Kwani kila asiyeoa anapata mtoto? Hivi hujui kuna watu hawataki ndoa na pia hawataki kuzaa au kuzalisha?
Uhuru wa mtu binafsi kwenye mambo yake binafsi ni muhimu sana.
Na si lazima kila mtu ajali ustawi wa jamii, taifa, uongozi bora kwa jinsi unayofikiria wewe.
Mfano, ikiwa kazi ya kugundua dawa ya kansa inataka mtu ayatumie maisha yake yote kuitafuta, asijiingize kwenye kuoa wala kuzaa, na mtu akifanya hivyo, mpaka akapata dawa ya kansa ambayo itaifaidisha dunia nzima, kwa yeye kutooa au kuolewa na kutokuwa na mtoto, huyo naye utamlaumu kuwa hajaoa au kuolewa na hivyo hajathamini ustawi wa jamii, taifa wala uongozi bora?
Unaelewa kuwa unanyanyapaa watu kuwa hawajakamilika mpaka waoe au waolewe na wazae, wakati kuna watu hawajaoa wala kuzaa na wana mchango mkubwa sana hapa duniani?
Haya, ikiwa mtu anajijua yeye ana matatizo ya afya ya kurithisha, na hataki kuwa na mke wala mtoto na kuwapa wengine tabu, huyo naye akikataa kuoa au kuolewa utasema hataki ustawi wa jamii, taifa wala uongozi bora?
Kwa nini mnataka kuwapangia watu maisha na hamtaki waishi kama wanavyotaka wao, kqenye mambo yao?
Mtu akisema hayapendi haya naisha, yamejaa magonjwa, shida , umasikini, na hata ukiwa tajiri ni matatizo tu kika simu unawaza kuulinda utajiri wako usiibiwe, na mwisho wake tunakufa tu wote, hivyo haoni point ya kuoa na kuzaa watoto kuwaleta kwenye dunia hii yenye shida, unawezaje kutaka kumlazimisha aoe na awe na watoto?
Kwa nini mnataka kuleta huu udikteta wa kijamii wa kupangiana maisha?
Kama unapenda kuoa si uoe wewe, kwa nini unamshikia bango na kumuuliziaulizia mwingine aoe kama ni lazima?
Kwani kuoa ni lazima?