Unapozomewa ni tafsiri watu hawakuheshimu kama unavyofikiria. Hawakuonei haya

Unapozomewa ni tafsiri watu hawakuheshimu kama unavyofikiria. Hawakuonei haya

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Habari za Sabato!

Kuna ile unafikiri watu wanakuheshimu kwa kiwango cha juu. Kiasi kwamba hata ukitema shudu, pumba, ukitoa boko basi watu kwa heshima waliyonayo kwako watakustahi.

Ni kweli mtu anayekuheshimu sana hawezi kukuzomea, kukukatili, kukukatisha, kukufedhehesha. Hilo ni kweli kabisa.

Lakini kuna ile mtu unajiona wa muhimu sana. Kwamba mimi siwezi kuzomewa. Kwa niliyofanya siwezi kuzomewa. Kwa jinsi tulivyo na mahusiano yetu siwezi kumwagiwa majitaka, kupigwa mayai viza.

Sasa kumbe heshima yako sio kubwa kihivyo. Sio kama unavyofikiria, unavyodhani, kama ulivyo jidanganya.

Ndio ile unaongea utopolo, unamwaga ukoko alafu watu hawakukawizi wanakumwagia majitaka. Dadeki!

Sasa kwa vile bado huamini unafikiri labda ni bahati mbaya, unakazana kuzima jaribio la kuzomewa hapo ndipo unaharibu kabisa. Watu wanafungulia Chemba zote za jiji, mwendo wa majitaka unamwagiwa tuu.

Ni muhimu kujua hasa ukiwa kiongozi wa siasa. Heshima uliyonayo sio kubwa kama unavyojidanganya. Heshima ndogo uliyonayo jitahidi uilinde ili aibu za rejareja kama hizo zisikupate.

Usiweke rekodi mbaya kwamba uliwahi kuzomewa mbele ya halaiki, mbele ya media, watu bila kusita walikumwagia majitaka. Kwani hiyo wapinzani wako wa kisiasa wataitumia sana Huko mbeleni kama reference.

Kiufupi ni kujiharibia CV kwamba haikubaliki kivile.

Mtu mwenye kupendwa na kuheshimiwa sana kamwe hawezi kuzomewa. Watu lazima wamvumilie, wamstahi.

Wataishia kusema mzee kazingua lakini sio kwa kummwagia ukoko na majitaka.

Nimemaliza

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Awamu ya 6 wanalazimisha mahaba kwa wananchi ambayo wameyaua wenyewe mioyoni mwa wananchi kwa matendo yao machafu na ya kikatili kwa sababu ya madalaka!!!

Sasa madaraka wameyapata lakini hawa aminiki na wanaodai waliwapigia kura za kutosha!!!

KARIBUNI TUTAFIKA WANAKOTAKA TWENDE.....
 
Mtu anayekupenda na kukuheshimu hawezi kukuzomea kamwe tena mbele ya halaiki. Lazima akustahi.
 
Awamu ya 6 wanalazimisha mahaba kwa wananchi ambayo wameyaua wenyewe mioyoni mwa wananchi kwa matendo yao machafu na ya kikatili kwa sababu ya madalaka!!!

Sasa madaraka wameyapata lakini hawa aminiki na wanaodai waliwapigia kura za kutosha!!!

KARIBUNI TUTAFIKA WANAKOTAKA TWENDE.....
Walivyo wajinga watajibu mapigo. Ki-vipi? Wataandaa hadhara nyingine, watapandikiza ma-chawa wengi. halafu jina la Samia likitajwa, watarukaruka kwa furaha na vigelegele kuonyesha kuwa ''anapendwa''. Serikali ya wapumbavu hii!
 
Sidhani maana Jana inaonekana angepiga Hadi simu ukumbini, ila ndio hivyo mission failed

Lengo la kuburudisha na kuwakutanisha Wasanii wa zamani limefanikiwa ila ajenda ya kumchomeka Mama na serikali yake limedunda live
 
Watoa Fedha a k.a wadhamini wa show,wamekosa airtime na promo,KAZI ishakua ngumu

Mikoani waende kufanya show na sio kulaghai raia

Ishikawa kipengele.
Hapo tricks isingekuwa hiyo.

Kazi za heshima hupewa watu wa heshima.
Hiyo kazi ya kumtaja Rais Samia angepewa Mwijaku au Dotto watu wa kazi cha lawama, kutukanwa kama sehemu ya kupima upepo.

Lakini mtu kama Mwana FA kuwa mtu wa majaribio kwa kazi hiyo tayari rekodi mbaya ameshaiweka. Kuzomewa. Sio jambo dogo katika mambo ya heshima
 
Hahahaha, watoa hela wote Jana wamekosa airtime

😃😃😆
Kumbe hao ndio wadhamini wakuu.
Hatari sana.
Round nyingine wawatumia kina Mwijaku na Dotto wao hizo ndio kazi zao wataweza kuparangana na mashabiki bila kuathirika kwani ndio kazi yao.

Lakini kuwatumia wasanii au viongozi ni kutaka kuwashushia heshima na kuwadhalilisha. Kutawaletea damage
 
Ilitabiriwa 2030 Ccm atakosa kiti Cha uraisi na akijaribu kulazimisha amani itatoweka milele Tanzania, wapo wataoingia msituni

Watu Wana hasira na Ccm na wote walioshiriki kuuliwa Kwa wananchi October 29, ndugu na jamaa zetu wamepoteza uhai Kwa kudhulumiwa

Vyama pinzani vitulie na visimamishe watu sahihi, vikishindwa , rais atatokea mtaani
 
Back
Top Bottom