Unamshauri nini kijana asiye na ajira ambaye yupo tu mtaani?

Unamshauri nini kijana asiye na ajira ambaye yupo tu mtaani?

Kumbe unaozeshwa, unaoewa na vitu
Ndio hio ni huko bush uko unaozeshwa yaan mke unapewa ni wazee wanaokuchakulia tu mke wanakuozesha na plot unapewa maana huko bush kuna maeneo makubwa tu hayafanyiwi chochote na wanyama wa kufuga yaan mifugo unapewa, anza maisha sasa sio huku town nani atakupa hivyo vyote?

Huku town Issue ni kutunga ndoa ya uongo na ukweli upate mtaji watu watachangishana michango ya huku na kule tembeza kadi za harusi door to door sasa ile michango michango ndio mtaji wako wa kuendeshea maisha hapo bado haujahesabu zawadi za hapa na pale utakazopewa na ndugu, jamaa na marafiki

Chukulia kadi moja mtu mmoja achangie 50,000/- wakiwa wawili wachangie 70,000/-

Wakichangia watu 100 tu

100×50,000 = 5,000,000

Hapo bado kuna wale wa kujitolea kulipia ukumbi na wakulipia misosi na kumlipa MC huku 5M bado inapumua

Hilo nimepiga kadrio la chini

Baada ya hapo songa mbele ushapewa mtaji tayari unasubiri nini? Au bado haujaisoma akili yako?
 
Kama Ni graduate na hana mtaji namshauri awekeze kwenye TECHNOLOGY kwasababu Tech ndio #Industry pekee unaweza kuanza kwa mtaji mdogo ukakua kwa haraka zaidi
#Ndio industry yenye future unaweza kuanza kwasababu huna mtaji wakutosha na ukajenga future yako humohumo
#Industry pekee hata mwenye mtaji mdogo anafanya kazi bila kutoka jasho wala kidharirika

Kwanza atafute kibarua Cha kumpatia pesa ya kula na bando hata 3000 per day then awekeze kwenye Niche yoyote kwenye Tech kwa mida wa miezi 5 anaweza yaona matunda

Traditional Business nyingi huwezi kuanza bila kuwa na mtaji wa kueleweka 1M kwenda juu chini ya hapo utakuwa machinga na Graduate na umachinga sivizuri.
 
Q
Ndio hio ni huko bush uko unaozeshwa yaan mke unapewa ni wazee wanaokuchakulia tu mke wanakuozesha na plot unapewa maana huko bush kuna maeneo makubwa tu hayafanyiwi chochote na wanyama wa kufuga yaan mifugo unapewa, anza maisha sasa sio huku town nani atakupa hivyo vyote?

Huku town Issue ni kutunga ndoa ya uongo na ukweli upate mtaji watu watachangishana michango ya huku na kule tembeza kadi za harusi door to door sasa ile michango michango ndio mtaji wako wa kuendeshea maisha hapo bado haujahesabu zawadi za hapa na pale utakazopewa na ndugu, jamaa na marafiki

Chukulia kadi moja mtu mmoja achangie 50,000/- wakiwa wawili wachangie 70,000/-

Wakichangia watu 100 tu

100×50,000 = 5,000,000

Hapo bado kuna wale wa kujitolea kulipia ukumbi na wakulipia misosi na kumlipa MC huku 5M bado inapumua

Hilo nimepiga kadrio la chini

Baada ya hapo songa mbele ushapewa mtaji tayari unasubiri nini? Au bado haujaisoma akili yako?
Mkuu kwa ulichoandika bilashaka wewe ni kutokea familia za kitajiri

Mtu ambae anaweza kuchangiwa hivyo kwenye harusi yake hawezi kuja hapa JF kulia kuwa anasota
 
Kwanza atafute kibarua Cha kumpatia pesa ya kula na bando hata 3000 per day then awekeze kwenye Niche yoyote kwenye Tech kwa mida wa miezi 5 anaweza yaona matunda
Sehemu pekee ambayo vijana wanaweza wanapata easy money per day ni viwandani ambapo wanalipa from 5k to 20k/25k per day huyo ni kibarua lakini kuipata hio connection ya kupiga kazi kiwandani kwanza ujuane na HR pili ujuane na Maboss wa kiwanda husika apart from that endelea kusugua bench

Kingine kuhusu issue za tech zinahitaji mtaji pia usichukulie simple simple mkuu mtaji ndio tatizo
 
Q

Mkuu kwa ulichoandika bilashaka wewe ni kutokea familia za kitajiri

Mtu ambae anaweza kuchangiwa hivyo kwenye harusi yake hawezi kuja hapa JF kulia kuwa anasota
Bado haujanielewa vizuri soma ukiwa umetulia utanielewa namaanisha nini
 
Nadhani kila moja wetu anafahmu kuwa hali ya maisha now imekuwa ngumu hususani kwenye swala zima la kipato na matumizi yapo juu sana. mpaka inapelekea maisha yanakuwa magumu sana, kila mtaa utakao pita utakuna na bodaboda.

Siyo kazi mbaya ila ndio kazi ambayo vijana wengi wanaweza kuifanya kupata ridhiki zao.

Sasa leo mchana nilikaa na ndugu yangu yeye kamaliza chuo lakini yupo tu mtaani, kaniuliza hivi kama nikikuomba ushauri nifanye kazi ili niingize kipato utanishauri nifanye kazi gani ghafla ghafla nimekosa jibu la kumpa.

Enyi wana jamiiforums naomba tushirikiane katika kutoa mawazo ya idea za biashara zenye uitaji wa mtaji wa kuanzia laki 1 na nusu hadi laki 3 ambazo zinaweza kuwasaidia hawa vijana wasio na ajira kuingiza kipato

Karibuni kwenye mjadala
Kwa uzoefu wangu mdogo nilionao kuhusu mtaa, ni mkwamba mtaji wa laki 1 au 3 ni ngumu mno kutoboa (ingawa mtaji wakati mwingine siyo hoja sana), ila wachache sana wanatoboa na hicho kiwango cha mtaji. Sasa ninachoweza kumshauri ni kuweza kujitofautisha na vijana wengine kwa kujiongezea elimu zaidi, ujuzi na maarifa. Kwamfano anaweza akaomba kufanya kazi mahala kwa kujitolea ili kupata uzoefu na ujuzi zaidi, baada ya hapo atakuwa kwenye nafasi ya kuajirika, tena pengine kwa maslahi mazuri tu.
 
Sehemu pekee ambayo vijana wanaweza wanapata easy money per day ni viwandani ambapo wanalipa from 5k to 20k/25k per day huyo ni kibarua lakini kuipata hio connection ya kupiga kazi kiwandani kwanza ujuane na HR pili ujuane na Maboss wa kiwanda husika apart from that endelea kusugua bench

Kingine kuhusu issue za tech zinahitaji mtaji pia usichukulie simple simple mkuu mtaji ndio tatizo
Kuna namna jamaa una Manipulate Sana Data zako unapoandika kuhusu pesa, kiwandani mishe nyingi amount per day ni 5000 mpaka 10,000 maximum hiyo ndiyo 90% ya viwanda ukiona mtu anapata 25K kiwandani basi hiyo kazi anayofanya ukipewa unakimbia sikuhiyohiyo.

Kuhusu Tech hakuna niliposema huitaji mtaji soma Hints zangu kwa umakini sana ukishindwa kwenye Tech kwa kipengere Cha mtaji sahau kabisa kuhusu kujiajiri hii Dunia kwa kigezo cha mtaji...Tech ndio sehemu inayotoa nafasi kuanza na mtaji mdogo zaidi.
 
Una uzima bas hushindwi kitu. Yaani Kaz zpo ila wahitaji hawapo. Watu wamesoma wanataka kukaa oficin
 
Atafte kazi ya sales tu, hawezi kushinda njaa japo mishahara midogo ila kuna kaunafuu mkuu. Kazi za sales kuzipata ni rahisi kidogo kwa kuwa ni za kuhenya ila akipata connection na kampuni tu maisha yanakuwa mepesi.
Kabisa,kwa Sasa kazi za sales ni nyingi saana na zimekuwa wazi. Ni suala ya uvumilivu,jitihada na kuamini kuwa Mungu anakuona ukipambana.
 
Mkuu umeona jambo hapo kumbe, akili inaamka na baraka zinaongezeka zenyewe ila asikosee kuoa mwanamke asieleweka atadata na kusaga meno na majuto ndio atakua mjukuu wake
Kweli swala la kuoa ni mchakato unaohitaji kutulia sana
 
Atafte kazi ya sales tu, hawezi kushinda njaa japo mishahara midogo ila kuna kaunafuu mkuu. Kazi za sales kuzipata ni rahisi kidogo kwa kuwa ni za kuhenya ila akipata connection na kampuni tu maisha yanakuwa mepesi.
True bro sema hapo kwenye uvumilivu ndio muhimu zaidi, maana sales ukijaliwa sana utapewa nauli na hadi ufanye sales za kukupa comission ya maana, kwa mwezi wa kwanza sio rahisi

Ila kama ulivyosema, ukiwa vizuri kwenye sales, kuingia vitengo vingine ni rahisi zaidi
 
Back
Top Bottom