Unamsaidiaje mtu anaetaka kujiua?

Unamsaidiaje mtu anaetaka kujiua?

Ngumu saaana kuzuia dhamira iliyo moyoni mwa mtu,

Nakumbuka nilimwahi mmoja nikamfungua kitanzi nikambembeleza nikamwelekeza na n.k lakin siku ya siku usiku alitekeleza dhamira yake
 
Inategemeana na kiwango cha maumivu ya mhusika
yeah ni kweli
Scenario 1
Mtu kafilisika ndugu hawamtaki tena hana pa kula,kulala hana tumaini tena.

Scenario 2
Binti kabakwa anaona aibu watu wakijua na anaona hana umuhimu wa kuishi tena

Scenario 3
Mtu kabet pesa ndefu na kaweka pesa yake yote inaliwa

Scenario 4
Mtu kaachwa na mpenzi/mwenza wake anaempenda na aliejitoa kwake kwa kila namna.
 
Msaada wa haraka, mwambie ndugu subiri kidogo, hiyo kamba ipo kwenye tawi dogo inaweza kukatika haraka kabla hujafa, sogeza kwenye lile tawi kubwa haitakatika. Maneno haya yanaweza kurejesha ufahamu wake haraka na utasikia kumbe hunipendi kiasi hichi. Baada ya hapo hatakuwa na hamu ya kuendelea na adhima yake ya kujiua. Hekima nyingine Mungu anaweza kukusaidia namna ya kufanya kwa wakati huo.
 
asante mkuu imekaa kikawaida sana lakini ni good psychological manipulation trick that can save a soul.
 
asante mkuu imekaa kikawaida sana lakini ni good psychological manipulation trick that can save a soul.
Kabisa, wewe hutotumia muda wako kupingana naye kwa maamuzi yake, wewe sapoti maamuzi yake kwa njia ambayo hakutarajia kabisa. Tena usiwe na utani uwe siriazi na kazia baadhi ya maeneo utamwona anashuka mwenyewe bila kutumia nguvu. Ukianza kumbebeleza ndio unampoteza kabisa.
 
Habari za wakati huu wakuu.

Wakubwa shikamoo, madogo wozah niaje.

Kuna ongezeko kubwa la kesi za watu kujiua kwa mambo mbalimbali, hata huku kuna dogo alimaliza la 7 akakataa shule, wazazi wakaforce sana akagoma, siku hio mzee wake akadamka akampiga biti dogo kama nikirudi hujaenda shule uhame hapa, dogo akajiua.

Ukigundua mtu anataka kujiua unamsaidiaje wakuu maana tunapoteza ndugu,jamaa,na marafiki zetu huenda ushauri wenu ukaokoa maisha ya mtu one day.
Njia rahisi ni kutoa taarifa hospitali kuna wataalam wa ushauri. Or else fika ofisi ya mganga mkuu wa wilaya wa eneo hilo. Sure unaweza kukutana na hali ya kutokukuchukulia serious, ni weakness za system zetu but, anapaswa atafute mtu wamsaidie ndugu yako.
 
Hakuna maisha mazuri kama hayo unayoyaoshi sasa, tatizo linakuja nikutaka kuishi maisha ya mtu au watu wengine na hapo ndio linapokuja tatizo ya ugumu wa maisha

Be real & live your life
 
Njia rahisi ni kutoa taarifa hospitali kuna wataalam wa ushauri. Or else fika ofisi ya mganga mkuu wa wilaya wa eneo hilo. Sure unaweza kukutana na hali ya kutokukuchukulia serious, ni weakness za system zetu but, anapaswa atafute mtu wamsaidie ndugu yako.
shukrani kiongozi neno lako laweza kuokoa maisha ya mmoja wetu ubarikiwe sana.
 
Zaidi ya kumpa ushauri au kumpeleka Kwa wataalamu wa saikolojia, sidhani kama Kuna msaada mwingine zaidi ya kumwachia Mungu
 
Kwa kijana mdogo kama huyo ni kumpiga tu mkwara kuwa anaejiua anaenda moja kwa moja motoni, Mungu hapokei wanaojiuwa. Motoni ni mateso ya milele.
 
Back
Top Bottom