Unamkumbuka Mussa Simba aka Black Moses: Huyu alikuwa bingwa wa Disco miaka hiyo

Unamkumbuka Mussa Simba aka Black Moses: Huyu alikuwa bingwa wa Disco miaka hiyo

Halafu enzi hizo naona hazitojirudia tena yaan disco lilikuwa juu hatari...na wanamuziki wengi weusi wa marekani ndo walikuwa wanatamba hatari
 
Kuna mtu ameniambia ana mkanda wa VHS wa mashindano flani ya disco yalifanyika pale magomeni Kota(ccm ndugumbi) kulikuwa kuna ukumbi mkubwa sana wa Disco wale watu wa zamani kama mimi mtakumbuka SWEET CORNER DISCO TEQ ndani ya huo mkanda jamaa anakutana fainali na mtu mmoja anaitwa BOSCO COOL J noma sana nataka nikiupata nitaubadirisha kuja kwenye mp4 alafu nitaweka hapa muone huyo mtu alivyokuwa na kipaji cha aina yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama imeshapostiwa hapa please nisaidie
 
Daah! Nimekumbuka kuna mashindano yalifanyika fainali akaingia black moses na mc chunusi, mc chunusi akaibuka bingwa black musa akalalamika kaonewa akaomba warudiane mc chunusi akasema apewe milioni moja ili warudiane basi black musa akasema mnaona huyu haniwezi ndio maana kataja dau kubwa ili asijitokeze mdhamini wa kutoa hiyo hela, black musa alisema mc chunusi hana style kali zaidi ya kuigiza kama kilema
 
umegusa jambo muhimu sana.
miaka ya 90 mshua wangu aliporudi nchini akitokea masomoni ng'ambo alirudi na panasonic camera ya kurekodia video kwa kutumia kaseti za VHS.

naikumbuka vizuri ile camera maana ndio nilikuwa najifunzia kurekodi video kwenye sherehe mbalimbali za kifamilia.

ilikuwa niya kubeba begani..hii hapa katika picha.
View attachment 853283

kwetu hakuna sherehe yoyote ya kifamilia iliyopita bila kurekodiwa.
kabati letu la sebuleni lilijaa mikanda ya VHS.

ila kama unavyojuwa watz sio watu wa kutunza kumbukumbu pia hatuthamini kuweka rekodi, ilipofika miaka ya 2000 mpaka 2005,mikanda ya VHS yote ikaanza kupotea na mengine kuharibika kabisa. mpaka hii leo hakuna mkanda hata mmoja uliobaki.so sad aisee.
cassete za father wangu za mwaka 1989 ndio mpaka leo hii anazo . Cassete ya kwanza kabisa aliponunua redio cassete kwa mara ya kwanza kabisa. Lucky Dube ;think about the children" na Yvonne Chaka Chaka "who's the Boss"
 

Attachments

  • images.jpg
    images.jpg
    35.2 KB · Views: 8
Mkuu Digadiga wala hakuwahi kumsumbua marehemu black moses alikuwa mpinzani wa kawaida sana, watu ambao walikuwa wanampa shida kila mashindano ni super ngedere wa moro , Kelly John, Bosco cool, bob kassim, baucha hawa ndio watu walikuwa wanampa shida Black moses ilikuwa Black moses akisikia hawa niliokutajia wapo kwenye mashindano basi Black moses anajipanga kweli maana kazi iipo....digadiga alikuwa kama body flani hiv mara kibao baada ya matokeo anaanzisha fujo kaonewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ommy sydney,Askofu mmakua,Wanne star,Hassan mzanzibari duh list ndefu.Imenikumbusha mbali. Black Moses alikufa kwa kipindupindu bbada ya kulost sana huko mitaa ya Usagara mwanza akitoa shoo kwenye kumbi za vijijini.
 
Duh huenda nilikuwa najifunza kupiga mswaki enzi hizo. Ni miaka gani hao jamaa walikuwa wanatumbuiza?
 
Hakuwa mchezaji kivile ila ujinga tu wa wabongo walidhani jamaa anajua kucheza kumbe sivyo. Nilimshuhudia michezo yake na nikawa nawashangaa abongo wanampigia debe kwa misingi gani maana jamaa hakuwa anajuwa kucheza kivile, alikuwa wa kawaida sana.
Inawezekana wewe labda ulikaa nje huko so ukapata nafasi ya kuwaona dancers wa huko. Ila wengine wengi kwao alikuwa mkali sana.
 
kwa maelezo yako haya nimebaini enzi za utoto/ujana wako ulikuwa unasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia. kama sio depression basi itakuwa social anxiety.

wataalam wa masuala ya afya ya binadamu watakufafanulia. watafute wakusaidie.

kuna kitu hawa akina "black moses" walikufanyia enzi za ujana wako, sio bure. ila huwezi kukisema kwa kuogopa aibu.
Labda walimnyang'anya demu wake au dada yake alitiwa mimba na mmoja wao. Maana jamaa gubu lake kama la mke mwenza.
 
Enzi hizo ukiwa Mbowe ule mziki wa mwisho ndio unakupa akili utaingiaje home wakati ulitokea dirishani.
Yaani wewe usipotaja Mbowe hujisikii

Kumbi unazokumbuka ni Mbowe tu siku zote
Chama unachokijua ni cha Mbowe tu

Nini siri ya mafanikio
 
Back
Top Bottom