Unanishaurije kusafiri peke yangu safari ya km 1000

Kama Mara ya kwanza jitahid sana usifunge vioo vya gari itakusaidia kujua gari inatembea kwa speed gani na wote walio kufa kwenye ajari wakiwa na magari binafsi walifunga vioo kwahiyo waliona gari kama haikimbii na kuongeza speed zaidi siku njema
Asante mkuu
 
Hii gari huwa siisahau ninapoikumbuka huwa inaniuma sana, nilikuja nikanyanganywa tu kwa nguvu na watu, unyonge kitu kibaya sana. Ilinyang'anywa makusudi na watu ikabidi niwaachie. Unajua kuna KUIBIWA na KUNYANG;ANYWA?. Kuibiwa na kunyang'anywa ni vitu viwili tofauti[/QUOTE]

Mkuu embu tuambie ilikuaje mpaka UKANYANG'ANYWA..?
 
Kama Mara ya kwanza jitahid sana usifunge vioo vya gari itakusaidia kujua gari inatembea kwa speed gani na wote walio kufa kwenye ajari wakiwa na magari binafsi walifunga vioo kwahiyo waliona gari kama haikimbii na kuongeza speed zaidi siku njema
Speed gauge haiwezi kumuonesha speed anayokwenda nayo?
 
Ushauri mzuri,ila mm nikienda taratibu ndio nachoka na naweza kusinzia.
Kweli kila mtu na uzoefu wake.
 
Mkuu usimshauri hii kitu ni hatari sana..
Usi mbebe mtu usie mjua hata kama anaonekana malaika kwenye macho yako. Never
 
Hizo 1000km Naziua kwa pikipiki...
 
Uzoefu wangu kwenye safari ndefu ni kujipanga kimawazo na kukata vipandevipande vya urefu wa safari.

Mfano kama ukipita ya Iringa, wazia dar-moro kwanza. Ukifika moro, wazia moro-mikumi. Ukifika mikumi, wazia rwaha mbuyuni hivyohivyo mdogomdogo kitonga, ilula, iringa(ipogolo), mafinga, makambako, njombe, madaba mwisho utastukia uko Songea.

Muhimu katika kila point unayofikia ujitathmin kama bado uko na energy sio lazima usimame. Ila ukihisi mawenge pumzika kidogo. Usingizi wa nusu saa unakuwezesha kabisa kuendesha hata masaa 6 tena bila wenge.

Muhimu kuliko yote. Ukihisi dalili ya usingizi, usilazimishe kuendelea au sijui kunawa, tafuta sehem salama park gari ulale kati ya nusu saa au Saa nzima ukipenda.

Safari njema ndugu
 
Mkuu Mark ii grande ulale njiani kwa km 1000??? Masikhara hayo. Mimi safari yangu ya kwanza nje ya Dar kwenda Iringa na kiMark x changu nimetoka saa moja Iringa nipo saa tano na nipo peke yangu.

Hakikisha tu gari yako iko vizuri, tairi, brakes, fanbelt na vikorombwezo vingine. Pia fungua madirisha kidogo ili usije ukasinzia.
CHA MUHIMU ZAIDI KUWA NA NIDHAMU BARABARANI, uwe unakimbia na gari au unatembea taratibu, nidhamu yako ndo salama yako. Epuka kuovertake ovyo.

Naamini by saa kumi au tisa utakuwa Ruvuma ukitoka Dar saa 12.
 
Mkuu usimshauri hii kitu ni hatari sana..
Usi mbebe mtu usie mjua hata kama anaonekana malaika kwenye macho yako. Never

I tried before and it went well, so, I think ur right!!!! nakubaliana na wewe mkuu!
 
Ukifika jiandae miguu kuvimba na kuuma pamoja na mabega waweza hisi hilo gari ulilibeba mgongoni vilee.
 
Mkuu hapa MASASI mabasi yanaanza kuingia SAA 9 kutoka dar,sasa wewe na huyo mnyama ukianza safari SAA kumi alfajili hapa so utaingia SAA 8kwa mwendo wa kawaida na kupumzika.Hivyo unaweza kulala au kunyooka kabisa,ila zingatia kipande cha MASASI ....songea kuna malori mengi ya dangote ambayo yako rafu sana.By the way hongera kwa kwenda kijijini kwenu na gari binafsi,asikuambie MTU kuna raha yake hasa ukiwa MTU wa misifa .haaaaaa
 


Mkuu wewe uko kama mimi! One man army! Juzi tu hapa nimetembea KM 1600, though huku double lanes inasaidia no worries za kupishana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…