Pitia kidogo hapa
1. Pet sematary - imekuwa inspired na Novel ya Steph King. Niliipenda idea yake ya eneo la ajabu ambalo hutumika kuzikia wanyama wa ndani (pets) kisha wanyama hao hurudi kuwa hai tena lakini katika namna ya ajabu kabisa. Shida inakuja pale familia moja ilipoamua kumzika mtoto wao mdogo hapo sababu ya kutokuwa tayari kumpoteza, matokeo yake familia nzima ikajikuta ardhini!
2. The Others - achilia mbali wazo lilizoeleka la nyumba fulani kufuatwa na mizimu na roho za ajabu, humu kilichonifurahisha ni muda wote nlokuwa natazama movie kumbe nilikuwa najiongopea, maana niliyekuwa namdhania ndiye akiteseka na mizimu, kumbe yeye ndiye mzimu wenyewe. Na wale waliokuwa wanadhaniwa ni mizimu ndo binadamu walokuwa wanakuja ndani ya nyumba hiyo.
3. The Orphan - familia moja iliyopoteza mtoto wao kichanga tumboni inaamua kum-adopt yatima wamlelee kama mtoto wao, ajabu ni kwamba mtoto huyo si mtoto bali ni mwanamke mwenye miaka 33 ila kutokana na matatizo ya hormones na pia make-ups amefanikiwa kujiweka kama mtoto. Mbali na hapo, anayeshuhudia mambo ya ajabu anayofanya yatima huyo ni mtoto bubu, kuhadithia hawezi akaeleweka.
4. The sixth sense - hapa mwanasaikolojia wa watoto anahangaika kumsaidia mtoto ambaye anajinasibu kuwa na uwezo wa kuona watu waliokufa. Haamini katika haya mambo lakini baadae anaanza kuamini anachosema.mtoto huyo lakini shida inakuja kwamba, mwanasaikolojia huyo naye alikuwa tayari ameshakufa na ndo mana akawa ana uwezo wa kuzungumza na huyo dogo. [emoji23][emoji23] si mchezo humo!
5. Get Out - nilipenda idea yao ya ku-transform mambo ya racism kwenda kwenye horror ambapo familia moja inamtumia binti yao kama chambo cha kuwavuta wanaume weusi nyumbani kwao ili wapate kuwafanyia surgery na kuwawekea ubongo wa wazungu wazee ama walemavu! Yani humo inaitwa kuingia ni BURE ila kutoka na roho yako sasa ndo KISANGA chenyewe!
6. The Visit - hapa watoto walikwenda kutembelea babu na bibi yao kwa mara ya kwanza kabisa ingali mama akiwa vacation. Watoto hawa wanaona vitu vya ajabu ajabu wakiwa huko. Baadae mama anakuja gundua kuna kitu hakipo sawa baada ya kuona picha za watoto wake na bibi na babu hao wanaoishi nao. Hakuwa anawatambua kama wazazi wake. Hakuwa anawajua kabisa! Na kumbe bibi na babu halisi walishakufa. Hao waliopo ni wagonjwa waliotoroka hospitali ya vichaa!
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using
Jamii Forums mobile app