Unapoona juhudi za kuwapiga chapuo makandarasi wa ndani zimeshika kasi ujue kuna mtu amefungua kampuni lake la ujenzi

Unapoona juhudi za kuwapiga chapuo makandarasi wa ndani zimeshika kasi ujue kuna mtu amefungua kampuni lake la ujenzi

Umaskini ni Mtazamo

Umaskini ni mpangoubongo (mindset)

Umaskini ni ngozi

Umaskini ni vinasaba (genes)

Umaskini ni harufu

Umaskini upo ndani ya watu maskini
 
Wakati wa awamu ya nne tuliona kampeni kubwa za kugawa tenda za ujenzi kwa makandarasi wazawa. Tuliona kampuni ya Mayanga Construction ilivyomwagiwa tenda mpaka ikashindwa na kuishia ku-subcontract kwa makampuni ya nje! Leo tunajua Mayanga Construction ilimilikiwa na nani.

Kampeni za kunyanyua wakandarasi wa ndani sio mbaya ila tu isiwe ni kichaka cha viongozi kutaka kujitajirisha. Tutegemee Abdul Construction safari hii?

Inaweza kuwa JV, rebranding na makolo kolo mengine yote:

F9Nuw_WXYAA3qAr.jpeg
 
Tenda haigawiwi Bali unaomba na Ukiwa na vigezo unapata.

Hata hivyo Kwa Sasa Serikali inachwza fair play Kwa sababu Huwa Kuna Tenda ziko restricted Kwa wakandarasi wa ndani ya Mkoa husika au Wakandarasi wadogo Ili kuleta fairness
wewe naye ni wale wale huna lolote
 
Kwani Kuna shida gani kama Abdul Construction itakuwepo na inafuata taratibu zote za ukandarasi?!
Watanzania tuache utoto utoto na tujue hatuwezi piga hatua kwa kupiga mdomo tu!
Uko sahihi, lakini uzoefu unaonyesha hiyo Nia njema huishia kwa makampuni ya matapeli wasio na uwezo, na makampuni hayo huwa na uhusiano wa Moja kwa Moja na viongozi, kiasi kuwa ngumu kuwawajibisha pindi wanapoharibu kazi.
 
Mtu mwenye cheo kufungua kampuni yake ya ujenzi Wala haihitaji debe Ili kupata kazi.Cheo tuu kinatosha kuwa guarantee ya kazi mfano mzuri ni Robert Gabriel licha ya kuwa RC wa Zamani lakini kapata kazi ya Bil.5 sembuse aliyeko kwenye cheo?.

Pili kwani Kuna ubaya mtu wa hivyo kufungua kampuni na kufanya kazi? Kipi Cha ajabu? Sheria zipi zinazuia?

Kwa hiyo usiwe mpumbavu,Wazawa wanatakiwa kushika uchumi wa Nchi hii ukiwepo wewe ,Makelele hayatakusaidia kuondokana na umaskini.
Hakuna tatizo, lakini wengi wenye vyeo huwa hawajotokezi kwa majina Yao, lakini unakuta ni wamiliki wa hayo makampuni. Na mara zote hayo makampuni Yao yanapoharibu kazi wanatumia vyeo vyao nyuma ya pazia kutetea hasara waliyoleta kwa umma. Huu Uzi ni wa angalizo maana haya mambo yanafahamika. Hivyo usiwe mkali bila kuangalia tafadhari aliyoleta mtoa Uzi.
 
Back
Top Bottom