Mshana Jr we si ulisemaga umeacha haya masuala,sasa hizi mada za nini tena?!muone na mawani yake yale[emoji35]
Anyway,niliwahi kukaa na mtu ana macho ya hivyo, kakitazama chakula changu tu aisee niliumwa tumbo wiki mbili,dawa hazifanyi kazi,nikaja kuponea na mafuta ya mzeituni aisee,nilipokunywa tu,tumbo linatoa upepo nusu saa nzima kama tairi inapata pancha ila ndio uzima ukarudi[emoji36]
Yule kijana alinisumbua sana alikuwa mfanyakazi wangu wa ofisini.Alikuwa ana jicho lake fulani hivi akitazama kitu basi panaharibika.
Anaweza kukuambia kitu na kinatokea.Alikuwa anatazama angani anaona kimondo kinashuka,kama kinaelekea upande wako basi una balaa na kweli linatokea.
Nikastuliwa na wasamaria wema,nikamfanyia uchunguzi nikajiridhisha.
Nikatafuta wazee wa dua,tukapiga dua zetu wiki mbili tu,nikaimbaimba zaburi zangu palee,aliaga mwenyewe kaacha kazi na mshahara kauacha,nikitaka kumtumia hataki kupokea hela yangu.[emoji23]
Sijui ndio zongo lile,maana lile jicho lake limenitesa sana,anakutazama unajikuta mlango unakubana vidole puuu,hapo kuna kitu kdogo tu mmepishana.
Aisee wakerewe mna matatizo sana nyie watu![emoji57]