Nini hujaelewa mkuu? Mbona ipo clear. Bwana mmoja, mwanasayansi wa mambo ya anga, anapewa kazi maalum ya kutafuta makazi mapya ya binadamu baada ya dunia kukumbwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na majanga ya asili kama vile ukame na vimbunga.
Kutokana na majanga hayo kumekuwa hakukaliki hivyo NASA wanafanya namna kutafuta makazi mengine ambayo yatamkidhi binadamu mbali na dunia wanayoishi. Lakini sabb ni hatari kupeleka watu wote kwa mkupuo maana hawana taarifa zaidi kuhusu huko, ndo wanaamua kuwatuma baadhi.
Filamu hii inachanganya kidogo maana inahitaji uelewa wa mambo ya sayansi ya space. Nadhani uliona mambo kama vile wormhole na dimensions. Sasa Wormhole ni njia za kinadharia ambazo zinaaminika zinafupisha safari ndefu za mambo ya anga za juu, yani kama vile shortcuts kwenye space. Na ndo hiyo wanayoitumia wanasayansi hao kufikia huko kwenye ulimwengu mpya wapate kuona kama pataweza kalika.
Sent using
Jamii Forums mobile app