Mimi
Gily naandika talaka hii kwa mpenzi wangu
Leejay49 tarehe 27/4/2023. Ya kwamba kwa dhati ya moyo wangu nimeamua kukuacha na kuvunja ndoa yetu ambayo uliifanya kuwa ndoano!
kwa kushindwa kutimiza mahitaji yangu ya kindoa mfano kuninyima unyumba na kunipikia uji wenye mabuja makubwa ya kunikaba hadi kulazwa na nilivyokuonya hukuacha tabia zako hizo. Kunipikia wali ukautia ndimu tangia lini wali ukatiwa ndimu. Kutaka gari vitz wakati kwenye ukoo wetu aliyenunua gari ni yule baba mdogo anayechukua watu misukule!.
Hivyo basi kuanzia leo mimi na wewe sio wanandoa tena na naomba muumba anjijaalie nisikukumbuke tena Wala nisiwaze kupasha kiporo. Hata ukinipa kiporo nakisusa kitakuwa kimechacha kutokana na tabia ya
Half american kula bila kunawa mikono na kulamba sana vidole vyake bila sababu ya msingi. .
Barua hii naituma kupitia washenga wangu
Johnnie Walker,
Binadamu Mtakatifu na
mshamba_hachekwi . Pia nakukumbusha tu kuanzia leo sina ujamaa na wewe mwambie mjomba wako
Analyse na shangazi yako
Lenie warudishe hela yangu niliyowaazima sikukuu ya eid. La sivyo tutakutana mahakamani. .
La msingi sijazaa na wewe
Leejay49 maana ningepata watoto wa kenge kama ulivyo mama yaoπ
View attachment 2601246