“Unaoa lini?” Ni swali lililoulizwa sana jana Uchagani

Kuna umri ukifika hili swali huwezi kulikwepa na inabidi ukubaliane nalo huwezi kusema watu wakuache na maisha yako, katika hatua za maisha ya mwanadamu ndoa ni moja ya hatua muhimu sana. Ni vile siku hizi maadili yamepungua watu wanapuuzia
Hizi sheria za kijima.

Mtu mzima ana maamuzi yake mwenyewe na kuoa si lazima.
 
Isiwe sizitaki mbichi hizi
 
ajali huwez linganisha na ndoa mkuu
...ndoa inaitaji maandalizi kifkra, kiuchumi na kiafya.
...sasa watu wengi huzani ndoa ni km kununua pikiki yakuwa unaamka tu na hela yako unaenda dukan kununua
...fikiria unaniuliza naoa lini wakat me hata milo mitatu kwang tabu je unazan ntakujibu nn km hatutoishia.........
 
Kuna umri ukifika hili swali huwezi kulikwepa na inabidi ukubaliane nalo huwezi kusema watu wakuache na maisha yako, katika hatua za maisha ya mwanadamu ndoa ni moja ya hatua muhimu sana. Ni vile siku hizi maadili yamepungua watu wanapuuzia
Aliyesema kwamba katika hatua za maisha ya mwanadamu, ndoa ni hatua ya muhimu ni nani?

Kwa misingi ipi?
 
Pia mimi ninapitia hayo masaibu nina miaka 45 na sijaoa,kila nikienda mkoani huwa waniuliza "mwali utaleta lini",huwa nakosa cha kujibu mpaka sai nimeamua kutokwenda mkoani.
Niko mid 30 naulizwa sana hili swali.

Linanikera sio kwamba sitaki kabisa kuoa ila katika mapambano yangu Sasa hivi ndio naanza kula matunda baada ya msoto mkali wa miaka 10+

Nina wanawake wawili.

Nimeacha hata kwenda Kwa ndugu sababu hili swali lazima waulize

Na wengi sio kwamba wananijali kivile ni watu wa mbali hawajui hata ABC zangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…