Mimi crush wangu nilidate nae form 3 mpaka O level inaisha, wakati nilimpenda tangu form 1 naogopa kumwambia. Sikuwahi kuwa na crush mwingine zaidi yake mpaka leo. After graduation alinambia anataka tupate mtoto anahisi siku zake za kuishi ni chache, nikaogopa na kufanya nae matusi tena.
Tuliachana rasmi after form 6 aliponishutumu kuwa simpendi ninamcheat. Wapambe walikuwa wengi baina yetu maana couple ilikuwa maarufu, taarifa zake nilikuwa nazo ila zangu hana. Long distance ilituharibia tukaachana kwa vitisho. Sadly, kama alijua vile kwani sahivi hayuko sawa kwa afya ya akili na kupona 100% sidhani.
Nilimpenda na alinipenda. Kwanza nilimtongoza leo akakubali kesho, tangu hapo nikitongoza mtu akanizungusha kidogo naacha najua akikubali kwa kuchelewa analazimisha. Pili, alikuwa ananijua in and out hata nimfiche. Mapema kabisa nilijua mwanamke akikupenda sana anajua kusoma emotions zako kwa kukusikia, kukushika au kukutazama.