MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
- Thread starter
- #81
Wewe mjinga mmoja usipochangia mjadala haidhuru.Tu
Tuletee kwanza picha ya amida.. ndo tuendelee na mjadala
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe mjinga mmoja usipochangia mjadala haidhuru.Tu
Tuletee kwanza picha ya amida.. ndo tuendelee na mjadala
Acha kujidanganyaAmida wenyewe wanasema ana nyota kali sana, yaan ukiwa na Amida nyota yako pia inahamia kwake ndio maana baada ya hao wote kua nao hakuna aluyepata kua na muendelezo mzuri, JB (Jibe) hakutoa tena zile hit song, hao matajiri wamefirisika na mpaka sasa ameolewa tena huyo Dada na tajiri mwingine,
Naona unahasira za masanja kutomuacha mke wake.pole Chawa wa katibuWewe mjinga mmoja usipochangia mjadala haidhuru.
Jifunze kuwa na nidhamu.Naona unahasira za masanja kutomuacha mke wake.pole Chawa wa katibu
DRC wanabadilishan ndoa kama kitu cha kawaida: jiulize Mbilibel alipofunga ndoa ya mkataba na Tab ley-------- mbilia bel hakuwa na ndoa?, Tab ley hakuwa an mke?, .Kwa Congo ndoa hazifafanani na za watanzaniaMfano mzuri ni wapi?
Mwana, wa kwangu akitoka tu nje ya lile geti pale kwa sababu za kingono nje na mimi, hatarudi tena hata afanyeje, ataenda popote hatapata msaada, inawezekana hujajua nini maana ya MWANAUME, Mpiana atakua ni mtoto wa kiume na si MWANAUME... MWANAUME yoyote ni SIMBA wa nyikani asiyetishwa, usifundishe watu ushoga shogaKwanza nawasalimu kwa jina la Chama Pendwa CCM.... Yaani penda usipende CCM imebeba matumaini yako kama mtanzania.
Tukirudi kwenye lengo la uzi ni kwamba nimeshangazwa sana na watu wanaomshambulia mmiliki wa kanisa la Feel-Free, comedian Masanja Mkandamizaji kwa kumsamehe mkewe anayesemekana kuisaliti ndoa yao. Wananchi wengi wameonyesha kushangazwa na ujasiri wa Masanja kuweka msimamo wa kumpenda mkewe hata ikitokea kamfumania LIVE kwenye lile tendo. Binafsi naweza sema wengi wa watu wanaomshangaa Masanja hawana mapenzi ya dhati.
Tutazame kidogo mwanamuziki tajiri toka DRC, JB Mpiana ili kuweza kutukumbusha mapenzi ya dhati yapo na pia msamaha upo kwa mtu unayempenda kwa dhati. Kwa wasiomfahamu JB Mpiana mfahamu kuwa huyu ni mwanamuziki mwanzilishi wa bendi maarufu sana ya Wenge Musica iliyotamba sana miaka ya 90. Wakati Wenge ikitamba huyu JB Mpiana ndo alikuaa kiongozi wa kundi akiwa na wenzake kina Werrason, Didier Masela, Alain Makaba, Adolphe Dominguez, Blaise Bula, Titina Alcapone, Tutu Kaludgi, na Roberto Ekokota. Lilikuwa kundi la moto sana kwa bahati mbaya likasambaratika na kuibuka kwa bifu kali sana toka kwa miamba miwili, JB Mpiana na Werrason.
JB Mpiana alikuwa mume halali wa mwanamama Amida Shatur na kubahatika kupata watoto watatu, Daida, Soraya na Junior. Lakini mnamo mwaka 2002, mwanamama Amida alimwacha JB Mpiana na kwenda kuolewa na bilionea wa madini aitwaye Didi Kinuani. Katika ndoa yao, Didi na Amida walifanikiwa kupata mtoto mmoja aitwa Diam. Lakini kwa kuwa kunguru hafugiki, zikaanza tetesi za Amida kuchepuka na bilionea mwingine aitwae Vital Kamerhe kitu ambacho Didi Kinuani hakuweza kuvumilia na kuamua kumpa talaka mkewe Amida. Katika muda wote huo wa ndoa ya Didi Kinuani na Amida, yeye JB Mpiana alikuwa single.
Ikiwa ni karibu miaka nane imepita baada ya kuachana na mkewe, June 2, 2009, supastaa JB Mpiana kwenye sherehe za kutimiza miaka 42 ya kuzaliwa, aliwashangaza watu waliohudhuria tafrija Grand Hotel Kinshasa kwa kuwatangazia kurudiana na mkewe Amida aliyeachika kwa Didi Kinuani. Na hakuishia hapo tu, alimpa zawadi pia mbele ya wageni waalikwa. Hili jambo liliushangaza umma kwasababu wengi walikerwa na jinsi Amida alivyomuacha Mpiana na kwenda kwa bilionea Didi. Mwanamuziki Werrason pamoja na kuwa walikuwa kwenye bifu zito na JB Mpiana baada ya kundi lao la Wenge kusambaratika ila naye alikataa dili la kwenda kutumbuiza kwenye harusi ya Didi Kinuani na Amida kwasababu ilimuuma kuona ndugu yake alichofanyiwa.
Furaha ya JB Mpiana ilikoma rasmi tena kwa mara ya pili February 14, 2019 pale mkewe alipomuacha tena na kwenda kuolewa na mchepuko wake wa muda mrefu bilionea Vital Kamerhe. Kinachouma zaidi ni kwamba binti zake Mpiana, Soraya na Daida, walihudhuria hii harusi ya mama yao na baba yao wa kambo Vital Kamerhe. Kwenye ndoa yao, Kamerhe na Amida wamebahatika kupata mtoto Isaac.
Ni kwamba tukiachana na hayo matukio rasmi ya ndoa, Mpiana amekuwa mara nyingi akiachwa na mkewe na kurudiwa baadae. Na mara zote Mpiana amekuwa akimsamehe mkewe kuanza mahaba upya. Tofauti na Masanja utaona Mpiana wabaya wake ni mabilionea ambao pia wana nguvu sana kisiasa. Vital Kamerhe ni katibu kiongozi kwenye serikali ya Tshisekedi huku Didi Kinuani akiwa ni mfanyabiashara mkubwa wa madini huku akihusishwa na kunufaika wakati wa vita huko Angola. Yaani hakuna kitu atawafanya.
Kitu wanachofanana Masanja na Mpiana ni utajiri. Wote wawili wana pesa za kutosha ila kwa bahati mbaya kwenye mapenzi ni mafukara. Ni wito wangu kwa watu wengine kusamehe wake zao wanapoachika na wapenzi wao. Hata kama atarudi na mtoto kama ilivyokuwa kwa JB na Amida.
Ni demu ya kisasaAmida na Kamerhe.View attachment 2379866
Lemutuz hana ishu maana anarudia rudia post zake na kuwaambia watu ITAENDELEA...Huyo Amida akueleze Lemutuz ndio utafurahi.
KabisaNoma Sana. Huo Moyo kwakweli Mimi sina hata kama nina madhambi yangu mengi Sana.
KabisaDRC siyo mfano mzuri
Kinukta ndio niniYaaan Hamida ni kicheche kama Jlo na kuzaa anazaa na hao mabilionea halafu JB kimya kama senge hivi[emoji57][emoji57]
Itakuwa ana kinukta si bure
Huwezi linganisha Mukulu ya Bhakulu ya Lunda na hiyo Scenario ya huyo takataka...Ukipata unayempenda utasamehe kama Masanja