Unamtaka nani humu, muwe naye kwenye mahusiano?

Unamtaka nani humu, muwe naye kwenye mahusiano?

Nani huyo mwana JKT anakutuma maua yeye mwenyewe hajitokezi...????!!
Habari za jumapili,

Nahema kwanza maana! Maelezo marefu ila ntajitahidi kuyafupisha.

Jordan, mhusika leo ni Jordan. Huyu tulikuwa wote kombania moja 832kj Ruvu kwa miezi 3. Enzi zile jeshini ni lazima na unaenda kwa kipindi cha mwaka mmoja, na ndani ya mwaka mmoja unaweza ukahamishwa kutoka kikosi kimoja kwenda kingine kwa sababu kadha wa kadha.

Nakumbuka nilianzia makutupora na miezi mitatu ya mwisho nilimalizia hapo ruvu.

Jordan alikuwa sulule mwenzangu, alikuwa anapenda sana mziki kucheza na kuimba. Nakumbuka tukiwa tunakaribia kumaliza jeshi siku moja jioni alichukua mike na kuanza kuimba na akasema wimbo huu namuimbia sulule mwenzangu jina kapuni. Ila macho yote yalikuwa kwangu kipindi chote anaimba na kesho yake tukiwa tunachimba handaki aliniambia Kasie ule wimbo ni ombi langu kwako, niko tayari kutumika maisha yangu yote kwa ajili yako. Aidha tujaaliwe watoto ama tusijaliwe, wewe ndo chachu ya mimi kupambana kiume.

Nilikuwa nacheka tuu na kuchukulia mizaha hadi tukamaliza jeshi kila mtu akasambaratika kwake.

Jana sasa, nilikuwa na upako wa kwenda mziki, nikaenda mahala wanapiga live band na kuimba nyimbo zile za zamani. Nikawa kila wimbo nanyanyuka kucheza na nilikuwa pekeyangu, tabia mbaya na nzuri ya wanaume wa Dar wakimuona mwanamke yuko pekeyake basi wanajua ametega anatafuta kuvuliwa. Nikawa wengine nakubali kucheza nao wengine nakataa nacheza mwenyewe tuu.

Saa isiyo na jina nasikia sauti ya tofauti kwenye kipaza sauti kugeuka jukwaani ni Jordan looh..... ananiimbia..... huku akinitizama....

Naomba lao nipate nafasi.

Niliishiwa stimu zote, nikajikuta nasimama sikucheza bali nilirudi kwenye kiti na kumuangalia mwanzo mwisho anavyoimba. Alipomaliza alikuja kukaa kwenye kiti changu, tukasalimiana nikamwambia naomba niondoke, akaniambia iwapo tuu utanikubalia ombi langu la kunipa nafasi kwenye moyo wako.




Jordan alioa akapata watoto 2, ambao saa hizi wote wako chuo ila mkewe alifariki baada ya kujifungua mtoto wake mdogo na tangu hapo alijikita kulea wanae hakuoa. Akaniambia watoto wake walipoingia chuo tuu akamuomba mungu ampe mwanamke wa kuzeeka nae. Ni mwezi sasa tangu aanze kuomba na jana kaonana na mimi, anaamini Mungu kamuonesha mimi ndo wa kuzeeka nae.....

Jordan, Jordan, Jordan.....
Ni kitambo kirefuu tangu tupotezane 832kj ruvu, Moyoni naumia eeehhhh...


Hata sielewi........... ila kama ni mpango wa Mungu, itakuwa tuu.

Kasinde Mahaba.
 
Back
Top Bottom