Unamzungumziaje mchambuzi Geoff Lea

Unamzungumziaje mchambuzi Geoff Lea

Alexander Lukashenko

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2017
Posts
4,140
Reaction score
9,667
Kuna kikundi cha waandishi kimeibuka, na wanapenda watambulike kama wasema kweli. Lakini kila nikitazama niuone huo ukweli siupati naona ni majungu na chuki tu.
Kwa leo tuanze na huyu GEOF LEA.

Huyu kijana sijui ana shida gani, ni mjuaji hakuna mfano. Bwana Geof lea anaamini kuwa ukosoaji kila kitu ndio kuonesha wewe ni mwerevu na mjuvi wa mambo.

Msimu uliopita alitoa kauli kwamba, haoni simba akifika mahala na beki ile,Mungu si athumani Simba anamaliza makundi amefungwa Goli mbili tu.

Amefikia hatua ya kuanza kusema eti simba na yanga zinatumia Nguvu kubwa kujaza uwanja, na wala sio kwamba mpira unapendwa Tanzania.( hii akizipinga page na wachambuzi wa nje).

Yapo mengi juu ya huyu kijana, naamiini kama na wewe umekutana nayo utasema.

Kama bado hujaona unaweza fuatilia tweet zake.

NB:Hatukatai ukosoaji ila hatutaki Ujuaji.

Screenshot_20210921-122754_Twitter.jpg
 
Aliwai kusema mwaka jana kwa ulinzi huu wa Simba siwaoni wakifika mbali CAFCL,akiwa dis zaidi babu Onyango na mzee Wawa.

Wachambuzi wengi wa soka awajui ila kwasababu wamepata nafasi ndo wanatomboka tu.
Rick Abdallah ndo bingwa wa kuchambua soka na mwengine kidoogo ni Farhan Kihamo.
 
Aliwai kusema mwaka jana kwa ulinzi huu wa Simba siwaoni wakifika mbali CAFCL,akiwa dis zaidi babu Onyango na mzee Wawa.

Wachambuzi wengi wa soka awajui ila kwasababu wamepata nafasi ndo wanatomboka tu.
Rick Abdallah ndo bingwa wa kuchambua soka na mwengine kidooga ni Farhan Kihamo.
Huyu kijana mie simuelewi, Kila kinachohusu soka la Bongo ye anaponda tu.
Mpaka unajiuliza huyu ana matatizo?

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Katika wachambuzi ambao wana uwezo mdogo ni huyu jamaa hua najiuliza anapataje chance za kuchambua kabumbu kwenye hizi radio zetu ila naona clouds FM walimtema maana uchambuzi wake ni hamna kitu
 
Katika wachambuzi ambao wana uwezo mdogo ni huyu jamaa hua najiuliza anapataje chance za kuchambua kabumbu kwenye hizi radio zetu ila naona clouds FM walimtema maana uchambuzi wake na hamna kitu
Nilidhani ni mimi tu naiona shida, kumbe hata nyie mmekutana na hili swala

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Kuna kikundi cha waandishi kimeibuka, na wanapenda watambulike kama wasema kweli. Lakini kila nikitazama niuone huo ukweli siupati naona ni majungu na chuki tu
Jeff Lea ni mjuaji na mjivuni mno, huwa hata akibishana na wenzake akiona anaelekea kushindwa anaanza kuongea kimombo, sasa hapo mkute mchambuzi Jemedari Said Kazumari anabaki kubung'aa tuu
 
Jeff Lea ni mjuaji na mjivuni mno, huwa hata akibishana na wenzake akiona anaelekea kushindwa anaanza kuongea kimombo, sasa hapo mkute mchambuzi Jemedari Said Kazumari anabaki kubung'aa tuu
Nimecheka sana mkuu, nimekumbuka matukio kadhaa.....alafu nikakumbuka kiingereza cha jemedari said, alichokiandika juzi kwenye birthday yake.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Labda kitendo cha yeye kwa sasa kutokuwa sehemu ya viongozi wa Simba, ndio kinamfanya awe na kijichuki. Ni kama ilivyo kwa Haji.
 
Mchambuzi wangu hapa bongo ni George Ambagile tu, kwanza huwa anajiweka pembeni na hizi siasa za simba na Yanga

Na pili akianza kuzungumza simba na Yanga anaongea as a Coach coz Yupo hatua za awali katika masomo ya ukocha

Hao wengine ni wachumia tumbo tu.
 
Jeff Lea ni mjuaji na mjivuni mno, huwa hata akibishana na wenzake akiona anaelekea kushindwa anaanza kuongea kimombo, sasa hapo mkute mchambuzi Jemedari Said Kazumari anabaki kubung'aa tuu
Kuna kipindi twita alinitukana mimi sina akili na sina hela kwa hiyo kuendelea kubishana na mimi ni kupoteza muda...hata leo naona kuna raia mmoja alikuwa anamwambia yeye ana akili zaidi ndio maana ana followers 20k halafu huyo anayebishana naye ana followers 58 tu🐒
 
Hebu mwenye kapicha kake akatundike kuna wajuzi wa kusoma picha za watu tunaweza kujua mengi kuhusu yeye na kwa nini ana behave hivyo
 
Nimesoma hiyo comment yuko sahihi 100%

Simba na Yanga zinajaza uwanja wa Mkapa kwenye matukio mawili tu

1. Simba/Yanga Day
2. K/Koo Derby

Sisi mashabiki ndio tatizo hapa, kwanini uwanja hatujazi hata kwa 70% tunapocheza na timu kama Ihefu?
 
Back
Top Bottom