“Unaoa lini?” Ni swali lililoulizwa sana jana Uchagani

“Unaoa lini?” Ni swali lililoulizwa sana jana Uchagani

Detachment gives power ....lazima tujifanye hatuwataki mtufukuzie
Kuwa makini maadam, hii principle ilifanya kazi miaka ya nyuma, kwa sasa unaweza poteza mtu muhimu sana kwa kujizungusha zungusha,
 
Unaoa lini? Kwa nini hutaki kuoa?

Hayo maswali hayana tofauti na kufanya mtihani... Sasa mtu unanifanyisha Necta bila sababu za msingi, unanikosesha raha kwa maswali ambayo kukujibu natumia nguvu na akili na sipati faida yoyote...
 
Mimi hainishangazi wewe kutokuoa hadi umri huu kinanishangaza ni hao wanaokuuliza mpaka umri huo wana akili gani?

Miaka 45 mtu anajiandaa kwenda kufa wewe usimshauri namna ya kujiandaa na yajayo ukamletee habari za kuzaa na kulea wajukuu?miaka 45 watu wanajukuu eti ndiyo kwanza umwambie mtu aoe?wana wazimu hao wanaokuuliza.
We jamaa fala sana, umepigaje hapo 😅🤣😂
 
Mkuu umeongea uhalisia tunasumbuliwa na ego, then watu wengi kukosa watu sahihi napo kunachelewesha kufanya maamuzi
Wenye ego ni wale wanaojiona wao wanajua zaidi jamii inatakiwa kuwaje miasi cha kuwalazimisha wengine waishi kama wao wanavyoona.

Hiyo ni zaidi ya ego, hiyo ni God complex.
 
Ukiulizwa tena jibu hivi,"kama ambavyo siijui siku yangu ya kufa ndivyo hivyohivyo siijui siku yangu ya kuoa/kuolewa",Ahsante
 
Kwa wanaume wengi siku hizi akiona upo detached atawaza haupo interested nae, ataacha kukufukuzia, uhusiano hautaanza, mwishowe wote mtasahauliana, cycle itaendelea, hamadi mtu unashtuka 40 hio hapo bila mume wala mke Mallerina
Detachment works better than attachment
Unayosema ni kweli
 
Niko mid 30 naulizwa sana hili swali.

Linanikera sio kwamba sitaki kabisa kuoa ila katika mapambano yangu Sasa hivi ndio naanza kula matunda baada ya msoto mkali wa miaka 10+

Nina wanawake wawili.

Nimeacha hata kwenda Kwa ndugu sababu hili swali lazima waulize

Na wengi sio kwamba wananijali kivile ni watu wa mbali hawajui hata ABC zangu.
Hilo ndo tatizo wanauliza unaoa lini wakati hata hali yako ya kiuchumi hawaijui!!!
 
Back
Top Bottom