Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
Kama wewe ni mwenyeji humu ndani utakuwa na uzoefu mzuri sana juu ya wale wote ambao huwa wanaomba ushauri humu na kile ambacho huwa wanakipata.
Ushauri unapata na kusimangwa juu,si ajabu hapo ulipo unahisi kama uanata kujinyonga kutokana na changamoto zako mbali mbali,sasa unataka kutafuta ndugu zako hapa jf wakufariji au wakupe moyo na njia ya kutoka kwenye changamoto yako hiyo,cha kushangaza ni kwamba hao hao unao wahitaji ndio wa kwanza kukwambia ujinyonge na ukafirie mbali.
Hapa ndio jf bwana,kwa wageni ambao hamna uzoefu na hii nchi ya jf basi habari ndio hiyo,hapa bwana unasemwa,unakandwa vizur tu na unapewa za uso mchana kweupe na members wenzako,kwahiyo unapoamua kuleta shauri lako humu basi jipange kisaikolojia kabisa la sivyo utajuta kwanini hata uliamua kuleta jambo lako humu,yani humu hakuna kulemba.
Kuna watu wamepagawa humu,yani wao muda wote wapo tayar kushambulia kama nyuki walichokozwa kwenye mzinga wao,kwahiyo kuwa tayar kukutana na maswahiba yote haya,kikubwa ni kwamba ukiweza kuishi kwenye jamhuri ya watu wa jf basi utaweza kuishi mahala popote pale duniani.
Nadhani sauti imetosha kabisa mpaka back bencher.
Ni hayo tu!