niliamua kujipa likizo binafsi,kwakuwa ninafanya kazi nyingi kwa takribani mwaka mzima bila kupumzika,nikaona huu ni muda muafaka wa kuipumzisha akili!

Hivi sasa ninapoandika huu uzi nipo hapa hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) nikiwa nimetulia zangu nikipata mvinyo baridi kabisa kutoka pale Dodoma!.

Nikiwa huku,mara zote nimekuwa nikipenda kusikiliza ngoma za miaka ya nyuma kutoka mamtoni,ngoma ambazo kizazi cha sasa kinaona kama zimepitwa na wakati!

Ahahahahaaa!,Vijana wa kisasa wameyakosa mambo matamu mnooo ambayo enzi zetu sisi tuliya-enjoy!
Nimekumbukia sana miaka ya 1998 hadi 2000!.Mwaka 1998 mimi binafsi nilikuwa nina miaka 10,aiseee nimekumbuka mambo mengi sana yanayohusu burudani nikiwa na washikaji zangu ambao wengi wao kwasasa ni Marehemu!.Kuanzia mwaka huo wa 1998 hadi mwaka 2001 wasanii wa marekani ndiyo waliongoza kwa kutoa Hitsongs ulimwenguni!

Nakumbukia sana wimbo wa I need a Girl wake P. Diddy feat Usher & Loon ambao ulitoka mwaka 2001,Huu wimbo umenikumbusha mbali sana kiasi kwamba hadi machozi yamenitoka kwasababu nawakumbikia washikaji zangu wengi ambao nilikuwa nazunguka nao kwenye Peugeot 306 ya home,wengi wao hivi sasa hawapo duniani!,Aiseee nimekumbuka mbali sana!

Demu wangu enzi hizo alikuwa anakaa km 160 kutoka nilipo,hivyo nilikuwa naondoka na ma-bro tunaenda kwao nachukua mzigo then narudi nap maskani!,Ooooh God!,please take back the days!

Mwaka 2002 wakati kibao chake Nelly kiitwacho Dillema kinachiwa nilikuwa kwenye huba zito kiasi kwamba huu wimbo sitokaa niusahau hadi nafukiwa kwenye udongo!

Kwakuwa pia nilikuwa nampenda Mungu,nilikuwa shabiki wa kwanya ya Tumaini,iliyotoa albamu yao iliyoitwa Shangilieni,kwaya hii inapatikana pale Arusha!.,Aiseeee !

Mwaka 1998 to 2000 ,inapaswa kuwa miaka yenye kumbukumbu kwa wengi wetu!

kibwetere

welcome Y2K vifaa kushindwa kutambua mwaka 2000
 
Nimezingatia neno
Nakumbuka mwaka 2000 nilivyopiga pepa la lasaba halafu kila mtu akanikatia tamaa kasoro bimkubwa .Dakika za jiooooooni nikafaulu kwa second selection.Shule yenyewe ya serikali ilikuwa moja tu wilaya nzima.Ile furaha ya mama yangu mpaka sasa hivi kama naiona ilikuwa ni pureeee.
2004 nikapiga pepa la four .Nikaharisha kweli kweli mitihani yote saba F kasoro D ya Kiswahili.Ile hudhuni ya mama yangu kama naionaa mpaka alitoa vitone.Ikabidi niwekewe mipango kazi mezani.1 Kuanza kushona charahani.
2.Kujiunga na mafunzo ya ufundi pikipiki.
“kuharisha”
 
Nakumbuka nikiwa mdogo na miaka kama 6 hivi, raisi wa marekani alikuja arusha, na kuna project alikua anaicheki jirani na kwetu (hospitali ya wilaya), sasa katika harakati na shamrashamra shule wanafunzi tukaruhusiwa mapema kwenda home...

Sasa yule baba(president) alivokua anapita kulikua na helkopta zinapita juu.

Ilikua ndio mara ya kwanza kuona hii kitu, nkaogopa nikakimbilia chini ya miti, bahatimbaya ule upepo wa helikopta ukikua mkali kiasi kwamba tawi la mti nililokuwa nimejificha likakwanyuka na kuniangukia

Niliisi nimekufa nikaogopa hata kujijeuza nlikaa pale bila kujigusa kama dakika 10, baadae ndio nikainuka uzuri sijaumia。。
 
Bill Clinton huyo mkuu,huyu Rais ndiye aliyeipa jina Arusha la GENEVA OF AFRICA
 
Ndo nilikua nmejua kusoma na kuandika hyo 98.
Micharazo yangu ilikua kwenye kuta za nyumba za watu.
Kistaarabu siwezi kuandika maneno ambayo nilikua nikiyachora kwenye kuta hizo lakn im sure wengi wanajua ni maneno gani.
 
Ulitisha sana mkuu!
 
Nelly mwenyewe anasema miaka hiyo kwake ilikuwa migumu kimziki , kwani kila msaniii alikua anatoa ngoma kali. Cha ajabu kila msaniii alikuwa anasikilizwa. Kuanzia akina ,P. Diddy, Jay Z, DMX, etc.
Mkuu Nelly anaongea as an artist,but ukweli ni kwamba,Nelly ndiye kiumbe alikuwa na Dunia ya peke yake kwenye suala la Uandishi,Mavazi na Mikato!

Hakuna wimbo uli-Hit duniani mwaka 2002 kama Dillema wa Nelly!,Hakuna na haitatokea tena!
 
Back
Top Bottom