Unamshauri nini kijana huyu wa zaidi ya zaidi ya miaka 40, ambaye hajaoa, hana mtoto wala ajira mpaka sasa anakaribia kutokua na sifa za kuajiriwa?

Unamshauri nini kijana huyu wa zaidi ya zaidi ya miaka 40, ambaye hajaoa, hana mtoto wala ajira mpaka sasa anakaribia kutokua na sifa za kuajiriwa?

40 ni mtu mzima huyo, ameshatoka kwenye ujana... Na umri huo ndio umri ambao wanaume wengi wanachanganyikiwa wasipokua vizuri.

Daah! pagumu hapo, ila kama mentality yuko fit anauwezo wa kufanya jambo maana ukiangalia watu wengi waliofanikiwa wengi wao walifanikiwa wakiwa kwenye umri huo ingawa wengi walianza kujitafuta mapema na hapo ndio wakajipata, ila kwa yeye ambae hajawahi kuanza chochote inabidi aanze chochote tu kwanza😅😅😅
 
Akae mbali na Ccm na asiwe chawa Kama kaka yake mwenye 50+ Ila analipwa 7K Kwa uchawa
Gentleman,
ndio maana haijulikani JF utaacha nini ile safari yako uliyoitangaza kwenye uzi Fulani ikiwadia kama mambo yenyewe ndiyo haya dah!🐒
 
Miaka 40 Bado kijana.mini Nina miaka 50 na Bado najiona ni kijana
umetisha sana gentleman 👊💪

unamhauri nini huyu ambae anazurura na kujificha ficha tu mjini na hana mbele wala nyuma?🐒
 
Cha kumwambia huyo Bwana Mkubwa, Maisha yanaanza paleunazaliwa na kuisha pale unapofariki. Hivyo kuwa na miaka 40 sio kigezo cha kukufanya ukate tamaa ya kupambana kutafuta hela, Unaweza ukaoa ukiwa na miaka 40 na bado ukaja kuwa na familia njema tu na furaha. Kitu ambacho katika miaka ya karibuni nimekua nikikiona kama ulemavu wa akili hasa kwa vijana wale wanaodai hawana ajira hivyo mambo yao hayaendi au wanaona kama future yao imevurigika. Niseme tu, kwa mtizamo wangu, ajira sio suluhu au tiketi ya kuchomoka kimaisha. Ajira ni ticket ya kuwa na uhakika wa kula na kunywa basi na sio zaidi ya hapo. Ukitaka uhakika mwingine zaidi inabidi uwaze nje ya Box.
Kwangu mimi, ajira hasa za serikali ( in exception of Higher Positions) ni utumwa na limbwata ambalo wengi wameshikika kweli kweli na limbwata hilo limekolezwa na urahisi wa kupata mikopo. Watumishi wengi wa serikali wapo kwenye circle ambayo mimi naiita Rat Race Trap (RRT) ambayo ni Working hard, Earn and Spend. So mtu aliyepo mtaani na hana ajira awaze tu nje ya Box, ajifunze skill yoyote huko mtandaoni. Atafute kakibarua hata kwenye kupandisha zege kwenye majumba akibahatika ku save 500k anunue Laptop pale kariakoo alfu apambane tena ku save anunue Simu yenye uwezo mzuri wa Kamera aanze na content creation ambazo zinaweza kua Faceless au za kuonekana. Anaweza asianze kupata hela miezi ya mwanzo ila baada ya Miezi sita anaweza akawa anatengeneza Hela nzuri kuliko hata hawa waliochomekea na vitambi wanaolipwa 500k take home. Kwa hiyo, nimtie moyo huyu mwamba awaze nje ya box ataacha kuziwaza ajira za Serikali.
Wanaonufaika na Ajira ni wale wenye nafasi za njuu ila hawa wa Chini ni Shida tupu, watu wanatembea wananuka madeni wakishindana kusomesha watoto kwenye ahule za gharama kubwa kuliko vipato vyao.
That's true
 
Huwa sijui kwanini watu wanaogopa kuitwa wazee,uzee ni sifa kubwa sana basi watu hawajui tu

BInafsi nafurahia uzee nilinao,na hizi mvi kichwani kwangu yani shikamoo kama zote
Uwa ni woga tu wa baadhi ya watu,ndo hawa kila mwaka hushusha umri wao huko serikalini,eti ili waendelee kula bata,!!,wakati kimwonekano unaona kabisa njema ishazeeka!!
 
Uwa ni woga tu wa baadhi ya watu,ndo hawa kila mwaka hushusha umri wao huko serikalini,eti ili waendelee kula bata,!!,wakati kimwonekano unaona kabisa njema ishazeeka!!
Ni upuuzi tu ujue,kuna watu nawajua kazi yao ni kuweka super black daily ili waonekane vijana,hauwezi kusimamisha asili,utuu uzima utaonekana tu

Hawa ni watu ambao hawataki kukubali ukweli kuwa umri daima unaenda mbele na haurudi nyuma
 
My Friends, ladies and gentlemen,
Heri ya mwaka mpya 2025.

Kama hoja ilivyo wazi hapo mezani,
nini mawaidha yako mwaka huu mpya wa 2025, kwa vijana graduates wa kike na wa kiume wa umri ambao nimeuanisha hapo juu, ambao bado wanaishi kwa wazazi wao, hawajaoa wala hajaolewa?

Kumbuka pia kijana hana ajira, biashara wala hajishughulishi na chochote, huku umri wa kuajiriwa nao unamtupa mkono kimasihara masihara tu.

Nimeonelea ni muhimu kusaidiana kwa mawazo na matendo, na zaidi sana kuaambiana ukweli, lakini pia kuonyeshana njia muafaka ya kutoka kwenye huo mkwamo wa kifedhea wa maisha wanayopitia.

Kumbuka, kijana akiambiwa suala la mchango tu, baada ya kuplage anazima na simu kabisa maana ni mtu mzima lakini hana jambo lolote kiuchumi.

Ni upi ushauri wako kwa vijana katika msimu huu wa kilimo na mwaka mpya2025?🐒

Mungu Ibarki Tanzania
Tuanze nakuwaambia 40 sio kijana tena ni umri wa kufikiria kustaafu kwa hiarii
 
Back
Top Bottom