Nilitoka shule ya kata (Kikwete kwa hili nitamtetea mpaka unipige ngumi) nikaenda shule flani kule Kilimanjaro. Kwanza nilichagua shule mwenyewe, nilichagua kwa kuzingatia shule iko jamii gani maana mimi kuna vitu siwezi vumilia na najua viko mazingira kadhaa hapa nchini.
Sijawahi faya maamuzi niiyofurahia kama hili jambo. Shule nilipokelewa na dogo mmoja alikuwa form III akanisubiri nitoke mapokezi akabeba mizigo yangu na kunipeleka dorm moja the zuri kwa kila kitu pale shule. Maisha ya kistaarabu kwa wanafunzi na wengi wa walimu, wakorofi hawakosi. Mkuu wa shule ni the best sijawahi ona: msikivu, ana msimamo, sio mbabe wala maamuzi ya kijinga. Tulimpenda wote hata wakorofi.
Nimetoka na marafiki kibao na still madogo kibao wananitafuta hadi sasa. Huwa nakariri sana watu na sibagui eti form six asiongee na form one, hiyo sina. Nilikuwa namiliki simu kiubishi na nilifanya sana transaction za madogo hasa nauli za likizoni. Nilikuwa kiongozi wa dini. Sijawahi jutia na huwa napamiss sana pale. Nitakuwa naenda sana na isitoshe K'njaro napakubali mno.
Nilikuwa natoka sana nje ya shule. Mitaa mingi nimeenda, sikuwa mhuni hata. Sikuwa maskini hata kidogo.