Sweta LA Tanzania
JF-Expert Member
- Aug 31, 2019
- 897
- 2,835
Naomba app ya kudownload mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naomba app ya kudownload mkuu
Umetisha Sana mkuuPitia kidogo hapa
1. Pet sematary - imekuwa inspired na Novel ya Steph King. Niliipenda idea yake ya eneo la ajabu ambalo hutumika kuzikia wanyama wa ndani (pets) kisha wanyama hao hurudi kuwa hai tena lakini katika namna ya ajabu kabisa. Shida inakuja pale familia moja ilipoamua kumzika mtoto wao mdogo hapo sababu ya kutokuwa tayari kumpoteza, matokeo yake familia nzima ikajikuta ardhini!
2. The Others - achilia mbali wazo lilizoeleka la nyumba fulani kufuatwa na mizimu na roho za ajabu, humu kilichonifurahisha ni muda wote nlokuwa natazama movie kumbe nilikuwa najiongopea, maana niliyekuwa namdhania ndiye akiteseka na mizimu, kumbe yeye ndiye mzimu wenyewe. Na wale waliokuwa wanadhaniwa ni mizimu ndo binadamu walokuwa wanakuja ndani ya nyumba hiyo.
3. The Orphan - familia moja iliyopoteza mtoto wao kichanga tumboni inaamua kum-adopt yatima wamlelee kama mtoto wao, ajabu ni kwamba mtoto huyo si mtoto bali ni mwanamke mwenye miaka 33 ila kutokana na matatizo ya hormones na pia make-ups amefanikiwa kujiweka kama mtoto. Mbali na hapo, anayeshuhudia mambo ya ajabu anayofanya yatima huyo ni mtoto bubu, kuhadithia hawezi akaeleweka.
4. The sixth sense - hapa mwanasaikolojia wa watoto anahangaika kumsaidia mtoto ambaye anajinasibu kuwa na uwezo wa kuona watu waliokufa. Haamini katika haya mambo lakini baadae anaanza kuamini anachosema.mtoto huyo lakini shida inakuja kwamba, mwanasaikolojia huyo naye alikuwa tayari ameshakufa na ndo mana akawa ana uwezo wa kuzungumza na huyo dogo. [emoji23][emoji23] si mchezo humo!
5. Get Out - nilipenda idea yao ya ku-transform mambo ya racism kwenda kwenye horror ambapo familia moja inamtumia binti yao kama chambo cha kuwavuta wanaume weusi nyumbani kwao ili wapate kuwafanyia surgery na kuwawekea ubongo wa wazungu wazee ama walemavu! Yani humo inaitwa kuingia ni BURE ila kutoka na roho yako sasa ndo KISANGA chenyewe!
6. The Visit - hapa watoto walikwenda kutembelea babu na bibi yao kwa mara ya kwanza kabisa ingali mama akiwa vacation. Watoto hawa wanaona vitu vya ajabu ajabu wakiwa huko. Baadae mama anakuja gundua kuna kitu hakipo sawa baada ya kuona picha za watoto wake na bibi na babu hao wanaoishi nao. Hakuwa anawatambua kama wazazi wake. Hakuwa anawajua kabisa! Na kumbe bibi na babu halisi walishakufa. Hao waliopo ni wagonjwa waliotoroka hospitali ya vichaa!
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kustream pekee mpaka kudownload
Naomba app ya kudownload mkuu
Hiyo movie inaitwa iron door.Mkuu SteveMollel aina yo movie ulizoziainisha hapo juu ni aina ya movie ninazozipenda sana na kuzikubali, kuna movie naitafuta sana niliiona kama sikosei 2010 iv ila jina nimelisahau ndo mana nashndwa kuipata, movie yenyewe inaanza jamaa anazinduka anajikuta yupo ndani ya chumba kina kabati tu na mzoga wa panya, hakina dirisha, mlango wake ni wa mviringo kama ile ya kuingilia sefu na ukuta ni bonge la zege, baada ya kusota akaiona funguo ya kabati na kufungua na ndani kulikua na mtung wa ges na vifaa vya kutindua ukuta, alifanikiwa kutindua ukuta kwa mbind ila akatokea tena chumba kama kile na kukuta jeneza lina mwanamke ila mzma, alipomshtua akagundua hawaongei lugha moja, ilifika mahali jamaa anakinga mkojo wake na kunywa, hata kale kamzoga alikataman, basi walihangaika sana mwisho jamaa akakata tamaa akaishiwa nguvu kabisa, bdad wakashangaa tu mlango unafunguka wenyewe ndo jamaa kupata na nguv ya kuamka, kama utakua unaifahamu mkuu naomba unitajie jina lake pia.
ni hii hapa iron doorMzee baba mimi mwenyewe ulivyonisimulia nmetaman kuiona. Mbona ina ka-mahadhi ka SAW? Ebu tungoje wadau watujuze.
Pitia pia na post #45 na #112 kuna mizigo mingine
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa simu hapana. Tupia torrents kwa pcNaomba app ya kudownload mkuu
Karibu tena bibie. Hapa umefika. Pitia pia na post #45 na #112 kuna mwendelezo.
Kama unatumia simu, kuna app mwenzetu kapendekeza inaitwa POPCORN TIME. Utaweza ku stream na kupakua pia.Naweza kupata wapi website ambayo ntaweza kudonwnload movie hizo jamaa apo alizokuwa anazielezea
Asante mkuuuKuchek movie au series yoyote kwa simu mbona rahisi sana mkuu! Ingia google tafuta app moja inaitwa popcorn time, I download aizidi ata mb 50.....tafuta movie au series yoyote unayoitaka, unaweza kuistream au kudownload kwa ubora wowote uutakao, yani ni wewe na bando lako tu mkuu