Unakumbuka Nini kuhusu maisha shule za bweni A level share kisa chako.

Kuogeshwa kwenye mto usiku.

Hiyo ilikuwa form 5. Nimetoka kusoma day O level, sijawahi experience life la boarding. Niliona shule chungu mnoo.

Shuleni pale palikuwa na mto usiokauka maji mwaka mzima. Wakulungwa/wajuba walikuwa wanakuja usiku wa manane ukiwa umelala, wanakubeba ivoivo ulivyolala, kama ulikuwa umelala uchi unaenda ivoivo. Wanakupeleka mtoni, wanakulazimisha uzame mzima mzima. Kisha wanakurudisha bwenini na kukuamrisha upande kitandani ivoivo.

Baada ya muda likatokea bonge moja la timbwili. Form 6 & Form 4 VS Form 5 & Form 3. Ilipigwa mechi kali mpaka FFU wakaja kutuliza ghasia.

Mwisho wa siku kuna wajuba walipeperushwa na shule hawakuimaliza. Hiyo ilikuwa kama laana maana mwaka mmoja nyuma kuna mwanafunzi mmoja wa shule jirani aliuawa shuleni hapo (Lyamungo vs Umbwe).
Unforgetable
 
Tulikuwa tunaita ambuuuush ticha akija usiku. Ukisikia hivyo ukiwa dorm unakimbia. Wanafunzi pamoja na utani, kwenye hili swala hatukuwa tunataniana.
[emoji851][emoji851][emoji851][emoji851][emoji851][emoji851]

Nimecheka kishenzi, kwamba mtataniana vyooote ila kwenye Ambush lazima heshima iwepo.
Unforgetable
 
Wavulana F6 2018 ifunda tech nadhani mnakumbuka vizuri kilicho tupata.

Our motto SKILLS AND EFFICIENCY
 
Hawa mafala wa ainahyo walinitesa Sana
Yani Cku ya kwanza kwenda class nakuta jamaa wanasolve trig Mara differentiation Mara integration aseeh jamaa wanabishana kinoma.. Nilijiona mjinga na nishafeli.. Niiwakariri wale jamaa na finally necta niliwaacha mbali Sana

Nakumbuka kuna siku nilikaa bwenini nikalia Sana.. Nikamkumbuka mama alivoniambiaga kuwa kuna Maisha magum duniani.. Ckuwahi kula marage ya wadudu.. Ugali mgumu wa Dona na kande la wadudu.. Mwanzoni nilikonda Sana.. Nilikuja nikazoea na nikatusua vizuri Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni ifundaaaa
 
Boarding bana dah ....
maisha ya kula kwa table dah, nikapangwa na wahuni full ubabe muda wa msosiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
kumiliki illegal material....
Naingia prepo saa mbili nipe nusu saa ni sha horizontal πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kuiba mahindi ya walimu usiku na kuchemsha juu ya dari, mchana kugoma kula sababu ya chakula kibaya.
Tukarudishwa nyumbani shule nzima, tukakaa home mpaka tukajisahau kama sisi ni wanafunzi. Wakati tunarudi shule tunakutana na mock ya mkoa wale wasongo wamepiga mapindi wakapasua sisi wengi tuliojua tulikua likizo tukapata marks zinazokaribia umri wetu. Ila ilipofika necta mkeka ulipinduka hatari.
Msuli wa zima moto ulikua mtamu sana.
Mwaka uliofuatia madogo wakaendeleza mtindo wetu wa mahindi, wakachoma bweni.
 
Advanced level student unaibiwa kiboya hivyo, wakati uko Olevel hukuwahi kusikia stori za shule za bweni? Ninesoma bweni Shule za Serikali miaka 6 sikuwahi kuibiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…