Wahenga walisema mapenzi yanatia upofu.
Si kwamba mtu hataki kuona kwingine ila kwa wakati huo macho yametiwa upofu na moyo umegubikwa na shahuku ya mtu mmoja aliyepita maishani.
Kupenda na kusahau na kuanza upya kupenda tena sio kazi rahisi na sio kila mtu anaweza. Ni wachache sana wanaweza hii kitu na ni watu imara sana kiakili na kiroho pia, ila bado utaona impact yake pale anapopitia hayo, utamkuta anaconcentrate sana kwenye kitu fulani kisichohusu mapenzi ili kuweka akili sawa. Tunawaita strong people na ni wachache sana.
Kuna watu wana hisia kali sana na wakipenda wamependa, wanafia hapo, wanaoza hapo na wananuka hapohapo. Mioyo yao inakua haijui kingine na wakati mwingine aliyependwa akiwa mtu mwenye makusudi, tendo lake moja laweza kusababisha mwenza kusitisha maisha. Hii ndio inasababisha yale uliyowahi kusikia kuwa amejinyonga kisa mapenzi.
Ukiona mtu kapenda leo kaacha au kaachwa halafu ndani ya wiki moja kapenda mwingine huyo hajapenda kule kunakoitwa kupenda, kutakua na kitu fulani tu alikipenda.
Wanaojua kupenda, hasa wakina dada, wanaelewa ninachomaanisha. Wanaume wachache wako hivi na wakisalitiwa hali huwa ni tete kwa mtu mwenyewe na wengine inaathiri hata maisha yao ya kimapenzi baadae.
Haya mapenzi haya, yaache tu kama yalivyo, kila mtu ana staili yake na namna yake.