Unamkumbuka Taribo West wa Nigeria, siku hizi ameokoka na ni mchungaji

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Taribo West mchezaji wa zamani wa Nigeria kwa sasa ameokoka na ni mchungaji kanisani kwake. Kanisa lake ni la miujiza na limeanza kuwa na waumini wengi siku baada ya siku.

Taribo alijipatia umaarufu akiwa anacheza soka, huku akiwa na style yake ya kusuka nywele na kuzipaka rangi ya kijani.
 
Sura ya Mchungaji ni kama ya Taribo West ni kama siyo ya Taribo West.

Ila yote kwa yote jamaa nilikuwa namwelewa sana, nimetunza picha zake za kwenye jojo akiwa na akina Finidi George, Captain Sunday Oliseh, Victor Ikpeba, JJ Okocha, Uche Okwechukwu,n.k, nilizozipata baada ya kununua jojo (big G) wakati nasoma Wailes Primary School mwaka 1998. Picha ninazo hadi leo. Ile Nigeria nilikuwa naipenda.
 
Enzi hizo Africa ilikuwa inazalisha talents kubwa sana.
 
Sitasahau lile shuti la Sunday Oliseh alilowafunga Spain,

Mkuu umemsahau mtu makini sana, Rashid Yekini R.I.P
 
Sitasahau lile shuti la Sunday Oliseh alilowafunga Spain,

Mkuu umemsahau mtu makini sana,Rashid Yekini R.I.P
Oo oo ooh! Lile halikuwa shuti, ilikuwa ni supersonic missile ilipigwa mita nyingi sana, almost katikati ya uwanja. Oliseh alifanya balaa.

Nilikuwa nimekaa sakafuni kwenye sebule ya jirani na nilishtukia tu Niko hewani nashangilia. What a good memory!🙆
 
We angalia mwaka 99 akiwa inter millan au AC millan eti alikuwana miaka 25,kama ameokoka atubu kwanza dhambi ya kudanganya umri
Nayenyewe ni dhambi tu,watu wa Mungu
Hivi Tinubu ana miaka 72?

Lakini umri wake uliathiri kiwango chake??
 
One of the most overated player,akiwa anacheza mpira umri waje ulikuwa unafikirisha sana,sura yamiaka 40 tukaambiwa ana 25.
Huyu alipunguza miaka si chini ya 15
Na sasa unamkadiria akiwa na umri gani?
 
Kidaftari cha stika za wachezaji, unakuwa unatazama kama albam za picha na washikaji, enzi hizoo
 
Wale ndio walikuwa truly the super eagles.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…