Unaomba ushauri mtandaoni; upo tayari kukabiliana na usiyoyatarajia?

View attachment 3610698

Kama wewe ni mwenyeji humu ndani utakuwa na uzoefu mzuri sana juu ya wale wote ambao huwa wanaomba ushauri humu na kile ambacho huwa wanakipata.

Ushauri unapata na kusimangwa juu,si ajabu hapo ulipo unahisi kama uanata kujinyonga kutokana na changamoto zako mbali mbali,sasa unataka kutafuta ndugu zako hapa jf wakufariji au wakupe moyo na njia ya kutoka kwenye changamoto yako hiyo,cha kushangaza ni kwamba hao hao unao wahitaji ndio wa kwanza kukwambia ujinyonge na ukafirie mbali.

Hapa ndio jf bwana,kwa wageni ambao hamna uzoefu na hii nchi ya jf basi habari ndio hiyo,hapa bwana unasemwa,unakandwa vizur tu na unapewa za uso mchana kweupe na members wenzako,kwahiyo unapoamua kuleta shauri lako humu basi jipange kisaikolojia kabisa la sivyo utajuta kwanini hata uliamua kuleta jambo lako humu,yani humu hakuna kulemba.

Kuna watu wamepagawa humu,yani wao muda wote wapo tayar kushambulia kama nyuki walichokozwa kwenye mzinga wao,kwahiyo kuwa tayar kukutana na maswahiba yote haya,kikubwa ni kwamba ukiweza kuishi kwenye jamhuri ya watu wa jf basi utaweza kuishi mahala popote pale duniani.

Nadhani sauti imetosha kabisa mpaka back bencher.

Ni hayo tu!

JF sio ya mchelemchele,hapa unakandwa mpaka akili zikukae vizuri.

Unataka uambiwe unayotaka kuyasikia,usikaribie JF.

📌AND TO VAYOLENCE,PEACE IS NEVER AN OPTION!!!!

MIKANDO IENDELEE,,,,,
 
Saikolojia inasema kabla hujaomba ushauri akili yako tayari inajua JIBU SAHIHI LA CHANGAMOTO YAKO.

Ila kinachotokea ni mtu anakuwa anapingana na jibu sahihi na anatafuta MAZUZU wa kumshawishi kuliendea JIBU AMBALO ANAJUA FIKA SIO SAHIHI😄😄

📌WAJINGA HAO WAPO NA WATAKUUNGA MIKONO NA MIGUU KATIKA UPUMBAVU UNAOTAKA KUUCHAGUA, ILA TAMBUA NA WEREVU WAPO PIA NA WAO WATAKUPA ZA USO ILI UKAE MSTARI!!!!
 
View attachment 3610698

Kama wewe ni mwenyeji humu ndani utakuwa na uzoefu mzuri sana juu ya wale wote ambao huwa wanaomba ushauri humu na kile ambacho huwa wanakipata.

Ushauri unapata na kusimangwa juu,si ajabu hapo ulipo unahisi kama uanata kujinyonga kutokana na changamoto zako mbali mbali,sasa unataka kutafuta ndugu zako hapa jf wakufariji au wakupe moyo na njia ya kutoka kwenye changamoto yako hiyo,cha kushangaza ni kwamba hao hao unao wahitaji ndio wa kwanza kukwambia ujinyonge na ukafirie mbali.

Hapa ndio jf bwana,kwa wageni ambao hamna uzoefu na hii nchi ya jf basi habari ndio hiyo,hapa bwana unasemwa,unakandwa vizur tu na unapewa za uso mchana kweupe na members wenzako,kwahiyo unapoamua kuleta shauri lako humu basi jipange kisaikolojia kabisa la sivyo utajuta kwanini hata uliamua kuleta jambo lako humu,yani humu hakuna kulemba.

Kuna watu wamepagawa humu,yani wao muda wote wapo tayar kushambulia kama nyuki walichokozwa kwenye mzinga wao,kwahiyo kuwa tayar kukutana na maswahiba yote haya,kikubwa ni kwamba ukiweza kuishi kwenye jamhuri ya watu wa jf basi utaweza kuishi mahala popote pale duniani.

Nadhani sauti imetosha kabisa mpaka back bencher.

Ni hayo tu!
Fact
 
Kuwa makini na shikilia zile comment unazohisi ni za kukupopoa, hizo ndizo zenye kukuambia ukweli. Ushauri hauna mbwembwe, ushauri sahihi umenyooka.
Sasa mfano unalalamika biashara anatokea mtu anakwambia ajira zote hizi wewe unakomaa na biashara jifie zako tu
 
JF kuna watu wa kila aina! Kundi kubwa lina stress na limevurugwa humu. Usitegemee generosity wala positivity kwa kila mtu humu. Unaweza pia mshauri mtu, akakushushia matusi ya nguoni. 😊
 
Back
Top Bottom