Unapoanzia uchawi ndipo sayansi inapoishia

Unapoanzia uchawi ndipo sayansi inapoishia

Eti kufumba na kufumbua umefika mahala ulipokusidia...zaidi ya supersonic speed....

Hatareee
 
Eti kufumba na kufumbua umefika mahala ulipokusidia...zaidi ya supersonic speed....

Hatareee
giphy.gif
 
Nawazo kwa nn wachawi wasiungane watengeneze usafiri wa chapu ambao utasajiliwa na sumatra alafu wadau tuanze ibukia California tukale bata
Inaonekana watu wengi wahajui uchawi ni nini na nini kinafanyika katika uchawi,hii haiwezekana maana uchawi huhusisha viumbe hai na ili utokee uchawi kuna baadhi ya viumbe hupata madhara unajua ili kupaa kwa mchawi nishati hai hutumika je unajua hiyo nishati inatoka wapi?

Ndio maana wazee zamani walikataa kuoa au kuolewa katika familia yenye uchawi maana uchawi huathiri wanaouzunguka kwanza kabla ya kwenda nje, wa ndani mnakuwa mshaumia kwa kujua au kutokujua.
 
Na uchawi unapoishia ndio Yesu anapoanzia, mfano mtu ameomba damu ya Yesu ifunike nyumba yake, mchawi anakuja usiku anakuta nyumba inawaka Moto wakati watu wapo ndani, anasema huu ni uongo , anaamua kuingia kiinguvu, ghafra anawaka moto na kuteketea, anatoka mbio lakini haisaidii, asubuhi anaamka akiwa marehemu!!
 
Tuanzie na zongo kule Tanga, hii ni aina ya uchawi unaokaa kwenye macho..... Mwenye hili fataki la zongo akikuangalia tu tayari transmission inakuwa imefanyika... Ni mfumo fulani wa wireless communications... Nusu saa kubwa utaanza kuumwa tumbo na kuharisha sana! Tiba yake ni nini? Unga fulani imekaa kama magadi unaitwa MAKATA... ukishakunywa hiyo dakika kumi nyingi umeshapona! SAYANSI hapa ingefanya nini? Ingetumia mlolongo mrefu wa kutengeneza bacteria wenye virus wa ugonjwa wa kuhara... Ingetafutwa njia na kumwambukiza mtu hao virus kisha aanze kuumwa... N baada ya hapo ungeanza mchakato wa matibabu.... Uchawi hauna longolongo zote hizo ni hit n run... Finish.... Na infant wireless transmission theory ni copy n paste toka kwenye uchawi

Mfano wa pili kupaa angani ama kusafiri..
Mchawi ana njia tatu rahisi sana
1.kwa kutumia kifaa kama ungo, fimbo ama ungo. Usafiri wa angani
2. Kutumia mnyama kama fisi nk.. Usafiri wa nchi kavu.
3. Kutumia wireless transmission.. Unajiandaa kisha unafumba macho... Sekunde kadhaa ukifungua umeshafika.. Hii inaitwa serve all purpose.. Mwendokasi wake ni zaidi ya supersonic speed... Kwa usafiri huo kama ni sayansi ingetumia mlolongo mrefu wa kutengeneza ndege magari na vyombo vya majini.. Na ingechukua muda na taratibu nyingi...

Mfano wa tatu.... Kuingia ndani kwa mtu... Kupitia pembe ya nyumba ama chumba chako... Mchawi ana uwezo wa kuingia na kukufanya chochote atakacho na akaondoka salama ukiwa wala hujui ulichifanyiwa.. Utastuka akishaondoka... (Usiwaze popobawa) sayansi haina uwezo huo... Wamejaribu wameshindwa..

Mfano wa NNE fumanizi la kunasiana... Ama kunasishwa mziho au kitu ulichoiba... Hii magnetism theory bado sana sayansi kufika huku....
Sayansi ina limitations nyingi kuliko uchawi.. Sayansi ni ubunifu wa kibinadamu kukopi nguvu asili zisizoonekana lakini zinafanya kazi na matokeo yanaonekana... Inapoishia sayansi ndipo uchawi unapoanzia.. Na kwakuwa sayansi ndio inaiga na kuhawilisha hivyo kamwe haiwezi kutenda kama halisi.....

Tofauti kubwa iliyopo kati ya SAYANSI na UCHAWI ni ITHIBATI... sayansi ina ithibati japo si kwa aslimia miamoja... Uchawi hauna ITHIBATI lakini matokeo yake ni asilimia mia moja.... Sababu ni moja tu... Uchawi una asili ya ulimwengu wa roho... Na ulimwengu wa roho ndio ulianza kabla ya ulimwengu wa macho ulimwengu wa sayansi....
Kiumbaji binadamu ndio kiumbe wa mwisho kuumbwa hivyo hata awe mjuzi na mbunifu Kiasi gani hataweza kufanya kitu kwa mafanikio ya asilimia mia moja bila kugusa ulimwengu wa roho... Ukisoma The mason doctrine utanielewa vema....

Asubuhi njema!

Mbona hizo theory zao wachawi wanashindwa kuzitumia kwenda Lumumba au Kizota au Ikulu au hata benki yoyote hapa nchini ??
 
Na uchawi unapoishia ndio Yesu anapoanzia, mfano mtu ameomba damu ya Yesu ifunike nyumba yake, mchawi anakuja usiku anakuta nyumba inawaka Moto wakati watu wapo ndani, anasema huu ni uongo , anaamua kuingia kiinguvu, ghafra anawaka moto na kuteketea, anatoka mbio lakini haisaidii, asubuhi anaamka akiwa marehemu!!

Yesu yupi ??? Yesu wa Luka au Mathayo ?? au yesu yule ambaye haingii katika ufalme wa Mungu kwa sababu ametoka katika kizazi cha zinaa kama biblia ilivyoandika ??
 
Mbona hizo theory zao wachawi wanashindwa kuzitumia kwenda Lumumba au Kizota au Ikulu au hata benki yoyote hapa nchini ??
Waende wakafanye nini sasa? Mambo mengine bwana ni kujidhalilisha tu mbele za watu.
 
Yesu yupi ??? Yesu wa Luka au Mathayo ?? au yesu yule ambaye haingii katika ufalme wa Mungu kwa sababu ametoka katika kizazi cha zinaa kama biblia ilivyoandika ??
Imeandikwa wapi hayo? We bwana mdogo jitahidi kuficha uchi wa akili yako mbele za watu.

Unajitia aibu sana kwani tunazidi kuuona utupu wako.
 
Imeandikwa wapi hayo? We bwana mdogo jitahidi kuficha uchi wa akili yako mbele za watu.

Unajitia aibu sana kwani tunazidi kuuona utupu wako.

Si useme tu uelimishwe ?? Inawezekana hata biblia yako huijui , Hivyo unavyoandika unajidhihirisha mwisho wa elimu yako
 
Back
Top Bottom