Unalalaje lodge ya 80,000 na bado hujajipata

Unalalaje lodge ya 80,000 na bado hujajipata

Kitambo kidogo tulipelekwa training DAR, ofisi wakatufanyia booking Sleep Inn hotel iko mitaa ya Kariakoo (Swahii/Mahiwa) kama sijasahau. Kuna binti tulikuwa naye yeye akafikia White Sand hotel, yaani akaacha booking ya bure, sponsor kamlipia huko. Asubuhi tunakutania mitaa ya posta, yeye analetwa na gari nene kwelikweli, sema demu mwenyewe alikuwa simple sana hana makeke kabisa. Siku ya mwisho anatutoa wote out kula kunywa juu yake.
Hahaha.........hao sio wenzetu ujue 🤗
 
Braza inaonekana ulienda safari na pisi, mara unaona imeenda lodge ya 80,000 na wewe uwezo wako ni 40,000 🤣🤣🤣🤣
 
Hapana, mimi nipo kati ya hao 8😊
Apostle Kuna muujiza huku 😜

Kuhusu wewe nimekataa ndugu mjumbe, nakumbuka kwenye ile seminar ya mwisho ulijilipia pale Morena hotel tena room ya 120k 🤗
 
Tuliwahi kusafiri kikazi mkoa fulani tukapewa per Diem 230,000/= kwa wiki mbili......nikaenda kulala guest ya 10,000/= mpaka namaliza mambo yangu.......umbali wa eneo la kazi na hiyo guest gharama yake ni 3,000/= kwenda na kurudi......

Mama ntilie wapo kama hatua ishirini kutoka hapo na sahani ya wali inaanzia 1,500/= mpaka 3,000/= kwa VIP........

Kwa siku nilikuwa natumia 20,000/= Tu.........

Waliofikia hotelini project ilivyoisha walikuja kuniazima nauri za kurudia.......

MAISHA HAYA.....NI SAFARI NDEFU SANA
 
Wanawake wana matumizi makubwa ya pesa kila sehemu wala sio jambo la kushangaa hilo.
Hata bando we unaweza kutumia la buku tatu na unafanya kazi, yeye akatumia zaidi ya buku tano kwa siku na hana kazi inayomuweka mtandaoni.
 
Ndio maana unalipwa perdiem kwa ajili ya kula na kulala si kwa matumizi mengine. Siwezi lala lodge uchwara eti ni save hela. Maisha na hayahaya, enjoy while you can.

Mwajiri wetu alijua tabia za wafanyakazi kutaka kusave bila kujali usalama na afya zao wakiwa kazini. Hotel unalipiwa five star na daily allowance unapewa. Tena hotel unalipia kwa Mastercard ya ofisi.
Kampuni zozote za maana wanakuambia utafikia hotel flan. Brand kwao ni muhimu.
 
Tuliwahi kusafiri kikazi mkoa fulani tukapewa per Diem 230,000/= kwa wiki mbili......nikaenda kulala guest ya 10,000/= mpaka namaliza mambo yangu.......umbali wa eneo la kazi na hiyo guest gharama yake ni 3,000/= kwenda na kurudi......

Mama ntilie wapo kama hatua ishirini kutoka hapo na sahani ya wali inaanzia 1,500/= mpaka 3,000/= kwa VIP........

Kwa siku nilikuwa natumia 20,000/= Tu.........

Waliofikia hotelini project ilivyoisha walikuja kuniazima nauri za kurudia.......

MAISHA HAYA.....NI SAFARI NDEFU SANA
Nimejifunza kitu..Nikitumia pesa vibaya kuna mmoja kati yetu ntakopa kwake.😂
 
Mtu ni mfanyakazi kama wewe hasa wadada mmepewa per diem za kawaida kabisa rate hizi hizi za night za 130,000 cha ajabu mnafika mkoa unashangaa mdada anaenda kulala lodge ya 80,000.

Aisee hatupangiani maisha lakini je Kwa maisha gani hayo unakuta nyumbani kaacha hela ndogo tu lazima uangalie na ulipotoka.. angalau ingekuwa umepata hela kubwa za miradi ila sio allowance za hizi activities za kila siku..

At least kidogo ukilala ya 40000 me sitashangaa.. Ila nacho fikiria hawa wadada wanakuwa na mitego yao mingine kunasa ma sponsor sio bure..
Punguza hasira mkuu, kama ulifukuzia mdada ukakuta anapolala ni ghali kuliko unavyoweza we kuwa mpole.

hotel ya hiyo bei lazima ukute rumu imetulia, hata ukilala na manzi nguvu za kiume zinarudi 😂🤣,

Asubuhi breakfast kali sio mkate na chai 😂.

Acha ubahili mkuu, hulali mwaka mzima hapi, mpe mtoto maisha upate utamu wote 😂😂😅🥸🥸
 
Marehemu babu yangu aliwahi kuniambia "mjukuu wangu KAMWE usishindane na mwanamke", nilimuuliza alimaanisha nini, akanijibu......mwanamke anaweza kuwa hana hata mia sasa hivi lakini baada ya masaa kadhaa akamilikishwa mali chungu nzima kwakuwa anacho kiwezeshi.
Ukweli mtupu....mbususu ni mtaji mmoja mzuri sana kwa wadada tena ongeza na tako ndio kabisaaa
 
Mtu ni mfanyakazi kama wewe hasa wadada mmepewa per diem za kawaida kabisa rate hizi hizi za night za 130,000 cha ajabu mnafika mkoa unashangaa mdada anaenda kulala lodge ya 80,000.

Aisee hatupangiani maisha lakini je Kwa maisha gani hayo unakuta nyumbani kaacha hela ndogo tu lazima uangalie na ulipotoka.. angalau ingekuwa umepata hela kubwa za miradi ila sio allowance za hizi activities za kila siku..

At least kidogo ukilala ya 40000 me sitashangaa.. Ila nacho fikiria hawa wadada wanakuwa na mitego yao mingine kunasa ma sponsor sio bure..
wanaume tunakwisha
 
Mleta mada ana hoja ila wadau wanamshambulia tu.

Ni sahihi kusema kwamba kwa perdiem ya 130,000 kutumia 80,000 kwa Lodge sio matumizi mazuri ya pesa.

Mpaka ulipwe 130,000 ina maana viwango vyako ni vya chini na unapaswa kubudget pesa kulingana na viwango vyako.

Mimi nakumbuka kuna mshkaji alijenga nyumba kwa pesa hizi hizi za safari, ndio alinipokea kazini.

Tukiwa safari ananielekeza namna ya kuishi mtu unaweza dharau hii hoja ila ina maana kubwa sana.
 
Back
Top Bottom