marco polo jr
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 362
- 1,771
Katika maisha shule kunakuwa kuwa na changamoto mbalimbali hasa tuliosoma shule za St kayumba mm nakumbuka baada ya kumaliza shule ya sekondari .Nilibahatika kufaulu na kupangiwa kuendelea na masomo shule moja ya boys huko mikoa ya nyanda za juu kusini.Muda ulipowadia kufunguliwa shule kijana nilijiandaa kwa ajili ya kuripoti nakumbuka tulitumiwa form za maandalizi nikanunua vitu vyote pamoja na sare .Siku ya kufunguliwa ikawadia nikabeba tranka langu na vifaa vingine mzee tulienda wote wahuni wakanipokea vifaa vyangu na kuvipeleka bwenini mm nikabakia na mzee kwa ajili ya kukamilisha Mambo Fulani .Baada ya muda kwenda nikaenda bwenini kucheki vifaa vyote hakuna kumbe wahuni walionipokea walikwenda kuviuza mtaani mm sura sikuwashika godoro ,tranka na ndoo nikawa nimepoteza dah! Sio mm peke yangu niliyeibiwa wengi tuu wanaoripoti walikuwa wakiibiwa na wababe wa pale shule form five tulikuwa tukiitwa form one wa kiangazi .nikabaki nikilia tuu mzee akaninulia vitu vingine akaniambia uwe makini ukiibiwa Tena sitokunulia toka siku iyo nikawa mbabe Sana nikaacha unyonge .ebu na ww unakumbuka ubabe gani uliokutana nao shuleni hasa za bweni.