Unamuondoleaje mtu hofu ya vitu kama wadudu

Unamuondoleaje mtu hofu ya vitu kama wadudu

Mawazo hapana hana.
Matukio ya nyuma hapana.

Yaani ni hofu tu kuona wadudu hao madude madude kama aliyopost mdau hapo. Hata mimi yananisisimua. Ila sio kwa kiwango kama chake ndio maana namuelewa anavyojihisi..
Yaani yanakusimumua tu ili hali hata ukimuuliza kwani unahisije huwezi kuwa na jibu. Yanatakudhuru hapana.
Basi suala la adrenaline response to fear.
Hilo mzee waone wataalamu ofisini kwao.
Watu tusije tukakudanganya humu.
 
Mmoja wala sio ishu angalia picha pia kama zimepostiwa hapo.
Hapo inatumika njia Moja kuua hiyo phorbia! Sio lazima umshikishe wadudu wote duniani Ila itamfanya awe na general concept ya wadudu wote kutibu phorbia aliyo nayo! Njia ya pili aende Kwa Mtaalam wa wildlife ampe positive life ya HAO wadudu nk japo hii am not much sure! Kuna negative concept anayo kuhusu HAO wadudu
Mfano mi sipendi Sana nyoka ila nilivyokuja kujua positive life ya nyoka na nini huwa wanamaanisha niliacha Kabisa kuchukia nyoka na hata nikimuona naweza muacha aende anakokwenda! Tumeaminishwa na vitabu vya "Mungu"kwamba nyoka ni viumbe hatari Sana na tukiwaona tuwaponde vichwa kbs kitu kilichopelekea reaction ya miili yetu kuanza kuleta effect chemically kwenye miili yetu Ila ukienda Kwa wamisri nyoka ni ishara nzuri Sana, wisdom,utukufu na maarifa,nyoka kama asingekuwa na maarifa asinge mfundisha Eve maarifa ya kuhusu tunda nk Sasa nini kimejificha nyuma ya Yale maarifa? Bila Shaka kilo Ila Sisi tumeangalia effect Tu ya kile kisehem kidogo cha nyoka na Eva Kula tunda na Sisi kuanza Kuogopa, Musa baada ya kuanza kutumia fimbo kama nyoka baada Tu ya kuja Misri ndio alipoanza kufunuliwa na kupewa utukufu na hatimaye kuwaongoza wenzie kwenda kwenye nchi ya ahadi Kwa culture ya wamisri nyoka ni alama kubwa Sana na njema!
Kuna phorbia zinatuumiza Kwa kuwa vitu husika vinaelezewa vby kwenye jamii Fulani ya watu Ila ukienda sehem watu wanavielezea vile vitu vzr wala watu hawawezi pata phorbia ya kitu husika!
Umeshawah kutana na watu ngono kwao sio dhambi? Kwa hiyo sio rahisi wakakusema vby baada ya wewe kupata ukimwi! Hiyo ni mfano kukusogeza kwenye ukweli
 
Entomophobia hiyo

Mm nina fear of height Acrophobia
yaan nikae sehemu juu ghorofani siwezi angalia chini naogopa nahisi nitaanguka

kila binadamu anaPHOBIA yake ndo maana samson pamoja na yote alisanda kwa Delilah

It's normal ni nature hata wewe unaPHOBIA yako ndo mana unashangaa wengine wanafanya kitu fulani lakini wewe huwezi

Hvyo ni kuwa nae karibu na kumfanya afeel safe akiwa na wewe
 
Inategemea mkuu ilisababishwa na nini.Maana phobia husababishwa na sababu kama;
1)Matukio ulopitia kulingana na unachokiogopa kama kung'atwa na wadudu n.k.
2)Hali za genetiki,
3)Mawazo kupitiliza.
4)Hali ya adrenaline response to fear.
Sasa hapa physician anakutibu kulingana na sababu.
Je shemeji yetu kwa mtoa mada yupo kundi gani??
Ni kweli unachosema mkuu lakini generally lazima TU concluded kuwa ni tatizo la akili yaani iwe itakavyo kuwa imesababishwa na Nini lakini mwisho tutarudi hapo tu kuwa ni shida hiyo
 
Hizi shule zinawaharibu sana kijana....
Yaani siku ukija niambia huo upuuzi jitakutandika khelbu hadi utasahau hicho kingereza chenu yenye mnaita sijui "ohh inisekiti ferari"...😠
Tuliza kipago. Utaliwa kavu kavu bi mdogo
 
Nilikua na hiyo shida mpaka natoka vipele kama vya barid
Majan yakiwa kama na vinundu nundu, miti ilotoboka hao wadudu ndo usiseme sijui imepunguaje
Saii naweza kutizama mwili usisimkwe saana.
Hadi usiku nilikua naota
Kama majongoo yanavyotembea nikiona lazima niteseke kulala
 
Sipatani na dudu washa tena likiwa linatembea ndo balaa, nakumbuka wakati nikiwa mdogo miaka 6-8 hapo tulipokuwa tunaishi tulivamiwa na madudu washa kwenye kuta za nyumba nadhani tatizo nililipatia hapo, kinyonga pia simtaki au jongoo ila dudu washa ni zaidi
 
Mimi pia ninayo but silii ila mwili unawasha,nimejaribu kutafuta suluhisho mtandaoni nimeshindwa...mimi hadi zile gif zinafanya mwili unasisimka,nikiwa nachat na mtu nampa taadhali asinitumie,...
 
Back
Top Bottom