Dalili za Mtu Anayefikiria Kujiua
1. Kuelezea hisia za kukata tamaa, au kujiona hana maana katika jamii.
2. Kujitenga na shughuli za kijamii tofauti na mwanzo, mfano hataki tena kwenda out, kujiunga kwenye shughuli za sherehe au misiba etc, au kuacha kucheza au kutembelea au kutembelewa na wenzake kama ni teenager/mtoto
3. Kuwa na mood swings mfano huzuni, hasira, wasiwasi, au ukimya tofauti na kawaida yake
4. Kuanza kugawa vitu vyake vya thamani, au alivyokuwa anavipenda zaidi hapo mwanzo, mfano nguo, pesa, picha nk, hii inaweza kuonesha kuwa anajiandaa kuondoka
5. Kuongezq au kuanza kutumia vilevi hasa pombe au hata madawa. Athari ya vilevi ni kuficha tatizo kwa muda mfupi kwake, hali inayoweza kuzalisha maamuzi ya kujitoa uhai anapokosa amani anayoitafuta, au kuzalisha tatizo jingine la kifedha na kuongeza msongo wa mawazo.
6. Utulivu wa ghafla: Hii inaweza kuja baada ya mhanga kupitia kipindi cha kuvurugika hisia , ghafla anakuwa mtulivu au mwenye amani, jambo linaloweza kuonyesha kuwa ameshafikia kabisa maamuzi ya kujiua na haogopi tena, anaamini kabisa ni suluhisho la kudumu.
7. Kuonesha dalili za kutokujali, kukosa empathy kwa wengine au kwake mwenyewe. Hapo shida tatizo limeshamzidia haoni chochote kinachotokea kwake au anachofanya kwa wengine kama ni ishu tena.
8. Kuzungumzia mara kwa mara kuhusu kifo au kujiuwa: Hii ni kwa wale ambao wanaweza kuongea, ni "a cry for help, " chukulia kama ni bahati sana maana kuna wale ambao hawaongei kabisa. Mtu anayeongelea kujiua ana nafasi kubwa ya kupata msaada kuliko anayekaa nalo moyoni, huyu mtakutana tu na maiti yake.
9. Kuacha kujijali. Mfano katoka usafi wa mwili, mavazi, makazi, ulaji (kupungua uzito au hata kunenepa inategemea hali au anakula sana ba anakuwa inactive, yote yanawezekana), pia kutojali muda, ratiba au ahadi anazopanga na wengine.
Toa msaada kwa kuzungumza naye. Lakini usijione kama anaweza kufunga kila kitu kwako, jambo zuri ni kuwasiliana na unayeona anamwamini zaidi.
Pia kibongobongo watu wanapopitia shida hatujui kudeal nao kabisa. Kati ya vitu vinavyoweza kufanya mtu ajiue ni tabia zetu za kusambaza maneno ya kile mwenzako anapitia, umbea na tabia za kuhukumu watu wanapopitia matatizo, au kukaa kimya kana kwamba huoni mabadiliko mtu anayopitia. Usichujulie shida za mtu kama fursa za kusambaza maneno, hakuna tuzo utapewa, ila akisikia shida zake zimesambaa kwa watu utakuwa umetia petroli kwenye moto, yaani hali yake itakuwa mbaya zaidi. Kama huwezi kusaidia, kaa kimya. All in all, mtafutie msaada wa kitaalam na uoneshe upendo.