Unapopokea sifa, omba Mungu wako akupe busara na unyenyekevu, wengi wamepotea kwa kulewa sifa

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
1736078878490.png

1736078841490.png

Adui namba moja wa mwanadamu ni "Sifa"

Sifa ni neno dogo lenye herufi nne, lakini limeumiza, limeangamiza, limeua na limepoteza haiba, roho, nafsi, karama, vipaji na uwezo wa wanadamu wengi sana duniani.

Bila shaka wahenga walijua madhara na athari za sifa, wakaonya kuwa "mgema akisifiwa tembo hulitia maji.” Bila shaka walikuwa wanaonya watu kuwa na tahadhari na sifa.

Nina uhakika, hata wewe umeshuhudia maishani mwako watu waliosifiwa sana, jinsi walivyopotea katika ulimwengu huu pamoja na uwezo mkubwa waliokuwa nao.

Katika mpira wa miguu, mfungaji bora mwenye magoli mengi akilewa sifa, akasahau mchango wa wenzie katika timu na kuona anapata magoli kwa uwezo wake, msimu unaofuata upo uwezekano wa kushindwa kupata japo magoli zaidi ya mbili.

Katika kwaya, wapo waliokuwa na uwezo mzuri na kubarikiwa sauti nzuri kiasi cha kusifiwa na wote. Mtu huyo akianza kuamini kuwa yeye ni zaidi ya kwaya, atapotea haraka sana katika ulimwengu wa waimbaji lakini kwaya itabaki.

Au hamkuona makundi mengi ya muziki Tanzania au Marekani yakivunjika baada ya kila mmoja kujazwa sifa kuwa yeye ndiyo analibeba kundi, wanamshangaa kwanini haendi kujitegemea kimuziki wakati ana uwezo mkubwa, je tunaonaga watu hao wakijitenga kinawatokea nini? Hayo ndiyo madhara ya sifa

Mifano ipo mingi lakini unaweza kufikiri na kuwaza katika eneo lako la kazi hapo ulipo, wenye vipaji na karama kazini wakikumbwa na mtego wa sifa, huwa hawachomoki

Huanza kuona uwezo wao ndiyo umebeba ofisi, halafu huinua mabega na kuvimba vichwa kuwa bila wao ofisi inaweza kufa.

Mwisho kabisa, watu wa namna hiyo hupotea, halafu ofisi huendelea vizuri bila kuonesha upungufu wowote. Tena, mara nyingi, ufanisi wa ofisi huongezeka bila wao.

Ukiona unasifiwa kwa jambo zuri, kazi nzuri na karama uliyopewa mbele ya jamii, omba sana Mungu akupe unyenyekevu wa kujua kuishi na sifa.

Laiti kila mtu angejua sifa zinavyozaa uhasama, kiburi, majivuno kisha zinakumaliza mapema kabla ya kufikia kilele chako cha mafanikio, binadamu wote wangeogopa kusifiwa.

Mimi mtu akinisifia huwa napata wakati mgumu sana, napoteza kujiamini kabisa na ninaishia kuona aibu na kuzikataa sifa rohoni mwangu.

Historia ina namba nzuri ya watu mashuhuri, magwiji na wababe wa kila aina ambao walipotea haraka sana, hawakufaidi hata vipaji vyao na karama zao kwa ulevi wa sifa.

Huwa nashangaa nikisikia mtu anatafuta sifa, huwa najiuliza mtu huyo anajua madhara ya sifa kweli?

Wasomi wa thiolojia wanasema hata kilichomponza Lusifa (Shetani kufukuzwa mbinguni na kutupwa duniani) sababu kubwa ilikuwa ni kulewa sifa.

Isaya 14: 13 - 16 "Wewe ulijisemea moyoni mwako: ‘Nitapanda mpaka mbinguni; nitaweka kiti changu juu ya nyota za Mungu, nitaketi juu ya mlima wakutanapo miungu, huko mbali pande za kaskazini. Nitapanda vilele vya mawingu nitajifanya kuwa sawa na Mungu Mkuu. Lakini umeporomoshwa hadi kuzimu; umeshushwa chini kabisa shimoni. Watakaokuona watakukodolea macho, watakushangaa wakisema: Je, huyu ndiye aliyetetemesha dunia na kuzitikisa falme?”

Kumbe hata shetani alikuwa ni Malaika mwenye uwezo mkubwa, bidii na Jina kubwa, lakini Sifa zilimfanya aone alipo siyo sehemu yake anasthahili zaidi ya pale.

Leo anasubiri moto wa milele.

Omba sana Mungu usikutane na upepo wa sifa na ukijazwa sifa hakikisha sifa azikutoi hapo ulipo.

Ukiona unasifiwa sana iwe kazini,mtaani au mahala popote, tafuta mzizi wa hizo sifa hakikisha unaurudishia mzizi sifa. Kama unapata Sifa kwa kipaji chako ulichopewa na Mungu, hakikisha haraka sana unarudisha sifa hizo na utukufu kwa Mungu aliye kupatia uwezo huo

Na kama ni timu inakufanya usifike, hakikisha unagawana sifa na timu husika iwe katika michezo au Kazini kwako.

Wengi walikosa maarifa ya namna ya kukabiliana na sifa, madhara yake wamepotea haraka katika ulimwengu kabla hawaja faidi matunda ya vipaji, akili au vipawa vyao walivyopewa na Mwenyezi Mungu.

Tupende sifa ila tujue namna ya kukabiliana madhara ya sifa tunazopewa.

Credit: Twitter
 
Credit: Boniphace Jacob
Huyu ni LISU..........................................................................mwenye tabia hii chafu
 
Kwa Lissu sioni sifa, hakuna sheria yoyote inayomkataza kugombea uenyekiti.

Mifano hai yenye anguko baada ya sifa kina Ronaldinho, Yamoto Band, Wakuu wengi wa wilaya / mikoa waliolewa sifa, n.k.
 
Back
Top Bottom