Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama imeshapostiwa hapa please nisaidieKuna mtu ameniambia ana mkanda wa VHS wa mashindano flani ya disco yalifanyika pale magomeni Kota(ccm ndugumbi) kulikuwa kuna ukumbi mkubwa sana wa Disco wale watu wa zamani kama mimi mtakumbuka SWEET CORNER DISCO TEQ ndani ya huo mkanda jamaa anakutana fainali na mtu mmoja anaitwa BOSCO COOL J noma sana nataka nikiupata nitaubadirisha kuja kwenye mp4 alafu nitaweka hapa muone huyo mtu alivyokuwa na kipaji cha aina yake
Sent using Jamii Forums mobile app
Nalikumbuka hilo pambano mzee, black moses alimaind sana kuwa kaonewaBila kusahau bingwa wa Kwanza wa disco tz kutoka mkoani.MC CHUNUSI Toka songea
cassete za father wangu za mwaka 1989 ndio mpaka leo hii anazo . Cassete ya kwanza kabisa aliponunua redio cassete kwa mara ya kwanza kabisa. Lucky Dube ;think about the children" na Yvonne Chaka Chaka "who's the Boss"umegusa jambo muhimu sana.
miaka ya 90 mshua wangu aliporudi nchini akitokea masomoni ng'ambo alirudi na panasonic camera ya kurekodia video kwa kutumia kaseti za VHS.
naikumbuka vizuri ile camera maana ndio nilikuwa najifunzia kurekodi video kwenye sherehe mbalimbali za kifamilia.
ilikuwa niya kubeba begani..hii hapa katika picha.
View attachment 853283
kwetu hakuna sherehe yoyote ya kifamilia iliyopita bila kurekodiwa.
kabati letu la sebuleni lilijaa mikanda ya VHS.
ila kama unavyojuwa watz sio watu wa kutunza kumbukumbu pia hatuthamini kuweka rekodi, ilipofika miaka ya 2000 mpaka 2005,mikanda ya VHS yote ikaanza kupotea na mengine kuharibika kabisa. mpaka hii leo hakuna mkanda hata mmoja uliobaki.so sad aisee.
Ommy sydney,Askofu mmakua,Wanne star,Hassan mzanzibari duh list ndefu.Imenikumbusha mbali. Black Moses alikufa kwa kipindupindu bbada ya kulost sana huko mitaa ya Usagara mwanza akitoa shoo kwenye kumbi za vijijini.Mkuu Digadiga wala hakuwahi kumsumbua marehemu black moses alikuwa mpinzani wa kawaida sana, watu ambao walikuwa wanampa shida kila mashindano ni super ngedere wa moro , Kelly John, Bosco cool, bob kassim, baucha hawa ndio watu walikuwa wanampa shida Black moses ilikuwa Black moses akisikia hawa niliokutajia wapo kwenye mashindano basi Black moses anajipanga kweli maana kazi iipo....digadiga alikuwa kama body flani hiv mara kibao baada ya matokeo anaanzisha fujo kaonewa
Sent using Jamii Forums mobile app
Inawezekana wewe labda ulikaa nje huko so ukapata nafasi ya kuwaona dancers wa huko. Ila wengine wengi kwao alikuwa mkali sana.Hakuwa mchezaji kivile ila ujinga tu wa wabongo walidhani jamaa anajua kucheza kumbe sivyo. Nilimshuhudia michezo yake na nikawa nawashangaa abongo wanampigia debe kwa misingi gani maana jamaa hakuwa anajuwa kucheza kivile, alikuwa wa kawaida sana.
Labda walimnyang'anya demu wake au dada yake alitiwa mimba na mmoja wao. Maana jamaa gubu lake kama la mke mwenza.kwa maelezo yako haya nimebaini enzi za utoto/ujana wako ulikuwa unasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia. kama sio depression basi itakuwa social anxiety.
wataalam wa masuala ya afya ya binadamu watakufafanulia. watafute wakusaidie.
kuna kitu hawa akina "black moses" walikufanyia enzi za ujana wako, sio bure. ila huwezi kukisema kwa kuogopa aibu.
Aliitwa Abdulhakim Magomelo (Mwenyezi Amrehemu) na kampuni yake "Kim & The Boyz".....Enzi hizo disco lilikuwa juu sana,hivi Abrahamu Magomelo yupo hai?..
Usimsahau nigger j enzi hizo,ambae ndio huyu masoud masoud,chini ya usimamizi wa the late choggo slyBlackMoses na Athumani Digadiga na kina Bosco CoolJ walitikisa jiji enzi zao.
Nigger J alikuwa Dj na sio dancer bila shaka. Chogole Selemani aka Choggy Sly.Usimsahau nigger j enzi hizo,ambae ndio huyu masoud masoud,chini ya usimamizi wa the late choggo sly
Kwahiyo hawa familia nzima walikua madansa?Huyo wa juzi tu,akina Moses walicheza na mama yake huyo dogo alikua anajiita Janet Jackson
Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani wewe usipotaja Mbowe hujisikiiEnzi hizo ukiwa Mbowe ule mziki wa mwisho ndio unakupa akili utaingiaje home wakati ulitokea dirishani.
We kweli mbongo halisiHAKUNA, wote walikuwa ma alosto tu.
Masoud wa Tbc?Usimsahau nigger j enzi hizo,ambae ndio huyu masoud masoud,chini ya usimamizi wa the late choggo sly
Kwahiyo hawa familia nzima walikua madansa?