Unalipwa 500,000 TZS? Jaribu kuishi hivi!

Watu kama nyie siwapendi sana.. Mnaojifanya mnajua saana maisha. Buku tano kwa siku unakula na kunywa inatoshaje?? maji kwa siku unakunywa robo lita? au unashindia kandolo?? toka hapa
Elfu tano kwa siku unakula na kushiba vizuri mfano kwa mtu wa Dar na bdo ulo peke ako unaacha buku ya maji hpo ni lita 2 mchana unakula buku 2 na usku buku 2 asubuhi unaacha hkun umuhimu huo
 
Kwanza nani analipwa hizo laki 5 mkuu? Watumishi wengi wakishakatwa mikopo wanabaki na around 200k. Hii ndio ulipaswa ufanyie hesabu mkuu. Acha kufake life.
 
Elfu tano kwa siku unakula na kushiba vizuri mfano kwa mtu wa Dar na bdo ulo peke ako unaacha buku ya maji hpo ni lita 2 mchana unakula buku 2 na usku buku 2 asubuhi unaacha hkun umuhimu huo
Maisha ya daslam kumbe ni mepesi hivo. me sikujua
 
ahaaaa, kumbe ndo ww wa hapa ofisini.. Sasa mbona unakuja kunisemea huku lakini? 😎
 
uzuri wa raia wa JF hapa, wote humu tupo na income za Tsh. > 4M kwa mwezi.

My point is, ukitaka ujue nguvu ya 500k kwa mwezi, fanya hiviiii tangaza Tangazo la ajira na uweke posho iwe ni 500k kwa mwezi, kisha vigezo kiwe mwombaji awe na elimu ya diploma au zaidi. Weka namba yako ya simu.

Kisha uje ulete mrejesho ni watu wangapi watakufuta kuomba hiyo kazi.

Financially speaking, kwa nchi ya chini kiuchumi kama TZ, hiyo 500k/month sio mbaya kwa kujitafuta kwanza then utajiongeza baadae. Wengi mno wangetamani hata kuipata tu hiyo kila mwezi.

Fanya tu hiyo research, kisha uje utupe mrejesho.



NB: tukumbuke it's 2026, na kima cha chini cha mshahara serikalini ni 500k kwa mwezi.

Na wafanyakazi wote za govt kwa sasa sidhani kama kwa idadi wanafika 1.3m kwa ujumla wao (walimu, afya, majeshi, utawala, n.k)

Nchi yetu zaidi ya 70% ya watu wamejiajiri katika sekta zisizo rasmi (small scale agriculture, vibarua, ujasiriamali, ajira zisizo rasmi, n.k.)..... hii kwa mujib wa takwimu za NBS (national bureau of statistics) za miaka mitatu iliyopita.

Na kipato cha sekta isiyo rasmi sote tunajua jinsi kilivyo hakieleweki, so mtu wa sekta hii ukimhakikishia net 500k kila mwezi, obviously atafuruhi.
 
Logic yangu bado haujaielewa ,nimesema kwa life la kikawaida Kilo 5 per month haitoshi labda uwe bachela ambaye hana majukumu yeyote.

Kuna kampuni za ulinzi zipo zinalipa laki na 20 kwa mwezi sasa mtu unakuwa unajiuliza hivi mwajiri anawaza nini kumpa mtu laki na 20 kwa mwezi?

Ningekuwa na mamlaka minimum salary kwa non pro ingekuwa 1m-1.5m na Pro not less than 3m.

Wenye makampuni wanabana mishahara kwa kuwalipa staffs halafu fedha nyingi inabaki kwao na ndiyo maana utaona watoto wa bakhresa au GSM wanatembelea magari ya mabilioni ,utasikia mabank yamepata faidi ya Trilioni kwa mwaka ,wafanyakazi wanapunjwa mishahara......Haypo mabilioni wanayoteketeza kwenye magari wangekuwa na uwezo wa kuwalipa staffs wao mishahara ya 1m hadi 1.5m kwa mwezi.

Sasa unampa mtu elfu 8 kwa siku ataitumia vipi? Chai tu asubuhi ili apate nguvu lazima apige chapati tatu(900) maharage ya jero na chai ya mia 2 jumla tu asubuhi (1,600/=) ,Mchana Ugali wa Buku Jero na usiku Wali wa Buku 2 ,nauli Tsh 2000 so matumizi ya siku ni Tsh 7000/= hapo hajanunua maji ,vocha ,umeme.
 
Eti usafiri buku mbili kwa siku.. Bange mbaya sana, hujui mtu anako ishi na bado unampanfia nauli kizembe hivo

Hayo ni makisio tu ya bajeti, unaweza ku adjust kulingana na mahitaji yako halisi. Msingi ni kuzingatia kipato cha laki tano. Unaweza kuta mwingine kwenda kazini kwake hata nauli hatumii kabisa.
 
Hayo makisio tu ya bajiti, unaweza ku adjust kulingana na mahitaji yako halisi. Msingi ni kuzingatia kipato cha laki tano. Unaweza kuta mwingine hata nauli hatumii kabisa
Mpaka hapa huu uzi hauna maana kabisa
 
Sawa sawa.. gotcha!

ila najaribu kujenga hoja nyingine hapa, sabb ikifika mahali kila mtu wa sekta rasmi na zisizo rasmi akiwa na uhakika wa kupata 1M kila mwezi, basi tujue gharama za life pia zitapanda, kuanzia house rent, fuel, medical bills, groceries, n.k.
Utashangaa purchasing power ya 1M ikawa sawa na 150K ya sasa.

Anyway, it's about uchumi na principles zake kwa social science, ili kupandisha kuna factors nyingi mno za kuzingatia vinginevyo inflation ya hatari itatokea.

Je solution nzuri itakuwa ni ipi?
1. Je, kuongeza paycheck kwa kila mtu?
2. Je ni kujaribu kucontrol inflation kwa mamlaka za udhibiti kwenye vitu muhimu vya basic needs? .
3. Kuongeza paycheck kwa kila mtu na pia kucontrol vitu.?
 
That time may never come. YOLO
 
Boom ni 250K mzee hio mambo ya stationary sijui Field ni mara moja kwa mwaka
 
Mzee unakumbuka ulienda kuchangia damu Muhimbii hili upate 25000 nilikuwa nakuangalia kwa nyuma unavyorudi nakuonea huruma 😂😂
Na hy 25k, buku 10k ilipotea Kwenye daladala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…