Elections 2010 Unamuunga mkono Dr. Slaa kugombea URAIS mwaka 2010? Jiandikishe hapa

hiyo list vipi mbona iko vile vile tuuuuuuuu!!!!?????????????????????????????????
 
ila sijapata logic behind kuhusu uamuzi wa Chadema kumsimamisha Slaa, why hawaja-support other opposition party candidate e,g. Lipumba. naona vile ikitoea akakosa uraisi tutammiss sana bungeni huyu mbunge maridhawa mtu wa watu!!
hata hivyo hongera Dr. Slaa
 
Mi tayari nimesha elimisha ndugu zangu 50 kijijini leo umuhimu wa kutumbukiza kura kwa Dr.Slaa.
 
Mimi naona hii ni serious miscalculation. Dr Slaa ametufaa sana katika nchi hii katika nafasi ya ubunge. Nina uhakika mchango wake baada ya uchaguzi huu utakuwa mchango finyu sana na tena usio na nguvu yoyote maana atakuwa anazungumza kama mgombea urais aliyeshindwa, atakachosema itahesabiwa ni 'maneno ya mkosaji', na ataingia rasmi katika fungu la 'wapuuzwa' akina Mrema, Lipumba etc. What a wrong move ya kutusababisha kumkosa Dr Slaa bungeni! Yaani hapo tutakosa vyote, urais hapati na ubunge keshautema! Too bad! I am mourning!
 
Wanasema mji ni watu. Hapa mie hongera kwa kweli naona bado. Wanaostahili hongera ni wale wote walijiandikisha tangu mwanzo kuanza kushinikiza Dr. Slaa agombee. Nina imani kabisa kuwa katika mawazo yake, basi aliwakumbuka na hawa watu 94+yeye wa JF kuwa na wao wanamtaka na JESHI hilo lipo tayari kuandaa wapiganaji wengine wengi huko mbeleni.

Mpambano ndiyo unaanza. Siku tukimaliza kazi naona ndiyo utakuwa wakati mwanana wa KUPONGEZANA,

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
:target:Hongera sana Sikonge. Hatimae watanzania angalau tuna matumaini tena na kauli za kusema ni lazima tuwe na JK miaka mingine mitano ziishie hapohapo. Yanawezekana watanzania tukafanya U-turn. Nothing for granted.
 
Kimsingi mimi namkubali Dr. Slaa, lakini kwa miaka hii mitano tu kafanya ya kuosha bale mjengoni. hebu tumwache naye hiimiaka mitano naye afanye mambo then baada ya hapo ndo tumpe nafasi hiyo.
Lakini kwa sasa tutakuwa tunamuuza kisiasa kama siyo kumpoteza kabisa. CCM sasa hivi wanashangilia sana na itafika mda wannchi wataona hii hali ngumuu na wataamua tu waachane nayo. kwa sasa wadanganyika wameongezeka kiasi kikubwa sana na ukimpeleka mtu mwenye calibre kama ya DR Slaa tutamkosea haki. kwanza Upinzani waanze mapema kujitandaza kwenye majimbo yote na halafu ndo wampeleke kafara Dr. wa watu.
 
Wandugu zangu,
Hapa ni kujiandikisha tu na hatujadili kitu kingine zaidi ya KUJIANDIKISHA kwenye listi.
Kama unaona HAFAI na au ATAPOTEZA ubunge, basi kuna thread wanajadili hayo. Huko kuna maelezo ya kutosha kwa nini wengine wanaona kuwa INAFAA agombee Urais bila ya kujali atapoteza au hatapoteza. Hapa watu hawaingii kusoma maelezo yenu. Sanasana wanaishia ukurasa wa kwanza kuangalia wamefika watu wangapi.

 
Mkuu Fidel80,

Safi sana na HONGERA kwa kazi unayoifanya. Hii ndiyo ninasema kuwa muda umefika kwa WASOMI wa Tanzania (achana na Vihiyo na wale waliosoma bila kuelimika) kuanza kutumia elimu yao kubadili maisha yao. Kitendo cha Waalimu wazima Wa Vyuo Vikuu kuwa wamenunuliwa na Wanasiasa ambao wengine hata form six hawakufika, inakuwa AIBU SANA.

Muda umefika wa Walimu wa Chuo kikuu kuwa walimu na siyo Madereva wa daladala au Wafuga kuku/ngo'ombe wa maziwa.
Muda umefika wa akina mama waanze kuzaa kama binadamu wa karne ya 21 na siyo kama kuku pale Temeke.
Muda umefika wa Watanzania kupika kwa kutumia Gas yao na si kumaliza miti inayozidi kupungua Tanzania.
Muda umefika Watanzania kuanza kutumika AKILI, VIPAJI na UWEZO wao waliopewa na Mungu.
Muda umefika ........................ Yako mengi sana.

Tukae chini na tuanze kujadili jinsi ya kufanya KAMPENI ambayo haijawahi kufanyika Tanzania. Watanzania wakiona hii kampeni basi wanaanza kulia na kutokwa machozi na kujiuliza, ilikuwaje wakawa WATUMWA wa kujitakia chini ya CCM kwa miaka 50? Nina imani Dr.Slaa atakuwa na sisi kusikiliza mawazo na maoni yetu ili kempeni ifanyike ya KUUWA mtu.

Kijiji changu nina imani wengi watamchagua maana ntaanza kampeni ya nyumba kwa nyumba. Ndugu kwa ndugu na hadi hapa Wilayani Sikonge kieleweke.
MUNGU IBARIKI TANZANIA. DR SLAA FOR PRESIDENT 2010.
Mi tayari nimesha elimisha ndugu zangu 50 kijijini leo umuhimu wa kutumbukiza kura kwa Dr.Slaa.
 
Mtwa, sasa unapokuja na kuweka maelezo marefu wakati nimeomba UJIANDIKISHE tu jina, nashindwa kuelewa unataka nikuandike au nisikuandike. Kama unapinga au una maelezo yoyote, basi nenda kwenye ule mjadala mwingine. Hapa watu wanakuja kuandika majina yao au kuelezea wamekusanya wapiga kura wa Slaa wangapi. Hapa tupo wale TUNAOUNGA MKONO tu. Kama kuna mwenye KUPINGA au ANAPINGA na KUUNGA mkono basi itakuwa VEMA mkijikusanya na kuweka listi yenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…