Unamkumbuka Mussa Simba aka Black Moses: Huyu alikuwa bingwa wa Disco miaka hiyo

Halafu enzi hizo naona hazitojirudia tena yaan disco lilikuwa juu hatari...na wanamuziki wengi weusi wa marekani ndo walikuwa wanatamba hatari
 
Kama imeshapostiwa hapa please nisaidie
 
Daah! Nimekumbuka kuna mashindano yalifanyika fainali akaingia black moses na mc chunusi, mc chunusi akaibuka bingwa black musa akalalamika kaonewa akaomba warudiane mc chunusi akasema apewe milioni moja ili warudiane basi black musa akasema mnaona huyu haniwezi ndio maana kataja dau kubwa ili asijitokeze mdhamini wa kutoa hiyo hela, black musa alisema mc chunusi hana style kali zaidi ya kuigiza kama kilema
 
cassete za father wangu za mwaka 1989 ndio mpaka leo hii anazo . Cassete ya kwanza kabisa aliponunua redio cassete kwa mara ya kwanza kabisa. Lucky Dube ;think about the children" na Yvonne Chaka Chaka "who's the Boss"
 

Attachments

  • images.jpg
    35.2 KB · Views: 8
Ommy sydney,Askofu mmakua,Wanne star,Hassan mzanzibari duh list ndefu.Imenikumbusha mbali. Black Moses alikufa kwa kipindupindu bbada ya kulost sana huko mitaa ya Usagara mwanza akitoa shoo kwenye kumbi za vijijini.
 
Duh huenda nilikuwa najifunza kupiga mswaki enzi hizo. Ni miaka gani hao jamaa walikuwa wanatumbuiza?
 
Hakuwa mchezaji kivile ila ujinga tu wa wabongo walidhani jamaa anajua kucheza kumbe sivyo. Nilimshuhudia michezo yake na nikawa nawashangaa abongo wanampigia debe kwa misingi gani maana jamaa hakuwa anajuwa kucheza kivile, alikuwa wa kawaida sana.
Inawezekana wewe labda ulikaa nje huko so ukapata nafasi ya kuwaona dancers wa huko. Ila wengine wengi kwao alikuwa mkali sana.
 
Labda walimnyang'anya demu wake au dada yake alitiwa mimba na mmoja wao. Maana jamaa gubu lake kama la mke mwenza.
 
Enzi hizo ukiwa Mbowe ule mziki wa mwisho ndio unakupa akili utaingiaje home wakati ulitokea dirishani.
Yaani wewe usipotaja Mbowe hujisikii

Kumbi unazokumbuka ni Mbowe tu siku zote
Chama unachokijua ni cha Mbowe tu

Nini siri ya mafanikio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…