Prodigy Oligarchy
JF-Expert Member
- Mar 21, 2020
- 571
- 653
SteveMollel Hingera kwanuandishi mzuri, na ahsante sana kwa usimukizi wako.
Nawezaje kuzipakua mtandaoni.??
Nawezaje kuzipakua mtandaoni.??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jack Ryan, Designated Survivor, Strike Back, Daredevil, The Blacklist na Blindspot. Anza nazo hizo mkuu.
Ahsante, boss... zote waweza kuzipakua mtandaoni. Pitia YTS tu kwa kupitia u-torrent utadownload upendavyo.SteveMollel Hingera kwanuandishi mzuri, na ahsante sana kwa usimukizi wako.
Nawezaje kuzipakua mtandaoni.??
Mkuu, ulishatazama EXAM?Shukrani sana mkuu nimeimaliza escape room muda huu, bonge moja la muvi....story yake[emoji119] By the way Zoey kazidisha utani wa muvi...
Mzee baba utaiweza astrophysics? [emoji1] [emoji1] au unataka ya juu juu tuHongera mkuu natamani mtu anisimuliee hii movie.kwa sababu naona majanga tu nikiangalia.
Mata watu wanarudi kinyume nyume wakitembeaa daah aiseee.
Ila hakuna mtu au mwalimu anauza CD akifunfisha mambo ya sayansi haya hasa space and time akiyazungumzia au mada mbalimbali za physics ?
Nipate hizo cd niskilize napenda sana kujifunza,nimeamini maisha yana raha ukiwa unajifunza vitu mbalimbali
Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante sana mkuu. Waweza pia kuelewa story lakini ukashindwa kuelewa flow ya matukio ama ukashindwa kuelewa 'signs' zilizokusudiwa au hata namna movie ilivyoishia. Mara nyingi movies huwa na twists mwishoni, mfano TRIANGLE.Mkuu upo vizuri aisee unajua sometimes kuna movies unakuwa nazo ila utamu wa story huujui mfano me nakiri kuna movies kati ya ulizozitaja hapa ninazo ila sikuwahi kujua story zake hivyo mkuu napenda kukwambia ukweli unakipaji cha uandishi hongera sana
Sent from my iPhone using JamiiForums
Sema kwenye ile inayokuja wata mtight washenzi, wameweka chance of survive ndogo sanaShukrani sana mkuu nimeimaliza escape room muda huu, bonge moja la muvi....story yake[emoji119] By the way Zoey kazidisha utani wa muvi...
Hapo umemaliza kwa burudani. Tazama phone booth kisha tukutane tena hapa ...Hapana mkuu nimechukua escape room, phone booth na vivarium
pc
Pamoja boss bila shaka umeona mzgo mpyaPamoja mkuu naendlea kuzioredhesha kwenye notebook yangu then nikipata time nazishusha.
Endelea kutufafanualia kadri upatavyo muda.
Mkuu Safi sna maana wengine ndio ulevi wetu huo movie vitabu...DEVIL ya 2010.
View attachment 1408538
Ushawahi kupitia siku fulani ambayo uliona kila kitu hakiendi poa? Yani upoupo tu, unajihisi mzito, mvivu au unajihisi hauna bahati kabisa siku hiyo? … kheri wewe ndugu. Hiyo tunaita siku mbaya tu, na inaweza ikawa ni kurasa moja tu katika wiki yako ama mwezi au hata mwaka kabisa, lakini ushawahi kusikia SIKU YA SHETANI?
Siku ambayo sio tu mbaya kama unavyosema zile zingine, la hasha! Bali siku ambayo unapigania uhai wako. Siku ambayo unakutana na shetani uso kwa uso akiwa amekubana kwenye kona mbaya haswa. Kona ambayo machaguzi ni mawili tu … kufa ama kupona!
IPO HIVI: Kwa namna siku hii inavyoanza inaonekana ni ya kawaida tu kama jana na juzi ila kiuhalisia ilikuwa ni siku ya shetani kujivinjari. Mwanzoni kabisa bwana mmoja anasikika akisema kuwa mama yake alishawahi kumsimulia kumhusu shetani. Muda mwingine shetani hutembea ndani ya miili ya watu na huwaadhibu mwenyewe wale walio wadhalimu kwa kuwafungia eneo moja kisha kumuua mmoja baada ya mwingine. Na siku ambayo shetani atakuwa katika uzuru wake mahali fulani ishara yake ni mtu kujiua katika eneo hilo.
Ingali jamaa huyo akiendelea kusimulia, ghafla kuna mtu anajiua kwa kujirusha toka kwenye ghorofa ya thelathini na tano ya jengo refu la ofisi ya Philadelphia. Mtu huyo anaangukia juu ya gari na kufa papohapo.
Baadae kidogo katika jengo hilo watu watano wasiofahamiana wanaingia ndani ya lifti na punde lifti inagoma katikati ya sakafu (floors) mbili ya juu na chini hivyo kufanya uwezekano wa kujinusuru kuwa finyu. Wakiwa wamepaniki na kukwazika, security aliyekuwa ndani ya lifti pia anawatoa hofu kuwa si muda mrefu mambo yatakuwa sawa.
Ndani ya lifti hiyo kuna namna za mawasiliano na eneo la kuongozea chombo hicho lakini siku hiyo katika namna ya ajabu, mawasiliano yaliyokuwepo yalikuwa ni ya video tu pasi na sauti. Yani maana yake ni kwamba kilichokuwa kinaendelea ndani ya lifti kilikuwa kinaweza kuonekana lakini sio kusikika!
Sasa kutokana na kile kisa cha mtu kujiua kwa kujitupa toka juu ya ghorofa, kuna mpelelezi mmoja aitwaye Bwana Bowden alipewa kesi hiyo aifanyie kazi. Na kutokana na kwamba mauaji hayo yalitoke katika hili eneo, basi mpelelezi huyo anajikuta akihusika na hili swala la hawa watu waliokwama ndani ya lifti kwa namna moja ama nyingine.
Lakini shida ni kwamba mpelelezi huyu, Bwana Bowden, hakuwa sawa kisaiokolojia. Si muda mrefu sana alikuwa ametoka kumpoteza mke na mtoto wake kwenye ajali. Kutokana na hilo alijikuta akijiingiza kwenye ulevi ulopindukia.
Sasa kwenye macho ya kila mtu, ikiwemo hata mpelelezi mwenyewe, kesi hii ya lifti haikuonekana kubwa sana ya kusumbua akili. Ni ‘system’ tu. Ndivyo walikuwa wanajidanganya. Lakini baada ya mtu mmoja baada ya mwingine kufa ndipo mambo yanapogeuka na kuonekana si utani hata kidogo!
Anayeua hajulikani ni nani lakini ni bayana yupo ndani ya lifti. Kila mtu anamhisi mwenzie. Haijulikani ni nani ni salama kuwa naye pembeni. Hofu inatawala anga. Lakini zaidi kila mtu aliyepo ndani ya lifti siri yake ya uovu inaanza kubainika.
Mpelelezi, Bwana Bowden, ana kazi kubwa ya kuwaokoa watu kabla wote hawajaisha. Ana kazi kubwa ya kumtambua muuaji. Na ana kazi kubwa ya kubeba na kung’amua zile toba za uovu wa wale waliopo ndani ya lifti.
Moja ikiwa inahusiana na kifo cha mkewe na mtoto wake.
NI KISANGA NA NUSU.
2. MARA ya 2018.
View attachment 1408540
Unakumbuka kile kituko ambacho husema hivi ‘unajaribu kulala uyasahau matatizo yako lakini mwishowe unaishia kuyaota!’ Hahah yani hamna kuyakimbia, yanakufuata mpaka ndotoni. Basi kwenye filamu hii ni kheri ukapambana na hayo matatizo yako ukiwa macho maana ukilala tu sio kwamba unayaota bali yanakuua kabisa.
Unakumbuka ile filamu ya A Nightmare on Elm Street? Yule bwana akiwa anawawinda na kuwaua watu wakiwa usingizini kwa njia ya ndoto? Basi filamu hii ya MARA ina mahadhi hayo lakini utofauti wake ni kwamba katika hii ‘bwana mkubwa’ hukupoozesha, yani unaweza ukawa unaona lakini mwili wako wote umepoa, huwezi kufanya lolote lile hata kunyoosha kidole, hapo ndo’ anatokea na kufanya kazi yake pasipo bughudha kabisa … tena huku ukiwa unashuhudia kwa macho yako.
IPO HIVI: Mtoto mdogo aitwaye Sophie anasikia kelele kutoka kwenye chumba wanacholala wazazi wake, ananyanyuka na kwenda kutazama. Huko anakuta baba akiwa amekufa na mama yake analia. Hivyo kutokana na mauaji hayo, mpelelezi, aitwaye Kate, anapewa kufuatilia kesi hii ambayo huonekana kabisa mshukiwa wa kwanza ni mama yake Sophie kwenye mauaji ya mumewe.
Mpelelezi huyu anamfanyia mahojiano mke wa marehemu apate kujua chanzo cha mauaji ya mumewe lakini mwanamke huyu ushirikiano wake ni haba kwa kuona kwamba hataaminika hata akisema yale ya kweli, lakini baadae mwanamke huyu analazimika kusema anachojua baada ya kuahidiwa kumwona mwanae, Sophie.
Anafunguka na kusema mumewe ameuawa na jini wa usingizini ambaye alimkaba mpaka kumtoa uhai wake. Kauli hii inaonekana ni mzaha hivyo basi inapelekea mwanamke huyu kupelekwa kwenye taasisi za watu waliorukwa na akili (asylum) na pia hapewi fursa ya kuonana na mwanae hali inayokuja kupelekea hata kifo cha mtoto, Sophie, baadae kuhusishwa na mpelelezi Kate kwa namna moja ama nyingine.
Sasa kadiri mpelelezi, Kate, anavyozidi kuzama kwenye kutafuta majibu ya kesi hii, ndipo anazidi kuthibitisha yale yaliyokuwa yanasemwa na yule mwanamke kuwa ni kweli baada ya kukutana na jamii ya watu waliokuwa wana ushuhuda na hili jambo ya kuwa kuna mtu anayeua wenzake wakiwa wamepooza usingizini. Jamii hiyo kila mtu ana kisa chake, kila mtu ana majanga yake, na punde tu mmoja wao anajiua kwa kujichoma moto baada ya kushindwa kuvumilia anayoyapitia.
Watu hao wanamweleza mpelelezi huyu kuwa huyo MARA akikutembelea kwa mara ya kwanza anakuachia ishara kwamba upo kwenye orodha, kitone cha damu kwenye jicho. Baada ya ishara hiyo, utapitia hatua ya pili kisha ya tatu ndo’ kifo chako kabisa! Hapo macho yote yakishakuwa mekundu mithili ya nyanya iliyoiva!
Sasa ubaya zaidi unakuja pale ambapo mpelelezi Kate anaanza kuona maruweruwe ya mtu ambaye haonekani. Siku hiyo anapolala na kuamka anajitazama kwenye kioo na kubaini ana alama ya tone la damu! Anahaha. Kile alichokuwa anakisikia kwa wengine sasa kimeshafika kwake. MARA yu mlangoni.
Pale macho yake yanapokuwa mekundu yote sasa anakuwa amefikia hatua ya tatu na mwisho … sasa anapambana apate suluhisho kabla hajalala kwani akifanya hivyo ndo’ utakuwa mwisho wa maisha yake.
innocent dependent Kimatu Prodigy Oligarchy safuher Rubawa Ignas lyamuya Sweta LA Tanzania mkorea mpinyo zipompa kajojo vesta davetz28 troublemaker The Gunners Vladimir Lenin kizaizai miminimkulimaakachekasana Mshuza2 Marvelous King Otorong'ong'o Jitu leusi elly obedy Weylyn