Unamshauri nini kijana asiye na ajira ambaye yupo tu mtaani?

Mkuu kwa sasa nafasi za kujitolea ni kama kuomba kazi tu nazo mpaka connection
Anaweza hata kujifunza fani yoyote nyingine mtaani itakayomuingizia kipato, zipo shughulu ambazo zinachukuliwa poa sana mtaani, lakn zinaingiza kipato kinachoweza kufaa kujikimu. Siyo lazima kuangalia zaidi ajira inayohitaji elimu ya darasani.
 
Kama fani zipi???
Kama hadi na hizo fani unahitaji tukuchagulie mzee baba... Bas endelea tu kuaa home kwanza. Ahh namaanisha aendelee kukaa home kwanza huyo jamaa. Mbona zipo nyingi tu, ni hizo shughuli unazoona semi skilled labour wanafanya.
 
Shida ni kwamba kila kijana aliyehitimu anapenda kuajiriwa kazi za ofisini.....lakini kama atapata fursa ya kulima basi ajikite kwenye kilimo tena kwa jembe la mkono...baada ya miaka miwili/ mitatu hawezi kulia njaa, aende vijijini ajiunge na vijana wanao fyatua tofali za kawaida ndani ya miaka michache atasimama vizuri kwa miguu yake
 
Watu mnarahisha sana mambo...mtu umechoka nani anakuchangia hizo hela[emoji3]

Ili uchangiwe lazima na ww uwe na hela/mtaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipo Karibu na viwanda flani min Ni 5000 ila mambo ya kichanganya Ni 2500O per day Ila niliacha baada ya kuona sio tu ngumu Bali unsafe watu kukatika vidole Ni kawaida
 
Distilled water Ni pure water unaweza uza kiwandani kwenye maabala achana na hao watu wa saluni sijui mgahawa kwanza hayafai kwa chakula
 
Nchi imejaa wasomi hawana nyuma wala mbele.

Wazazi wamechoka kununulia kifurushi,

Bahati ilimwendea mmoja tu Majaliwa,
 
Mkuu huyo kijana mwambie aende akaombe kazi kwenye makampuni ya ulinzi makubwa mfano G4S au GARDA WORLD.

Mara nyingi kwa kijana ambaye hana connection, hizi kazi za ulinzi huweza kumexpose kijana au kumuweka kwenye platforms flani ambazo ni rahisi yeye kuonekana / kuonana na watu wengi wazito ambao ni ngumu kuonana nao in a normal way.

Mfano akishaajiriwa, anaweza kuwekwa kwenye malindo nyeti kama Mahoteli makubwa (SERENA, HYYAT ,SLIP WAY, CORAL BEACH, n.k) au ofisi za BALOZI mbalimbali mfano Us embassy, EUROPEAN UNION, TURKEY EMBASSY, n.k, au pia anaweza akapangiwa lindo la mtu binafsi mwenye pesa zake, au makampuni mbali mbali ambapo kiuhalisia yatampa EXPOSURE nzuri sana. Maeneo haya ni rahisi sana Mlinzi mwenye sifa za kitaaluma kupata kazi endapo zikitangazwa, kwanza ni rahisi kuaminika na kupewa kipaumbele kuliko mtu mwingine wa nje.

Kazi ya ulinzi ni kazi nzuri sana kwa kijana anayetaka kutafuta exposure na connection huku akiendelea kusubiri na kupambania ajira ya ndoto yake aliyosomea japo sometimes anaweza pia akajikuta amepata michongo mingine mikubwa out of profession yake.

NOTE
Mungu humsaidia anayejisaidia, usitegemee miujiza ikukute huku ukiwa unashinda ndani tu unafungua mahotpot ya vyakula na kulala kama mjamzito. Ulinzi ni kazi ngumu , akubali kudharaulika, kufubaa,,kukosa usingizi,,kurisk maisha yake (kuuza roho) na mengine mengi.
 
Nchi imejaa wasomi hawana nyuma wala mbele.

Wazazi wamechoka kununulia kifurushi,

Bahati ilimwendea mmoja tu Majaliwa,
Dah hali ya ajira ni ngumu mama.ila Mungu umpa mtu kwa wakat wake tuendelee kupambana.
 
Njoo dm, nikupe mchongo wa ajira. Wakala wa ajira serikalini na sekta binafsi
 
Ajifunze kuogelea
Ashinde maeneo ya maziwa...
Aombe neema kama ya majaliwa
Napita tu..asiombee ajali
 
Aende sokoni atoe aibu achague kitu kimoja auze weather ni matunda, dagaa au mboga za majaniii akikomaa mwezi mmoja hayo mawazo ya ujobless yataisha na uzuri mtaji wa sokoni unaanza hata na laki 2 tu inatosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…