Unakumbuka tukio gani ulilonusurika na ukaamini ni mkono wa Mungu umekunusuru?

Asante kwa kunichekesha leo [emoji3][emoji3][emoji3], nilikuwa nimenuna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwaje ukawa katika hali hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwa na miaka 8 au 9...nilimkwepa mshua nkazuga naenda kuteka maji na sufuria...ilibidi niende kweli,kufika pale nilimkuta Dada anafua pembeni ya kisima...nikamsalimia nkaingia na sufuria yangu pembeni ya kisima...sijui mawazo au Nini,loh sufuria ikaponyoka ...katika kupambana isizizame,nkatelezea na Mimi ...nshaanza kunywa vikombe kadhaa...bahati yule Dada anafua alikua amemaliza maji anakuja kuteka mengine...loh ndo kaniokoa



1 Form 3 I think...nilikua napenda Sana michezo zaidi basketball,Kuna siku tulitoka kwenye mazoezi ya viungo magumu kidogo


Sasa shule yetu mipira ilikua imeharibika na tulikaa bila mipira kwa siku nyingi....kwahiyo kipindi Cha michezo muda mwingi tuliutumia kwa mazoezi ya viungo na riadha


Siku tunatoka mazoezi Mara tukapewa mipira mipya na mkuu wa shule,kwa ajili ya munkari siku niliopt kucheza football


Rafiki angu Ray alishauri nisicheze kwa sababu tulikua tumefanya zoezi Kali kidogo

Nilipangwa no Saba pembeni


Nakumbuka ilipigwa pasi ndefu Sana kwangu,nkawa naiwahi isitoke nje kwa Kasi,nikataka kuutudisha ndani mpira kwa kisigino


Lahaula[emoji21][emoji21][emoji21]kwa spidi yangu na mpira,nilijikuta nimeupanda ule mpira kwa juu nikasafiri nao mita kadhaa,kabla ya kurushwa juu na kuangukia kichwa kwa kisogo


Nakumbuka niliinuka,lakini ghafla nkaona narudi chini,na kuhisi nagandamizwa na uzito mkubwa kutosimama Tena,niliona naanza kupata taabu kupumua...nkasikia kwa mbali watu wanapiga mayowe anakufaa


Kilichoendelea siku jua,nilishtuka nesi ananichoma sindano....nkamuuliza kwani vipi,mbona unanichoma...kumbe nilivyoanguka,nikianza kutoa povu na damu,na wengi walikimbia...wachache jasiri walikuja kunipepea mpaka nkawa kwenye Hali ya kawaida kiasi


Naambiwa nilikua naongea Mambo yasioeleweka,mpaka leo tukio hili nahisi limeniathiri kiasi....Nina tatizo kubwa la kusahau


Mwaka huu chimbo Fulani,niliumwa tumbo na mgongo kwa nusu saa,kiasi nikianza kusufforcate kupumua,nkajua navuta,nililia Kama mtoto huku nasali,mbaya ilikua mbali na hospital... ntashukuru nilitoka mzima


Ya wanaosema kufanyiwa ushirikina Ni mengi,ila Sasa sina uhakika,Kama kweli au lah


Hizo Ni hatari nilizoziona,lakini naamini ziko nyingi Mungu kanikinga na anaendelea kunikinga ambazo sizifahamu pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
lee van cliff, Ndio maana silale bila net hata Kama hakuna mbu...

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni keeling neti inasaidia kuzuia wadudu wengi wasiingie kitandani,lakini amini nakuambia nyoka akiwa ndani anaweza kukuuma hata Kama umeshusha neti,ni angonga tu Kama umeweka mkono au mguu kugusa neti usingizini na Kama unakoroma ndo anachukia zaidi.
 
Dah mungu yupo man
Siku moja tulikua site
Tunafanya maintenance kubadiri nguzo ya HT...kuangalia belt(kwa wasioijua Ni ule mkanda wakujifunga kiunoni unakushikiza na nguzo unavyokua juu) kuchek belt yangu imefunguka Ile lock yake
Dah afu nipo kama meter 12 juu

kelphin kepph
 
Hiki ni kichaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Dah mpaka mwili umesisimka


Sent using Jamii Forums mobile app
 

mmmh mkuu nimejikuta nasisimka, it impressed me and touched
 
Matukio yayanafanana,nakumbuka nikiwa miaka fulani hivi kwenye nyumba ya Asili nimelala kifua wazi Nyoka akaniangukia kifuani nikamrusha na mkono "automatically " jasho lilinitoka nakahisi kufa nyoka akashika njia yake nami nikakimbia nje nahema natazama kama kaningata kifuani. Hakika Mungu anasaidia!
 
Umetumwa sio?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama uko na tatizo la kusahau..!mbona hizi habari ujazisahau?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…