Unapotaka kuhamia sehemu au kununua makazi, kuna umuhimu wa kuangalia aina ya majirani?

Unapotaka kuhamia sehemu au kununua makazi, kuna umuhimu wa kuangalia aina ya majirani?

Unahama kutoa sehemu A kwenda B, kuna umuhimu wa kuangalia utapakana na majirani wa aina gani?? Kabila au dini zao?? Financial status??

I'm just asking.
Pesa yako ndio itaamua utapata jirani wa aina gani. Hivi unafikiri unanunua kiwanja sehemu yenye bei kuanzia 100m kwa 600sqm utakutana na jirani wa hovyo hovyo? Au ununue nyumba huku kwetu mbagala halafu utegemee jirani kama wavMasaki?
 
Jirani ni mtu muhimi sana na kwa bahati nzuri au mbaya jirani humchagui, jirani anajileta na hana mpango wa kuondoka Leo wala kesho kwa hiyo ni vema kuishi na jirani kwa akili sana kwenye matatizo ya ghafula kama misiba , magonjwa, majanga ya moto, wezi nk mtu wa kwanza kukufikia ni jirani yako!
Kinyume chake kama jirani hafai ni janga kubwa kuishi na mtu wa aina hiyo mfano mshirikina, mwizi , mlevi tena wale wa kupiga kelele usiku, wagomvi kila kukicha familia ina migogoro yaani utajuta kwa nini ulijenga hiyo sehemu!
Kuna jirani yangu hapa alinikuta nilishajenga na uwanja wake ulikuwa mdogo baadae tukamsaidia kununua kiwanja kilichokuwq karibu yetu na kwa sababu alikuwa anaishi mbali mara kwa mara tulihakikisha uwanza wake tunaulima kwa gaharama zangu na kupanda mazao ya msimu na akaonekana ni mtu mwema sana !
Baada ya kuhamia huyu jirani hakuna rangi tumeacha kuiona , haipiti miezi hata 3 hajaleta waganga kuja kupiga ramli na kusoma visomo usiku wa manane, nimehuhudia haya maajabu zaidi ya mara 4 akifanya hiyo kuchinja mbuzi zaidi ya 10 unaweza kushangaa unaamka usiku unakuta na harufu za udi huku kuna ndege akitoa sauti za ajabu akizunguka kila kona ya fensi yake huku watu kadhaa wakiendelea kutoa sauti na miguno isiyoeleweka, nilidhani ni mimi peke yangu ndio huwa nasikia hizo mambo kumbe kuna majirani zangu nao pia wanalichukia hilo suala, kwa kweli hii imekuwa kero kubwa kupata kutokea maishani mwangu! Sasa natamani nimfuate nikamueleze huo uhuni na ushirikina wake anaoufanya au nasubiri arudie tena siku hiyo usiku nitamtolea uvivu hatoamini kitakachomkuta maana siku zote tumemkalia kimya! Kuna mengi ya kuandika ila ngoja Nitshie hapa
 
Unahama kutoa sehemu A kwenda B, kuna umuhimu wa kuangalia utapakana na majirani wa aina gani?? Kabila au dini zao?? Financial status??

I'm just asking.
Muhimu Sana maana hayo ndio yataamua mustakabali wa furaha na amani katika maisha yako na majirani
 
Unahama kutoa sehemu A kwenda B, kuna umuhimu wa kuangalia utapakana na majirani wa aina gani?? Kabila au dini zao?? Financial status??

I'm just asking.
Kuna tofauti kati ya MAJIRANI zako na JAMII ya eneo unaloishi

Majirani ni watu unao pakana nao au waliokuzunguka kwenye nyumba yako ambao UTALAZIMIKA kushiriki nao mambo mbalimbali kutokana na ujirani wenu

Jamii inayo kuzunguka ni hulka za watu wanaoishi eneo hilo kwa ujumla wao

Jirani huna ujanja naye..... Unaweza kujenga Masaki na ukapakana na jirani mtata balaa

Kuhusu jamii inayokuzunguka hapo ni swala la FEDHA....... Uzunguni kajenge Masaki Obey nk, Maisha ya kati kajenge Sinza Mwnge Tabata nk. Uswazi kajenge Kwa mtogole vinginguti nk
 
Unahama kutoa sehemu A kwenda B, kuna umuhimu wa kuangalia utapakana na majirani wa aina gani?? Kabila au dini zao?? Financial status??

I'm just asking.
Kuna maeneo ya uswazi fulani..maisha yake raha sana.....labda tuite "uswazi smart".....
 
Pesa ndio inaamua, kule Goba kuna sehemu inaitwa Half London, bila 100m-200m hujapata kiwanja. Unadhani jamii inayoishi humo ni ya aina gani? Njoo sasa uswekeni, wanakata hata 10x10, unategemea ni jamii gani inaishi humo?
 
Muhimu sana zingatia sana
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom