Unapoenda kuabudu kwa kuhani Musa Kimara Temboni zingatia haya

Unapoenda kuabudu kwa kuhani Musa Kimara Temboni zingatia haya

Nadhani Calabash. Ukitoka Mwenge ikiwa unaenda Ubungo,ni kituo cha kwanza tu kiitwacho Mpakani. Upande wa kulia kwako.
Sasa wewe umeelekezwa Kimara Temboni unaleta habari za Mwenge mpakani. Kama hupajui si unanyamaza waumini watoe jografia ya eneo?
 
Iwapo unataka kwenda kuabudu kwa Kuhani Musa lazima uzingatie haya.

1. Hairuhusiwi kupiga picha au kutumia smart phone kwenye ibada.

2. Hairuhusiwi kusinzia ibadani.

3. Hairuhusiwi kuegemea kiti mbele yako.

3. Unapotoa ushuhuda salumu ni Bwana Yesu atukuzwe na sio Bwana Yesu asifiwe.

Kuna wasimamia ibada ambao wanawaangalia waumini wakati wa ibada ili kufata masharti haya.

Ratiba ya Ibada ni Jumanne saa 9 mchana mpaka saa 6 usiku ,Ijumaa muda huo huo.

Jumapili muda kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 2 au 3 usiku.
masharti ya kiganga.
 
Hio ibada gani asubugi hadi sa tatu usiku?

Ndio mnatuharibia ratiba za familia zetu kiukweli

Mtu anaondoka asubuhi kaacha familia hajui inakwendaje sikuhiyo


Sipingi ibada lakini badilisheni ratiba
Ndoa zikivunjika wasiwalaumu wadada wa kazi. Maan waumini wengi hapo ni wanawake
 
Hizo siku za kuabudu ni nyingi na huo muda ni mrefu sana.

Siku ya kuabudu iwe Jpili tu, hizo siku nyingine Watu wakafanye kazi maana ibada sio kazi...Hao anaotaka waende ibadani siku za kazi ni nani atazalisha kwa niaba yao? nani ataijenga nchi kwa niaba yao?.
Hili ungeanza na mwingine anaitwa Mashimo na kundi lake pale stendi ya daladala mbezi mwisho. Wanahubiri kila asubuhi
 
Back
Top Bottom