Mkuu huyo kijana mwambie aende akaombe kazi kwenye makampuni ya ulinzi makubwa mfano G4S au GARDA WORLD.
Mara nyingi kwa kijana ambaye hana connection, hizi kazi za ulinzi huweza kumexpose kijana au kumuweka kwenye platforms flani ambazo ni rahisi yeye kuonekana / kuonana na watu wengi wazito ambao ni ngumu kuonana nao in a normal way.
Mfano akishaajiriwa, anaweza kuwekwa kwenye malindo nyeti kama Mahoteli makubwa (SERENA, HYYAT ,SLIP WAY, CORAL BEACH, n.k) au ofisi za BALOZI mbalimbali mfano Us embassy, EUROPEAN UNION, TURKEY EMBASSY, n.k, au pia anaweza akapangiwa lindo la mtu binafsi mwenye pesa zake, au makampuni mbali mbali ambapo kiuhalisia yatampa EXPOSURE nzuri sana. Maeneo haya ni rahisi sana Mlinzi mwenye sifa za kitaaluma kupata kazi endapo zikitangazwa, kwanza ni rahisi kuaminika na kupewa kipaumbele kuliko mtu mwingine wa nje.
Kazi ya ulinzi ni kazi nzuri sana kwa kijana anayetaka kutafuta exposure na connection huku akiendelea kusubiri na kupambania ajira ya ndoto yake aliyosomea japo sometimes anaweza pia akajikuta amepata michongo mingine mikubwa out of profession yake.
NOTE
Mungu humsaidia anayejisaidia, usitegemee miujiza ikukute huku ukiwa unashinda ndani tu unafungua mahotpot ya vyakula na kulala kama mjamzito. Ulinzi ni kazi ngumu , akubali kudharaulika, kufubaa,,kukosa usingizi,,kurisk maisha yake (kuuza roho) na mengine mengi.